Namuunga mkono Kigwangalla dhidi ya MO Dewji

Namuunga mkono Kigwangalla dhidi ya MO Dewji

Huwa simkubali Kigwangwala daima, lakini katika hili yuko sahihi na ninamuunga mkono.

Dewji ameonyesha utoto, ujinga, ujanjaujanja na utapeli mkubwa kuhusu uwekezaji ndani ya Simba.
acha chuki binfsi hizo
 
Nilisikia kiwa transition ya kutoka kwenye club inayimilikiwa na wanachama kwenda kuwa kampuni haijakamilika...

Meaning...Simba bado haijawa kampuni rasmi ili kumruhusu MO kuweka hela za thamani ya hisa alizochukua.

Sasa ikiwa mchakato wa Simba kuwa kampuni haujakamilika...Mo anawekaje mpunga wa 20b now? Akitoa huo mpunga sasa wakati kampuni tarajiwa bado haipo, nani atakuwa amepewa?

Nionavyo mimi...si kuwa Mo ameshindwa kuweka mzigo...ila ni miundombinu na mfumo wa kuifanya Simba kuwa kampuni bado haujakamilika. Na hii unamfanya investor yeyote ahofie security ya uwekezaji wake.

Kampuni ikiwa tayari...na waka call shares watakaoshindwa kuzilipia ndio walaumiwe...but not now. Maana Mo hatakuwa mwanahisa pekee kwenye club. Bado majority wenye 51% ambao mainly watakuwa wanachama....hao nao watatakiwa kulipia hisa zao.
 
Kigwa ana point sema mashabiki wa mbumbu Mo aondoke Simba ..... Simba itaendeshwa na wanachama kama alivyoikuta na haitakufa....
Aden Rage aliwahi kusema washabiki wa simba ni mbumbu
sisi mashabiki wa simba sio mbumbumbu wewe ndio mbumbumbu mashabiki wa simba tunajitambua na ndio maana tumemuamini mo na timu inashinda
 
Sitaki kuamini kama kuna watu watamtilia maanani kigwa, ana pointi sawa na sidhani kama hajui sehemu ya kwenda kuhoji ili apate majibu ya uhakika, kwanini ayatafutie majibu tweeter? Nahisi dhumuni la kigwa siyo kuhoji kuna cha ziada. Ila tangu nione ubabaishaji anaoufanya kwenye miradi yake binafsi nimekuwa na ukakasi wa kuamini vingi asemavyo na kuhoji.
 
Ule mkopo wa pikipiki ndio tatizo.

Kigwa ni mtu mzima sasa ameaminika kwa kupewa cheo cha juu, aache njaa hizi za aibu.

Ajiamini asihonge wajumbe. Kazi zake na kuwajibika kwake jimboni kumbebe asijidhalilishe kwa matajiri.

Bora angemkopa DAB.
Alitaka kukopa pkpk alipe na kiinua mgongo cha bunge
 
Nilisikia kiwa transition ya kutoka kwenye club inayimilikiwa na wanachama kwenda kuwa kampuni haijakamilika...

Meaning...Simba bado haijawa kampuni rasmi ili kumruhusu MO kuweka hela za thamani ya hisa alizochukua.

Sasa ikiwa mchakato wa Simba kuwa kampuni haujakamilika...Mo anawekaje mpunga wa 20b now? Akitoa huo mpunga sasa wakati kampuni tarajiwa bado haipo, nani atakuwa amepewa?

Nionavyo mimi...si kuwa Mo ameshindwa kuweka mzigo...ila ni miundombinu na mfumo wa kuifanya Simba kuwa kampuni bado haujakamilika. Na hii unamfanya investor yeyote ahofie security ya uwekezaji wake.

Kampuni ikiwa tayari...na waka call shares watakaoshindwa kuzilipia ndio walaumiwe...but not now. Maana Mo hatakuwa mwanahisa pekee kwenye club. Bado majority wenye 51% ambao mainly watakuwa wanachama....hao nao watatakiwa kulipia hisa zao.
Nyamazeni tu asije kususa. Ila msilazimishe sababu zisizo make sense.
 
Ule mkopo wa pikipiki ndio tatizo.

