Namuunga mkono Rais Magufuli 100% kuendeleza Chato

BLUE BALAA

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
1,222
764
Nimeshawahi kusikia Watanzania wakiwalalamikia Marais waliopita kwamba hawakufanya mambo ya maana makwao kama Baba wa Taifa hakufanya mambo ya maana Musoma vivyo hivyo Mkapa hakufanya mambo ya maana Masasi.

Nami naungana nao kuwalaumu. Kikwete hakufanya mambo ya maana Bagamoyo na Mwinyi hakufanya mambo ya maana Mkuranga.

Hivyo basi naunga mkono yote anayofanya Magufuli kule Chato kwani miundombinu anayoitengeneza Chato ni kwa ajili ya Watanzania wote kama tukiingalia kama fursa.

Huwa najiuliza kama anayofanya Magufuli Chato yangefanywa na viongozi waliotangulia Musoma, Mkuranga, Masasi na Bagamoyo, Je leo Tanzania ingekuwa wapi?

Hivyo watu waache kukaa kwenye vijiwe na kuanza kumsema Rais kwa miundombinu inayofanyika Chato ila waichukulie kama fursa.
 
Kutumia madaraka kwa upendeleo ni ufisadi. Itakuwaje kama kila mwenye madaraka atapendelea kwao zaidi? Wenye kutoa ajira wapendelee kwao, mawaziri wapendelee kwao, madaktari wapendelee kwao, na kadhalika? Usishabikie matumizi mabaya ya madaraka.

Abuse of power is corruption. TAKUKURU waangalie hili la Rais kutumia fedha za nchi kwa upendeleo.
 
Musoma, Mkuranga, Masasi na Msoga kungekuwa na yafuatayo!

1. Uwanja wa mpira wa miguu wa Mkapa ungekuwa kijijini na si DSM. Tuseme tungekuwa na maviwanja hayo vijijini!
2. Hospitali za rufaa zingekuwa huko vijijini
3. Viwanja vinne vya kimataifa tungekuwanavyo huko vijijini kwa hao marais!
4. Mengineyo

Sasa unadhani hayo yangefanyika,ni maeneo gani mengine muhimu yangekosa huduma?

Tumia akili kufikiri!
 
Angejenga hata chuo kikuu pale Mwanza ningemwelewa sn maana hakuna chuo cha serikali pale zaidi ya hivyo vitawi vidogo
 
Musoma,Mkuranga,Masasi na Msoga kungekuwa na yafuatayo!

1.Uwanja wa mpira wa miguu wa Mkapa ungekuwa kijijini na si DSM!Tuseme tungekuwa na maviwanja hayo vijijini!..

Kwahiyo kwako wewe unafarijika sana kuona zilivyo

1. Musoma
2. Masasi
3. Bagamoyo
4. Mkuranga
 
Unajitekenya na kucheka mwenyewe. Pole sana
Kutumia madaraka kwa upendeleo ni ufisadi. Itakuwaje kama kila mwenye madaraka atapendelea kwao zaidi? Wenye kutoa ajira wapendelee kwao , mawaziri wapendelee kwao, madaktari wapendelee kwao, na kadhalika? Usishabikie matumizi mabaya ya madaraka.

Abuse of power is corruption. TAKUKURU waangalie hili la Rais kutumia fedha za nchi kwa upendeleo.
 
Kwahiyo kwako wewe unafarijika sana kuona zilivyo

1. Musoma
2. Masasi
3. Bagamoyo
4. Mkuranga
Kama hayo yanayofanyika Chato yangefanyika huko,leo tusingekuwa na uwanja wa Mkapa pale DSM!

Nikuambie tu, hizo pesa hazitoki mifukoni mwao bali ni kwenye makusanyo ya kodi! Ina maana kama wangeangalia kwao kwanza, sehemu nyingine zingekosa huduma muhimu!

Mfano Mkapa angemwaga Trilion Moja Masasi kwa ajili ya manedeleo, ni barabara ngapi zisingejengwa? Hospitali ngapi zisingejengwa maeneo yenye uhitaji?

Unamjua Mobutu Seseko?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom