Namwacha Mchumba wangu kwa sababu ya SIMU!

Namwacha Mchumba wangu kwa sababu ya SIMU!

Nilishakamata mtu mwaka 2006 wakati nipo chuo.

Hahaaaa, unajua nini, hii kitu huwezi ficha aisee, ni sawa sawa na kuweka kaa la moto mfukoni.

We wasema tena...juzi nimejionea hii mwenyewe nilichoka....
njemba moja inakulaga wake za watu, ukimtumia m pesa ni jina la kike ila akituma yeye ni jina la kiume ha ha ha
kila siku wezi wanabuni mbinu mupya!!!
 
We wasema tena...juzi nimejionea hii mwenyewe nilichoka....
njemba moja inakulaga wake za watu, ukimtumia m pesa ni jina la kike ila akituma yeye ni jina la kiume ha ha ha
kila siku wezi wanabuni mbinu mupya!!!

Hii ngumu kuelewa.
 
Nimegundua wanawake sio viumbe wazuri hata kidogo,nina umri wa miaka 36 na mchumba wangu ana umri wa miaka 34,tumekutana miezi minne iliyopita na uhusiano wetu ulikuwa mzuri kwani nilimwamini na kwa kweli ana uwezo kunizidi,mtakumbuka miezi ya hapo nyuma nilileta mada hii hapa,ilikuwa ni true story kabisa
kitu kimoja ambacho huyu dada amekuwa akinisumbua nacho ni simu zake mbili za mkononi,huko nyumba tumewahi kugombana mara kadhaa kwa ajili ya simu,yaani anazificha na hataki kabisa mimi nizishike japokuwa kila simu ina password
jana usiku nililala kwake lakini asubuhi nilipoamka nikagundua simu zake hazipo hapo chumbani kwake,nikamuuliza simu zako ziko wapi?
akachukua begi lake la mkononi na ku search ndani yake hakuna kitu,halafu akawa kama ameshtuka na kusema nilizisahau kwenye gari jana jioni,nikachukua fungua za gari na kwenda kuzichukua lakini sikuona kitu
nilipomuuliza zaidi akawa mkali na kuniwakia eti simwamini kwa sababu ya simu,kilichonishangaza ni kwa nini awe mkali kuulizwa habari ya simu??niliamua kuondoka asubuhi ile ilikuwa saa kumi na moja na kuchapa yeboyebo zangu kurudi kwangu
nimeamua kumwacha kwa sababu japo nilishaanza kumwamini lakini trust yangu imeuwawa na kitendo cha yeye kuficha sana simu
kwani hizo simu zina nini cha siri??nilikuwa nataka tufunge ndoa kabisa mwaka huu lakini kwa mpango huo nitakaa alone milele hapa duniani
bora niishi peke yangu kuliko kuwa na mwanamke mwenye siri
this is true story!!!!
Dooh pole sana, hivi si utakuwa na usingizi sana eeh? ebu nenda kalale manake umeamka saa 11 alfajili hujamalizia usingizi jamani lol!
 
Simu unaleta matatizo sana katika mahusiano,hivi kwanini ulikuja wakati watu wakiwa bado hawajajiandaa kukupokea na matumizi yako?Simu unatutesa sana kila siku kiasi kwamba hatuna amani na imekuwa bila wewe maisha yetu na hata mapenzi yetu yanaonekana si kitu.

Mkuu kwa umri wako inafaa ujue kuwa mwanamke alipoamua kuwa na wewe basi inafaa umwamini yeye kama yeye na ukishughulika sana na nini anafanya au nani anawasiliana nae utajikuta unapata ugonjwa wa moyo.

Huu ni wakati sasa kwako kuwa na maamuzi yaliyo bora kwako kwani umri ndio unakutupa mkono hivyo kama jambo la simu tu unatoka katika mahusiano basi wenzako tunavumilia mengi.

Kaka umesema kweli kabisa
 
Episode unatakiwa kuwa makini labda kazi yake anayofanya inahitaji kuwa na siri, usiangalie upande wa wanaume tu, sawa, kuwa mvumilivu taratibu mtajuana...
 
Hii ngumu kuelewa.

Ukishika namba mpya fasta unaim-pesa kujua ni nani...
sasa namba ya huyo njema ukiitumia m pesa inakuletea jina la kike umetuma pesa kwa eva ila akituma yeye linakuja jina la mwanaume, yote hii kukwepa kushikwa!!!
 
Mmh, huo umri ukishafika na wenyewe una changamoto za hali ya juu sana. Maana unatamani upate mke lakini kila unayempata anakuwa ni magumashi. Hakuna kipindi kigumu kama hicho kwa mwanaume. Wakati walipokuwa wapo tele, hukuwa na mpango wa kuoa, unapofika wakati sasa unataka kuoa, wanaopatikana wote ni manyoka. Mbona utakoma kulinga? Mwisho wa siku utajikuta unaokota chochote kinachoonekana barabarani ili angalau maisha yaendelee. That is how it works.
 
Pole sana lakini unaonekana una tatizo sana na simu kuliko siri zilizoko kwenye simu!
 
La maana hapo ni kuwa umetambua kwa uhakika kuwa mchumba huyo si MWAMINIFU hata nukta, kama ulimwamini kiasi kutotumia kinga,wahi kupima afya ili ujue kama hajaingiza wadudu mwilini mwako,kisha usongeshe mkuu!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
ila sidhani kama ni sahihi,ungetaka ndoa iwepo wala usingehangaika na cm yake,simu ya mpenzio ukishika ni presure unatafuta
 
Mkuu umri wako umeenda sana na karibia unaingia 40, angalia hayo mambo ya simu na the so called life cheating ungetakiwa ufanye ukiwa na umri below 25...hakuna mwanamke asiye na vimbwanga katika mahusiano...maisha ya mahusianao huwa ni yale yale tuu...
 
Back
Top Bottom