Nani alimshtua Lowassa?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,197
25,517
Alipogusia kashfa ya Richmond huko Dodoma na kuahidi kuizungumzia zaidi tarehe 30/5/2015 huko Arusha,Lowassa alishaingia kwenye 'kumi na nane' za Dr. Harrison Mwakyembe, Samwel Sitta na waliokuwa wajumbe wa Kamati Teule ya Bunge. Kimsingi, hata Lucas Seleli angeibuka na kumwanika Lowassa. Lowassa angeumbuka mchana kweupe kwa kuwekwa hadharani hata yale yaliyofichwa Bungeni mwaka 2008.

Huko Arusha Lowassa hakuthubutu kuelezea kuhusu kashfa iliyomng'oa kwenye Uwaziri Mkuu ya Richmond kama alivyoahidi Dodoma. Nini kilimshtua? Nani alimshtua? Lowassa atambue kuwa anaishi kwenye nyumba ya vioo na hivyo asichokoze ugomvi wa mawe.
 
Katishia nyau na nafikiri ameona upepo ulivyovuma , na kaamua kuingia mitini.

Ile hotuba yake isivyokuwa na mpangilio ndo dalili za kuchanganyikiwa. Waswahili wanasema hata Abson alikuwa Arusha , ujumbe gani kamfikishia haijulikani.

Umenena ukweli Mkuu
 
Katishia nyau na nafikiri ameona upepo ulivyovuma , na kaamua kuingia mitini.

Ile hotuba yake isivyokuwa na mpangilio ndo dalili za kuchanganyikiwa. Waswahili wanasema hata Abson alikuwa Arusha , ujumbe gani kamfikishia haijulikani.
Abson=Apson?
 
Lowasa anajua kuwa alichemka alipoongea kule Dodoma. Anajua pia uwezo wa Sitta na Mwakyembe jukwaani na hasa juu ya kashfa hii ya richmond
 
CCM inawayawaya, ukizingatia hata huyo Mzee wa standard alivyotuingiza chaka kwenye katiba waliyoipendekeza. Wote watazidi kuigawa CCM vipandevipande kwa vinywa vyao.
 
Kabla ya kukabidhiwa dola, ameanza kwa ahadi hewa, watu tumeacha kujenga taifa tusikie alichotuahidi yeye anaongea maneno ya ajabu ajabu akikolezea neno maamuzi magumu, jamaa wote kelele bila hata kujua kuwa hapo alipo ameshakimbia amuzi gumu alilowaahidi kuwaeleza.

hakuna kitu pale.
 
Hakuna mwenye nafuu wote tunawadai, Mwakyembe tunamdai hayo aliyoyakalia kuiokoa serikali, Samweli Six kwann alikubali yaletwe baadhi na mengine yaachwe, ila mwisho wa sikuu wakiendelea hv ukweli utafahamika na wote watatu tutawaalani na kizazi chao kwa kutuficha ukweli kwa mda wa miaka 7 na hivyo kuwapa uhalali watawala ambao walikuwa wamepoteza uhalali, kwa ufupi wote ni wasakatonge, ingekua China death penalty ilikuwa halali yao wote watatu!!
 
wizi wizi tuu, alikuwa wapi siku zote hizo kama hakuhusika?!

ndio mda aliona unafaa kusema ,kwan aliposema hahusiki si ulielewa alichosema! alikuwa wapi siyo jamb la msing, la maana ni yy kusema alichodhamiria ww uelewe, na uvhambuz wako uanzie hapo!
 
Nionavyo mimi

Lowasa alijua akisema basi mkuu atakuwa anahusika hivyo kusababisha yeye Lowasa kutopita huko CC.
Ameamua kaa kimya ili akipitishwa aseme au akiwa Raisi aseme kilichotokea na kwanini alikuwa kimya

Kati ya watu wenye akili wewe ni mmoja wao.You Great Thinkers big up brother
 
Back
Top Bottom