Namuomba msamaha Haji Manara kwa kumpinga aliposema waandishi wengi wa Tanzania ni "takataka" leo EFM radio wamethibitisha

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,211
42,074
Wasalaam,

Haji Manara aliwakera wengi sana alipo diriki kuwaita waandishi wa habari hasa za michezo kuwa ni "takataka" kwakweli ni maneno yaliyo fikirisha sana wengi na wengi walioneshwa kukerwa sana na kitendo kile cha udhalilishaji kilicho fanywa na haji manara na wengi walitegemea hatua zaidi zinge chukuliwa kabisa.

Lakini mchezo wa ligi kuu utakao wakutanisha Simba na Yanga ambao utafanyika jumamosi hii, jana Haji Manara msemaji wa Simba Club alikuwa anaongea na waandishi wa habari lakini katika kikao chake tukio lililo gonga vichwa na kusambaa sana kwenye Mitandao ya kijamii ni tukio la kuwashambulia baadhi ya waandishi wa habari akiwemo Mtangazaji wa Clouds Fm Prisca Kishamba aliyemuuliza swali ambalo lilimkera haji na swali lilikuwa liko wazi na liliekezwa kwenye rekodi ya simba anapo kutana hata na Yanga mbovu.

Swali husika lilimkera Haji Manara na kuanza kumshambulia mtangazaji Prisca Kishamba na kutaka asihudhuria press conference yeyote ya simba hata kama yeye hayupo.

Tukio lile lilikuwa la udhalilishaji kwa muandishi husika na watu wa kwanza kulikemea walitakiwa kuwa wa kwanza kulikemea bila kupepesa macho lakini walitakiwa pia kutoa nafasi ya kumsikiliza haji.

Nilipata wasaha wa kuwasikiliza watangazaji wa Clouds FM kwenye kipindi cha michezo jioni walisema wazi na walikemea wazi kabisa japo Haji Manara mwenyewe hakuwepo na nilitamani kama angelikuwepo kuona kama wangesema walio sema lakini niwapongeze kwa uthubutu.

Lakini leo Haji Manara alikwenda kwenye kipindi cha Sport Heaquater cha EFm Radio.

Baada ya kusikia Haji ana maongezi pale EFM radio matarajio ya wengi na watanzania wengi hasa kwenye tasnia ya michezo walitarajia kuwa watangazaji wa EFM wakiongozwa na Tunu Hassan, Jemedari Saidi, Jeff lea, na watangazi wenzao wamuulize maswali ya nguvu manara kuhusu tukio lile na ikiwezekna wamwambie kama anaona umuhimu wa kuomba radhi kwa mtangazji husika na kwa uwazi walipaswa kuhakikisha Manara anaeleza wazi ili tukio lile lisijirudie na nina hakika Manara angehojiwa vizuri wala asingesita kuomba radhi.

Lakini ukweli ni kwamba EFM RADIO kupitia watangazaji wake wenyewe wakiongozwa na Tunu Hassan wamethibitisha wazi ule usemi wa Haji Mnara kuwa baadhi ya waandishi na wachabuzi hasa wa michezo ni "takataka" ni kweli leo watangazaji wa EFM Wamethibisha kuwa wao kweli ni "takataka" kama alivyo tuambia Haji Manara.

Yani watangazaji wameshindwa kumwambia wazi tena machoni Haji Manara kuwa anapaswa kuomba radhi na alikosea kabisa na alikosea na atakiwi kurudia yale makosa yale kabisa na kibaya zaidi kwenye kipindi cha leo alikuwepo mtangazaji mwanamke mwenzie Prisca ambaye ni Tunu Hassan lakini na yeye alishindwa hata kuuliza hilo swali hata kumuomba aombe radhi kwa udhalilishaji aliofanyiwa mwenzie.

Leo nimethibitisha watangazaji na waandishi ni watu wa hovyo hovyo sana hapa Tanzania.

Kwa muktadha huu naomba nichukue nafasi hii kumuomba msamaha Haji Manara kwani nilimpinga aliposema waandishi na watangaziji/wachambuzi wa michezo tz ni taka taka, hakika nimethibitisha leo.

