Leo ni 8/8 ,Sikukuu kubwa sana Mkoa wa Mbeya na Songwe

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,785
Kwa wale msiofahamu,Leo ni Sikukuu kubwa sana kwenye Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini hasa Mbeya,Songwe,Iringa na Njombe.

Pia 8/8 inapewa uzito mkubwa kwenye Baadhi ya Mikoa ya Kanda ya Ziwa ambapo watu hununua nguo Mpya na kula vyakula vyenye hadhi ya sherehe kama tuu sherehe zingine za kawaida.

Maeneo mengi ya Nchi hakuna mtu ana habari na 8/8 isipokuwa Nyanda za Juu Kusini.

Kwa kuzingatia ukweli huu,ni vyema Serikali ikaufanya Mkoa wa Mbeya (Nyanda za Juu Kusini) kuwa mwenyeji wa Kudumu wa sherehe za 8/8 Kitaifa kama ilivyo 7/7 Kwa Dar.

Aidha Maonesho yapewe hadhi kubwa ya Kimataifa kama ilivyo 7/7 kama njia ya kuwaenzi Wakulima na Mikoa hii ya Nyanda za Juu ambayo huipa uzito siku hii.

Kuna Maonesho ya Kilimo 8/8 yanaendelea kwenye Kanda zingine lakini hakuna watu wa kwenda kutembelea kama inavyoonekana kwenye Viwanja vya John Mwakangale Uyole Mbeya.

Mwisho Serikali imesema itakuwa na viwanja 2 vya Maonesho ya Kilimo 8/8 Kwa ngazi ya Kimataifa yaani Dodoma na Mbeya ila nashauriwa sherehe za Kitaifa yaani kilele chake kiwe kinafanyika Mbeya.
 
Hapo unaona fahari mwenyewe
 
Back
Top Bottom