Clark boots
JF-Expert Member
- Jun 5, 2017
- 6,402
- 5,526
Haya wakulima wenzangu wale, wafanya biashara pia na makampuni mbalimbali katika kuelekea kilele cha siku ya wakulima almaarufu nanenane naomba tutumie uzi huu kupeana updates. Ni kwa namna gani mambo yanazidi kunoga huko viwanjani.
*kanda ya Nyanda za juu kusini - Mbeya
*Kanda ya kusini - Lindi ngongo
*Kanda ya Magharibi
*Kanda ya kaskazini
*Na kanda zote kwa ujumla.
Binafsi nipo Morogoro mji hapa naona mambo yanazidi kunoga jamani mabanda kama yote, makampuni mbalimbali yapo hapa karibuni sana tuje kujifunza mambo mbalimbali kuhusu sekta hii nyeti ya kilimo.
Morogoro standup.
====
SIKUKUU YA KITAIFA YA WAKULIMA/ SIKUKUU YA NANENANE
Nane Nane ni sikukuu ya wakulima nchini Tanzania, inayoadhimisha tarehe 8 mwezi wa 8 kila mwaka ambayo huwapa fursa wakulima, taasisi na wadau mbalimbali wa kilimo kote nchini kuonesha bidhaa zao na mafanikio yao katika mwaka husika
Miaka iliyopita sherehe hizi zilikuwa zikifanywa tarehe saba Julai kila mwaka. Sherehe hii inatayarishwa na kuratibiwa na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kwa kushirikiana na Shirika la Chama cha Kilimo Tanzania ‘TASO’ na kuhusisha Taasisi, Wizara na mtu mmoja mmoja wanaoshughulika na kilimo
Nanenane iliadhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1977 ili kuongezea nguvu sera ya Serikali ya wakati huo ya ‘ Siasa ni Kilimo ‘, ambapo wakulima katika wilaya, mkoa na kitaifa walionesha mazao yao ya kilimo, pembejeo pamoja na kufundishwa namna ya kutumia pembejeo
Maadhimisho haya husherehekewa katika ngazi ya kanda ambapo kanda ya nyanda za juu za kusini zinafanyika viwanja vya John Mwakangale mjini Mbeya. Kwa kanda ya Kaskazini, sherehe zinafanyika viwanja vya Themi, Arusha, wakati kanda ya Mashariki zinafanyika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Morogoro na Kanda ya Ziwa, zinafanyika Mwanza, Viwanja vya Nyamhongolo na Kanda ya mwisho ni kusini, zinafanyika Ngongo