Mbunge Condester Sichalwe: Karibuni Mtembelee Banda Letu la Momba NaneNane Mbeya 2023

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

MHE. CONDESTER SICHALWE - "KARIBUNI MTEMBELEE BANDA LETU LA MOMBA NANENANE MBEYA 2023"

Mbunge wa Jimbo la Momba Mkoa wa Songwe, Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe ametembelea Banda la Momba Nanenane Mbeya na kuitumia fursa hiyo kuwaalika watu wote kuona fursa mbalimbali za Kilimo na Mifugo zinazopatikana Jimbo la Momba.

Condester Sichalwe amezungumza na kusema shughuli kubwa za watu wa Momba ni Kilimo na Ufugaji, hivyo amewaomba na kuwakaribisha Watanzania wote kutembelea Banda la Maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) mwaka 2023 zinazofanyika kitaifa Mkoa wa Mbeya.

Mbunge Condester amesema katika Banda la Momba lililopo Nanenane Mbeya watu wataona aina mbalimbali za Mbegu bora kutoka kwa Wataalam wa Kilimo, Mifugo (Kuku, Bata, Nguruwe, Ng'ombe), Maharage, Asali,Korosho, Alizeti, Chumvi, Mazao ya Mbogamboga, Mazao ya Nafaka na Nafaka mbalimbali zinazopatikana katika Jimbo la Momba.

Mbunge Condester amesema watu wataona Mchele mzuri sana unaolimwa kutoka bonde la Kamsamba, Bonde Kasinde, Bonde la Msangano na Chitete kutoka kwenye Skimu ya Umwagiliaji ya Namingong'o katika Banda la Maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane Mbeya 2023.

Mbunge Condester Sichalwe anawakaribisha sana watanzania wote na wawekezaji kuja kuona fursa mbalimbali ili waweze kuwekeza ndani ya Jimbo la Momba.

#FahariYetu
#MombaYetu
#MazaoYetu
#UtajiriYetu


WhatsApp Image 2023-08-05 at 22.28.32(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-08-05 at 22.28.32.jpeg
WhatsApp Image 2023-08-05 at 22.28.29(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-08-05 at 22.28.30.jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-08-05 at 22.28.28.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-05 at 22.28.28.jpeg
    87.1 KB · Views: 6
Back
Top Bottom