Kumradhi Haji Manara
 
Waandishi wa Tanzania hawajali maslahi mapana ya nchi yao japo kuwa mama mjengo kawapa uhuru wkutosha.

Swali nalijiuliza manara anapat wapi nguvu alaizo nazo kuta mka hayo maneno, na nani aliyeko nyuma ya manara mpk waandishi wanamuogopa wana muona kama mungu mtu kwenye maswala ya michezo.

Sithani kama maneno yale angeyatamka msemaji wa yanga ungesikia saivi kashafungiwa.

Kikubwa wanishi wa habari za michezo hawana ummoja kabsa kila station za radio na tv zina vuti kwakee coz ya njaa kali na kutafuta upo polarity wa kijinga wakati hamna kitu, tukio kama lile waandishi wa habari za michezo wangetakiwa wasiriport kuhusu press ya manaraa kwa umoja wao na kukemeaa waone wanakuja kulalamika na kutafuta huruma za wanachi.
 
Huyo Manara mwenyewe takataka kama hao waandishi wa habari anaowatukana. Mtu mwenye akili zake timamu kwa nafasi aliyonayo Manara anapaswa kutambua kuwa tegemezi lake kuu la kufanikisha kazi yake ni waandishi wa habari.
Tatizo linakuja kuwa hao waandishi wa habari wenyewe hawajui umuhimu wao kiasi kwamba wapuuzi kama kina Manara wanajiaminisha kuwa wanaweza sema chochote na maisha yakaendelea. Hii ni kwa Tanzania tu by the way.
 
Wasafi media(team diamond),mawingu media(team kiba),efm(team konde) je unafikiri kutakuwa na umoja kweli? by then kwa soka letu la sasa sioni umuhimu wa timu kuwa na msemaji wa timu.
 
sawa prisca tumekuelewa
 
Waandishi wa Tanzania hawajali maslahi mapana ya nchi yao japo kuwa mama mjengo kawapa uhuru wkutosha.

Swali nalijiuliza manara anapat wapi nguvu alaizo nazo kuta mka hayo maneno, na nani aliyeko nyuma ya manara mpk waandishi wanamuogopa wana muona kama mungu mtu kwenye maswala ya michezo.

Sithani kama maneno yale angeyatamka msemaji wa yanga ungesikia saivi kashafungiwa.

Kikubwa wanishi wa habari za michezo hawana ummoja kabsa kila station za radio na tv zina vuti kwakee coz ya njaa kali na kutafuta upo polarity wa kijinga wakati hamna kitu, tukio kama lile waandishi wa habari za michezo wangetakiwa wasiriport kuhusu press ya manaraa kwa umoja wao na kukemeaa waone wanakuja kulalamika na kutafuta huruma za wanachi.
Hivi mtu kama manara anawapa nini hadi wanamuogopa namna hiyo?
 
Wanaogopa jamaa kuwaumbua kwa kuweka mambo yao binafsi hadharani. Ogopa mtu mwenye taarifa zako nyeti ambazo usingependa zijulikane.
hahahaha nimekumbuka siku Maulid Kitenge alivyo ufyata hahaha
 
kwanza bila shaka hichi cheo cha kijinga kipo tz tuuu
Wasafi media(team diamond),mawingu media(team kiba),efm(team konde) je unafikiri kutakuwa na umoja kweli? by then kwa soka letu la sasa sioni umuhimu wa timu kuwa na msemaji wa timu.
 
Huyo Manara mwenyewe takataka kama hao waandishi wa habari anaowatukana. Mtu mwenye akili zake timamu kwa nafasi aliyonayo Manara anapaswa kutambua kuwa tegemezi lake kuu la kufanikisha kazi yake ni waandishi wa habari.
Tatizo linakuja kuwa hao waandishi wa habari wenyewe hawajui umuhimu kiasi kwamba wapuuzi kama kina Manara wanajiamisha kuwa wanaweza sema chochote na maisha yakaendelea. Hii ni kwa Tanzania tu by the way.
kusema kweli Manara ni mmoja ya watu wenye mtindio wa ubongo ukimtazama vyema lakini hawa wakina Tunu na wenzie ndio wameonesha wazi kuwa wao ni takataka
 
manara anajikuta mungu mtu dawa yake muro ndo uwa anamchana bila uwago
 
Back
Top Bottom