Uchaguzi 2020 CHADEMA na LISSU zingatia haya, ni Muhimu sana kwenu

Nzwangendaba

JF-Expert Member
Nov 9, 2019
501
710
Amani iwe kwenu ndugu wanaJF.

Kwanza kabisa napenda kuchukua nafasi hii kukupapope Mr. Lissu kwa madhira uliyoyapata, kwa ujasiri wa kurudi nyumbani (najua mtu mwingine angeogopa kabisa kurudi kutokana na tukio lile baya), na pia nakupongeza sn kwa kuchaguliwa kwenye Chama chako kushika bendera kwenye Kinyang'anyiro cha urais kwenye uchaguzi wa JMT 2020.

Najua wananchi wengi sana wanakupenda. Huenda sauti za wananchi kwenye kila kona ya nchi hasa mitandaoni, ndio iliyowapa nguvu viongozi wenzio na wajumbe kuona hawana namna ni Kukuchagua wewe Kugombea nafasi hiyo kubwa zaidi.

Nikiwa kama raia mwema, mpenda mema, maendeleo ya nchi yetu, amani, utulivu na mshikamano; nimewiwa kuwashauri haya yafuatayo, ambayo huenda si mimi tu bali wapo wengi wenye mawazo kama yangu, ambayo naamini Chama chenu na muhimu zaidi wewe binafsi mkiyatafakari na kuyafanyia kazi yatawasaidia sana kwenye harakati zenu na za Uchaguzi kwa mafanikio na kuepusha shari nyingi nyepesi nyepesi.

Nisipoteze muda zaidi, ila naomba haraka iwezekanavyo, Chama na wewe Mwenyewe uache haya yafuatayo ili muda huu mchache utengeneze crefibility na Personality nzuri ya Kiongozi Mkubwa wa Kitaifa. Kumbuka kipindi hiki kosa moja linaweza kuwa na impact kubwa sn. Ndio maana wagombea wengi nyakati hizi huwa wapole na wanyenyekevu kwa sababu wanajua wapo jirani na wanafuatiliwa mno na waliowengi.

DON'Ts

1. Binafsi nimesikitishwa sn na kitendo mlichofanya cha kuuchakachua wimbo wa Taifa na kufanya remix ambayo mnaifanya kama ndio wimbo official wa Taifa. Hiki ni kitendo cha uchokozi wa wazi kabisa tena pasipo sababu ya msingi. Kitendo hicho hakioneshi kuwa na impact yyt kwenye sanduku la kura. Hivyo, nawaombeni sn na pengine ulisimamie mwenyewe, Vitendo vya kufanya uchokozi tena kwenye vile vyenye unasaba na sheria na katiba ACHENI MARA MOJA. Epukeni kufanya mambo yyt ya makusudi ambayo yanaweza kuwafanya vyombo mbalimbali kuhangaika na nyinyi kwenye kesi na majibizano mabaya. Kitendo hicho hata wengi miongoni mwa wapenzi wa Chadema hawakukipenda. FANYENI YALIYO YA MSINGI ZAIDI.

2. EPUKA KAULI ZENYE KUTAKA SHARI NA KUIBUA HISIA HASI KWA MAMLAKA ZA SERIKALI. Mfano, kauli ya kusema ngoja tuongeze ubeti mwingine halafu tuone watatufanya nini? Kwa kweli hapo no kujipanga tu kwa shari. Epuka kabisa kauli za namna hii, wanaweza kuhangaika na wewe halafu wakupotezee muda na malengo yaliyopo ya kichama. Dhibiti matumizi yako ya lugha.

3. KUWA MVUMILIVU NA DHIBITI HASIRA
kuna wakati unaonekana mwenye hasira kiasi. Relax na pima jambo kabla hujaliongea. Najua yaliyopita bado yanakupa hasira flani (labda), lakini jidhibiti. Kauli za tutaingia barabarani, nk nk. Kwa sasa acha kwanza. Hasa kipindi hiki kabla ya kuchukua fomu na kabla ya kuanza kampeni. Bora uyaseme baadhi ya haya majukwaani kwenye kampeni, ingawa nako pia busara na kuchunga kauli ni muhimu muda wote. Kumbuka kauli zako nyingi ndio zimepelekea kesi karibu zote. Kipindi hiki ndo kibaya zaidi.