Kigwa ni mtu mzima sasa ameaminika kwa kupewa cheo cha juu, aache njaa hizi za aibu.

Ajiamini asihonge wajumbe. Kazi zake na kuwajibika kwake jimboni kumbebe asijidhalilishe kwa matajiri.

Bora angemkopa DAB.
Je alichokisema Kingwangala kina ukweli hakina ukweli? Kaweka na makubariano ya kuwa 10% ilibidi ilipwe na siku hiyo na 90% ndani ya mwezi toka apokee barua ya kupewa hisa. Leo mwaka wa tatu hakuna kitu.
Sasa Mo ni mfadhiri au mwanahisa?
Watanzania sisi ni watu wa ajabu sana, kuna wanaofurahia anayofanya Mo bila kufuata makubariano kisa wanaona kwa sasa mambo yanaenda sawa, lakini hao hao utawasikia wakilalamika kuwa Magufuri hafuati katiba, anachukua tu pesa anajena barabara bila kufuata mwongozo.
 
Ile issue ya.mo na Kigwangala haijaanza leo ilianza toka kipindi kile mo anatishia kujitoa simba aliposema anatumia pesa nyingi kuhudumia simba akamwuliza hizo pesa ni sehemu ya bilioni 20 au zake za mfukoni .
Kigwangala amehoji mambo ya msingi ila kwa ujinga walionao watu wengi wamemjadili zaidi yeye binafsi ikiwa pamoja na mo kukwepa mjadala na kuingiza personal issue.
Mo anapaswa kutoa majibu kwa wanasimba na sio kwenda kutoa majibu kwa wasafi fm ambao tunajua watangazaji wake wengi ni yanga wa kutupwa.
Kuna madudu mengi kuhusiana na uwekezaji wanmo ila madudu hayo hayaonekani kwa sababu ya mafanikio tunayoyapata uwanjani.
Ajatoa bilioni 20 kwa sababu mchakato haujakamilika lakini ameshakuwa na madaraka makubwa kabla mchakato haujakamilika.
Kuna bidhaa zake ambazo hazipo kwenye mkataba na simba lakini amekuwa akizitangaza kupitia simba mfano mo protector sasa ukiacha zile pikipiki zake sasa kama anamleta CEO ambaye ni msaidizi wake binafsi ataweza vp kutenganisha maslahi ya simba na ya kampuni anazoongoza mo.
Kuna kanga zilikuwa zinauzwa simba day hazijulikani nani ametengeneza na pesa zinaenda kwa nani ukichukulia na yeye anamiliki viwanda vya nguo.
Mpaka sasa simba haijaweza kujitegemea leo mo akitoka simba itasimama vipi pamoja na mishahara mikubwa ya wachezaji.
Uko sawa kabisa Kigwangala kahoji mambo ya msingi na kuya backup na ushahidi. Il kwakuwa watanzania uwa hawashawishiwi na facts bali mapenzi hawataki kuona points zake . Mpaka sasa Mo hajulikani kama ni mfadhiri au mwekezaji maana hata hisa hajazilipia lakini anafanya maamuzi makubwa ndani ya sima kama major shareholder.
 
Tapeli kishafanya yake ya kujipatia 50% of shares bila hata ya kulipa senti moja huo ni WIZI!!! Nasikia katishia kujitoa Simba lakini ni KITISHO UCHWARA tu tapeli huyo kishaonja asali ya utamu wa Simba sasa kachonga mzinga. Mara tu tutasikia ana miliki 100% ya shares za Simba.

Dewji linapokuja swala la 20b anakuwa mkalis sana hapa ndio panapo leta mashaka

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
 
Lazima tujiulize... unauliza 20b km kiongozi, kama shabiki ama nani.

Ikiwa ni kama kiingozi.. tunataka wewe unaeuliza, jukumu na mchango wako ni upi mpaka sasa kufanya uhoji 20b?

Ikiwa kama shabiki... unataka nini unapoulizia 20b... je yaliyofanyika hadi sasa hayadiserve heko kwa huyo uneyemuuliza 20b kaweka wapi?
Je hufurahii matokeo ya simba ya sasa
Je wachezaji wanalalamika au hawana morali..

