hiyo tabia ya mama yako imekuwa kawaida tu siku hizi kwa wazazi wengi. nakushauri msamehe kwani naye ni binadamu kama wengine. endelea kumheshimu hivyohivyo na ikibidi uongeze heshima lakini pia uwe na bidii kutafuta kujitegemea kwanza na kisha kama ni mapenzi ya Mungu uwe na mali ya ziada na hata uwezo wa kuwasaidia wengine akiwemo mama yako huyo.
kumbuka kuwa kama hujajitegemea, hilo ndo kikwazo cha kwanza cha wewe kuheshimiwa na watu. jitahidi ujitegemee kwanza. kama tayari unajitegemea, ni vyema lakini usiwe unaomba kusaidiwa na ndugu zako au kupeleka mashitaka nyumbani kwenu kuwa ndugu zako hawakusaidii. jitahidi kupigana peke yako na ikiwezekana shirikiana kwa karibu na marafiki wema ili kuangalia namna ya kunyanyuka kimaisha kwani siku utakaponyanyuka, utaheshimiwa na wote.
mwisho usipuuze haja ya kujiendeleza kwa kutafuta elimu kubwa zaidi. wengi walishindwa kupata maisha mazuri kwa kuyatafuta mitaani, wakayapata kirahisi kupitia darasani. Mungu hawezi kukunyima vyote, Yeye ni mwaminifu kwao wamchao na hakika siku moja atasikia sala yako atakuinua kwa wakati wake
Jina la Bwana lihimidiwe
mkuu mimi ni mwanaume na ni wa kwanza kuzaliwa,wadogo zangu wana uwezo lakini mimi sina uwezo sana ila mungu amenisaidia kuridhika na hali niliyo nayo
judith umenipa ushauri mzuri sana
lakini mimi ni mtu mzima tayari na natamani nigeweza kumsamehe na kusahau lakini kila nikifika nyumbani nakumbuka na kulia machozi,namkumbuka baba yangu ambaye ni marehemu alivyokuwa mtu mwema na mpole
mkuu inawezekana wewe na mama yako mna
tofauti kubwa ya personality....wanaita personality clash....
Sasa wewe mwanaume unalia machozi kwa kukumbuka ya zamani????
Mimi naona hapo unakuwa weak na pengine mama
yupo more strong na anataka wewe uwe strong na ku fight...
Mama yako ana drive na ambitions ambazo wewe huna naona..
So mnazidi kutengana...
judith umenipa ushauri mzuri sana
lakini mimi ni mtu mzima tayari na natamani nigeweza kumsamehe na kusahau lakini kila nikifika nyumbani nakumbuka na kulia machozi,namkumbuka baba yangu ambaye ni marehemu alivyokuwa mtu mwema na mpole
siamini kama wewe ni masikini kiasi hicho,kwani masikini hana ata access ya jamiiforum!shukuru mungu kisha pambana ktk maisha!unataka mama akuthamini huku huna uwezo wa kumtimizia shida zake?akija dar anafikia kwa mtoto aliyempokea na gari ubungo,ataenda kwa mtoto ambaye chakula anachotaka anapikiwa,alale chumba chenye kiyoyozi,akatibiwe trauma centre au agha khan si wewe una mpeleka mwananyamala hosp etc

Na isimlaumu sana mama yako.....

Huwezi jua maisha yame mfunza kitu gani...

Inawezekana life haikuwa kind kwake.....

Unajua the boss,inawezekana kabisa ikawa anajisikia vibaya mwenyewe tu, na ile hali ya ma infiriority, kwa kuwa tu wadogo zake wamemtangulia kimaisha, na amini nakwambia ukiweza kujipa moyo na kuridhik na ulichonacho utaona mama yako ni kawaida tu, na vile wakati mwingine anakuonea huruma kukuombaomba misaada pia unajisikia vibaya

Life was so cruel......so na yeye anatoa kile ambacho life imempa....

Hakuheshimika labda na society kwa umasikini...

So na yeye kwa kuuchukia umasikini,anawachukia mpaka watoto masikini..
Halafu kuna vitu vingine vinaanzia mbali sana
je baba yako alikuwa tajiri?
Kama alikuwa masikini,mama yako alimchukuliaje??
Kama alikuwa anakasirishwa na baba yako kushindwa
kutumia nafasi alizopata kuondokana na umasikini
si ajabu na wewe umerithi tabia za baba yako
so chuki ya mama yako kwa baba yako imehamia kwako.......