4. Usiseme jambo kubwa au kutenda pasipo ushiriki ama muafaka wa kichama. Mfano leo umeongea vzr kwenye mkutano wa ACT Wazalendo, ila maamuzi juu ya namna na nini cha kushirikiana ni vyema ikawa ni maamuzi ya chama zaidi ya mawazo binafsi.

Nadhani haya yatakufaa kwa nini kuepuka. Wadau wanaweza ongeza zaidi kwenye maoni.

Nakwa upande mwingine, naomba sasa kuwashauri mambo ya kujikita nayo kwa kipindi hiki na hata kwenye kampeni zitakapoanza.

1. Jikite sn kuzungumza maslahi ya wafanyakazi. Tengeneza lugha nzr na mipango madhubuti ya kichama, ser na iwepo pia kwenye ilani, NAMNA GANI MTAWAPUNGUZIA UGUMU WA MAISHA WATUMISHI WA UMMA. Kwa muda mrefu watumishi hawajaongezewa mishahara, madaraja, nyongeza za kila mwaka na kodi pia ijuu. Zungumza zaidi unafuu kwa kundi hili. Ubora wa maisha ya watumishi ni ubora wa kazi na jamii inayowazunguka pia.

2. Kilimo. Zungumzia (andaeni mipango na ilani iseme kuhusu huduma kwa wakulima)

3. Elimu na kero zake, ikiweno kero namaisha magumu sn kwa kundi hili maalum la wafanyakazi. Chamgamoto zote za elimu zinapaswa zichambuliwe vzr. Muda huu ni muda wa kukusanya taarifa sahihi na yote yahusuyo sector hii. Serikali, imejitahidi ila bado yapi mengi ya kufanya. Mikopo kwa kila mwanafunzi hadi waliosoma shule za binafsi maana wote ni watanzania.

4. Afya na changamoto zake
5. Huduma za maji mijini na vijijini
6. Madini na rasilimali zingine za nchi. Hapa kuna mengi sn ya kuyaongea maana ni issue ya kujenga uchumi wa nchi. Hapa unaweza ingia ktk mikataba na wizi wa rasilimali zetu.
7. Utalii
8. Sector zingine zote muhimu
9. Katiba mpya
10. Utawala wa sheria, uhuru wa habari, nk
11. Ujenzi wa miundo mbinu
12. Mahusiano ya kimataifa
N.K

Hitimisho:
Ni mengi nimeongea na kupendekeza nini cha kufanya na cha kuepuka. Mimi sikisurutishi wewe wala chama chako kuyatenda haya, ila ni mapenzi mema tu kwa Tanzania yetu. Haya maoni hata hivyo, yanaweza kumfaa yeyote ktk miongoni mwa vyama vya siasa, ila wananchi watapima uwezo pia kujieleza kwenye hayo maeneo na ushawishi. Kwa hiyi CCM wakiyachukua pia nayo yanaweza wafaa, ila nimeyaelekeza kwako kwa maana watanzania wameanza kukuchukulia kwa utofauti na kwa siku 2 tu nimeona unavyoongea na kutenda unaweza jikuta kwenye marumbano na viongozi wengine na vyombo mbali mblali. Mfano mzuri tayari Msahiri ametoa onyo dhidi yenu.

Naishia hapa, wadau wanaweza kuongeza mengi kuhusu nini cha kufanya /kuongea kwa sasa na nini cha kuepuka ili kuepusha shari zozote. Najua, wanaweza tokea wa kubeza na kutukana, ila ni uhuru tu wa kutoa maoni nimeutumia. I submit

Asante sana.
Mpenda Amani
 
Back
Top Bottom