Namzimikia sana Faizafoxy!

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Kama kuna kina dada ninaowazimikia humu Jamii Forums.

Basi FaizaFoxy ni nambari wani. Huyu dada kwa kweli ni mjuvi wa Lugha na jasiri wa kutetea hoja zake hata kama ziko Upogo, ni mtamu wa kupanga mtiririko wa mawazo yake Ingawa mawazo yake mengi siyakubali kabisa na ni mtoto wa mjini haswa kwa aina yake ya matumizi ya Lugha.

FaizaFoxy anazo kumbukumbu nyingi kuhusu Kariakoo ingawa natofautiana naye kwenye kuamini kwake kwamba Kariakoo ni ya watu fulani tu. Yaani wale wale kwa miaka nenda miaka rudi,watu wapya wanaoishi Kariakoo hivi sasa kwa FaizaFoxy si wanakariakoo bali ni "wakuja".

FaizaFoxy ananivutia sana na kama tungekutana enzi zile wakati wa Fanifani na fete za Mnazi Mmoja inawezekana kabisa leo hii angekuwa ni Mrs kigarama. FaizaFoxy anautetea sana utu wa mwanamke kwenye kuwakilishwa kijamii na tabia njema kwa wanawake.

Mimi ni mswahili na FaizaFoxy kingine anachonivutia nacho ni uwezo wake wa kuendesha mipasho na kusuta watu kama vile tuko mitaa ya uswazi tunashuhudia muuza mapupu anasutwa na mkusanya skrepa.

Namzimikia Faiza Foxy.
 
Mimi juzi alinishushua ila nilipata funzo kwa kupitia hilo shushuo lake!!
 
Ni kawaida mwanaume kwa mwanaume kuongea lolote lakini sio mwanamke especially mwanamke mwenyewe akishavaa ushungi kichwani

Ushungi unahusiana nini na kuongea?

Nioneshe nilichokukwaza hata unishambulie bila mpango. Unanshangaza! wengi wenu huwa hampendi ukweli na mfumo dume unawafanya muone kuwa wanawake ni watu wa kukaa kimya na hawajui kitu, hiyo inatokana na malezi uliyolelewa nayo.

Wanawake wa Kiislaam tuna rights zetu kwa zaidi ya miaka 1400 leo. Usione ushungi kuwa ni kitu cha ajabu hata ma nun wanauvaa huo, kwanini?
 
Basi nitakula tende za hiyo mitende mipya. Lakini ujuzi hauzeeki!!
 
Ushungi unahusiana nini na kuongea?

Nioneshe nilichokukwaza hata unishambulie bila mpango. Unanshangaza! wengi wenu huwa hampendi ukweli na mfumo dume unawafanya muone kuwa wanawake ni watu wa kukaa kimya na hawajui kitu, hiyo inatokana na malezi uliyolelewa nayo.

Wanawake wa Kiislaam tuna rights zetu kwa zaidi ya miaka 1400 leo. Usione ushungi kuwa ni kitu cha ajabu hata ma nun wanauvaa huo, kwanini?

Ushachokozwa!!
 
Back
Top Bottom