Mashabiki wa simba ama wengineo mnaoleta chokochoko acheni hizo... mo anaweka pesa lengo afaidike pia... na katika uwekaji hizo pesa lazima kuwe nautaratibu.. kumbuka wako katika kipindi cha mabadiliko.. simba pesa zilikua zinaliwa hovyo hovyo na walaf wachache bila kuonesha faida... kwa hiyo wakati huu lazima kuwe na utaratibu wa usimamizi, kujenga uaminifu ili maendeleo yaongeze kazi katika club.

Acheni wafanye kazi.... sisi mashabiki tufurahie matokeo tu... hata kama akiweka iyo 20b kwe akaunt... kama shabiki huwezi pata hata mia.... shabiki jukumu lako ni kushangilia tu... na wao kazi yao ni kutupa furaha tu... mo kazi yake ni kuhakikisha club inatoa burudani kwa namna yeyote.
Si mlitaka simba igeuzwe kuwa club ya kisasa ya wanahisa, na mkabadirisa katiba, mkaweka utaratibu na Mo akasema ananunua hisa 50% kwa 20B. Sasa ni mwaka wa tatu hizo hisa hajalipia lakini anafanya maamuzi kama majorshareholder.
Je Mo ni mfadhiri au mwanahisa? Maana akiulizwa tu anatishia kujitoa kamavile mfadhiri. Wabongo tuache kufanya business as usual kisa tu mambo yanaenda sawa, afuate makubariano waliyoingia na ndicho Kingwangala anachouliza.
Sema badala ya kutazama point zake za msingi mnamshambulia tu.
 
Mh. Kigwangala kwenye siasa huwa simuelewi kabisa ila kwenye suala la Simba ana point kubwa sana, CEO wa simba si suala la gender wala experience kwenye soka maana sio CEO wa kwanza kwenye soka. Je, kwanini awe na vinasaba na moja kati ya mtu anayetaka kuinunua club ya wanachama?

Simba siyo NGO binafsi ya Mo ni taasisi ya kubwa ya mamilioni ya watu ambayo inahama kwenda kwenye corporate entinty nafasi kama ya CEO ambaye ni mtendaji mkuu wa club lazima itangazwe kwa absolute transparent maana interest ya mamilioni ya watu relay to her hatutaki mtu biased hasa tunaopoelekea kwenye mchakato wa mabadiliko.

Our future must be secured, siyo kwa sababu tunapata matokeo basi mambo yafanyike kienyeji tu bila weledi mkubwa, suala la kukopa kwa kila mpambanaji ni kawaida tu as longer analipa kwa wakati!

NB: Yajayo yanafurahisha, tuendele kupata matokeo lasivyo aaaah, Mo kwenye 20b anakuwaga Mwamedi.
Hakuna cha hoja za msingi hapo suala ni unafiki na chuki za kijinga tu. Anahoji za Mo vipi zile 51% amezihoji?

Hawa wanataka kuturudisha kulekule kwenye makundi ya friends of Simba ili waendelee na upigaji wao na udalali.
 
Anayehoji swala la Simba kwanza tunataka awe na hela mtu hata Mia huna afu unamuhoji mtu anayetumia pesa nyingi kulipa mishahara na kusajili.hatutaki kelele weka kwanza ww izo 20b afu ndio uanze kuongea
 
Je angehoji kama angekopeshwa?
Kaweka screenshot kuwa kaanza kuhoji hili toka January hata kabla hajaomba mkopo, so si kwamba kahoji kisa hakupewa mkopo. Na angekuwa ana kinyongo baada ya kumnyima mkopo asingekwenda kununua tena hizo pikipiki kwa Mo kwa kutumia cash baadae.
Hapa point ya msingi je anayohoji yana ukweli?
 
Anayehoji swala la Simba kwanza tunataka awe na hela mtu hata Mia huna afu unamuhoji mtu anayetumia pesa nyingi kulipa mishahara na kusajili.hatutaki kelele weka kwanza ww izo 20b afu ndio uanze kuongea
Simba ikijuwepo Tangu zaman kama alikuwa anataka kwanini hakuichukua yeye?!!
 
Hakuna cha hoja za msingi hapo suala ni unafiki na chuki za kijinga tu. Anahoji za Mo vipi zile 51% amezihoji?

Hawa wanataka kuturudisha kulekule kwenye makundi ya friends of Simba ili waendelee na upigaji wao na udalali.
51% zipo tangu 1936, kazikuta. Sasa yeye aweke zake.
 
MO akitaka kubaki salama, aunde club yake na aendelee kuwa shabiki wa Simba.
Timu ya Simba ina mashabiki wengi wenye madaraka Serikalini.
Haingii akilini MO akiingia uwanjani akashangiliwa kuliko Rais ambaye naye ni shabiki wa Simba.
Mtawala huwa hapendi mwanainchi wa kawaida kuwa maarufu kuliko yeye.
MO akianza kupingana na Kigwangala mwisho wa Siku ataanza kupingana na Majaliwa na kumalizia na MH. Magufuli.
Rais Mstaafu Kikwete alisema, hatutaki club inayomilikiwa na mtu moja.
Michezo ni burudani na tunataka kushangilia kilicho chetu na si cha mtu.
Msahafu unasema .
"Ole wake mtu yule amuaminiane mwanadamu kama kinga yake, mbinguni amelaaniwa"
Club ya Simba sasa inamuamini MO kama kinga yao, mbinguni wamelaaniwa.
Je kesho Mo kama hayupo Duniani club ya Simba itakuwa na hali gani?
Let us think beyond one year.
Wajifunze kwa yanga, walikuwa wanapata matokeo na manji, alipoondoka tuu, timu ilibaki kama yatima, halafu hawa matajiri wawekezaji wa hizi timu wajanja sana, hawaweki misingi ya kuzifanya team zijitegee, toka simba imeenda kweny madiliko,hakuna chochote kikubwa kilichofanyika kuifanya timu kuwa na mapato yake mbali tu na wale wadhamin, hata mfumo wa bidhaa za timu kama jezi upo hoi bado,wachache wanapiga peaa.

Mashabiki na wanachama wa simba wanafurahia tu matokeo uwanjan,bila kujua timu imesimama kutoka mfukon mwa mtu mmoja,akikohoa tuu hawana lolote.
 
Tapeli kishafanya yake ya kujipatia 50% of shares bila hata ya kulipa senti moja huo ni WIZI!!! Nasikia katishia kujitoa Simba lakini ni KITISHO UCHWARA tu tapeli huyo kishaonja asali ya utamu wa Simba sasa kachonga mzinga. Mara tu tutasikia ana miliki 100% ya shares za Simba.
Akijitoa simba ashitakiwe maana ameitumia simba bila kulipia senti na anaifanya simba imtegemee badala ya kujitegemea
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kaweka screenshot kuwa kaanza kuhoji hili toka January hata kabla hajaomba mkopo, so si kwamba kahoji kisa hakupewa mkopo. Na angekuwa ana kinyongo baada ya kumnyima mkopo asingekwenda kununua tena hizo pikipiki kwa Mo kwa kutumia cash baadae.
Hapa point ya msingi je anayohoji yana ukweli?
Alihoji toka Mo alipotishia kujitoa baada ya simba kufanya vibaya kwenye kombe la mapinduzi
 
Dewji linapokuja swala la 20b anakuwa mkalis sana hapa ndio panapo leta mashaka

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app

Ukiona nyuki wamekuwa wakali ujue kuna asali.
Mo akisikia mtu anazungumzia 20bil. Mkali baraa, nakumbuka aliwahi kuhojiwa na wasafi tv kuhusu hizo 20bl. Aliishia kujibu mimi niwakukoswa 20 bl.? Hakika halikuwa jibu! Dr kigwa anahaki yakuhoji maana anajua kila kitu,

Mi najua mo atakuwa kamuweka huyo dada ili aanze kuongeza zero zero kwenye matumizi mpaka 20bl ziishe, itakuwa senzo alimkatalia labda.
Anatakiwa aweke hizo 20bl. Ilisimba ijiendeshe badala yakumtegemea yy.
 
Back
Top Bottom