Namuacha shemeji yenu!

Namuacha shemeji yenu!

Kumuacha unaweza kumuacha ndio,ila una uhakika wa kupata mwanaume mwenye pesa kuliko huyo uliyenaye Sasa?Jiulize Hili swali kabla hujafanya maamuzi.

Mimi sioni umuhimu wa wewe kumuacha.Cha kufanya mhimize akatafute kazi ya kufanya asiendelee kukaa kwa shemeji. Kumuacha sio suluhisho la kudumu.
 
Kuwa na hela inategemea zaidi "status " ya uliyenaye.

Kwa mfano huyo mwanaume aliyetajwa angetafuta wa size yake tusingesikia haya.
KILA MBUZI ALE KWA UREFU WA KAMBA YAKE
Wa size yake yupi? Mwanaume kutokua na hela ni aibu. Wanaume wengine wanafanya kazi za ajabu ili mradi awe na kitu mfukoni. Mwanaume kusema huna hela kila wakati haipendezi
 
Yaani mimi kuwa na mwanaume ambaye hana pesa naona mzigo kwangu na kwa familia yangu. Mwanaume wangu hana kazi yupo idle tu, mimi nina kibarua changu. Jana nimempigia simu (maana siku hizi anani-text tu mimi ndio huwa nampigia) nikimuuliza kwanini unanitext tu, anasema hana hela ya vocha text kaunga za mwezi, hata pesa ya kula hana na yupo kwa shemeji yake anaumwa yeye ndio anamhudumia, dada yake amesafiri.

Nikamuuliza, unaishije hapo kwa shemeji yako ata mia huna na wewe ni mtu mzima inabidi siku moja moja unachangia? Ananiambia sasa nitachangia nini wakati hela sina na kazi sijapata?

Aisee tangu nianze mahusiano yangu huyu mwanaume ndio hana pesa, wanaume wangu wawili wa nyuma walikuwa na mkwanja ukikohoa kidogo tu M-Pesa yako inasoma muda huo huo, ila huyu nawaza kumuacha kila siku, sioni anachonisaidia.

Amewahi kuninunulia kuku nusu tu wakati mapenzi yanaanza, tangu hapo hamna alichonipa tena zaidi ya neno lake sina pesa. Shida niliconcetrate sana kwenye muonekano wake, shemeji yenu ni li handsome sana, shida halina pesa! Hicho tu yaani dah!
Tatizo lako umegeuza mapenzi kama kitega uchumi, halafu ni kosa kubwa sana unafanya la kumlinganisha mwanaume wako wa sasa na wazamani.Huo ni umalaya.Namsikitikia mwanaume mwenzangu kwa kuoa malaya.
 
Minafikiri hapo tatizo ni unamwanaume ambae hana akili.
Pesa ni kitu kingine, ina kuepo na inakwisha pia.
Nafikiri mwanaume wako ni aina ya wale wavulana wavivu na hapendi kujishughulisha.
Kumuacha ama kuto kumuacha sina la kukushauri, lakini kwa dalili hizo inakupa picha kubwa ya aina ya msalaba utakao ubeba huko siku za mbele.
 
Shida ya wanawake wa kibongo mnawaza pesa tu mupewe nyie.

Kuna muda mume unamtengeneza wewe. Kama unampenda na una nafasi ya kipesa kama ulivyosema. Usimpe hela ya kula, Focus kumtengeneza mume wa maisha yenu ya baadae. Mtengenezee biashara ya kueleweka,mdanganye hii biashara nimekopa hela bank tutairudisha kwa muda fulani. Hapo ni kumpima kama anaweza kuiendeleza hiyo biashara.
Au kama yeye ana uwezo wa kufanya biashara fulani,mpe mtaji mwambie nimekopa tutairudisha. Then aangalia hiyo biashara inaendaje. Kama inatembea,ongeza nguvu hapo.

Maisha yanaanza kwa mtindo huo. WASICHANA JITAHIDINI HATA NYIE KUWAANDAA WAUME ZENU WA BAADAE,MSIKAZANIE NA KUWAZA KUISHIA KWENYE MAPENZI TU. MAISHA YA KESHO NI VILE UNAVYOYAANDAA WEWE LEO.
 
Muache harakaaa, ukibeba mimba yake tu umekwishaaaaa
Nyieee majobless hawaachikagi kirahisi mjue....hapo mwanaume anaoga kutwa mara tatu, msafi anang'aa...na hivo anakaa Kwa dada anadowea pafyumu ya Shemeji ananukia....yaani anafaa Kwa maonesho ya kuringishia mashost🤣🤣🤣
Halafu ukimtaka anytime huyu hapa, na mkoba anakubebea....ndo ukute tall and black 🤣🤣🤣🤣 weuweeee

Hapo tumshauri amvumilie apate hela Ili aachwe yeye....huyu ubavu Hana, Kwanza anayeacha hasemi.
 
Wa size yake yupi? Mwanaume kutokua na hela ni aibu. Wanaume wengine wanafanya kazi za ajabu ili mradi awe na kitu mfukoni. Mwanaume kusema huna hela kila wakati haipendezi
Hapo nakubaliana na wewe lazima mwanaume afanye kazi yoyote inayomuingizia kipato (halali), ila tukubaliane kuwa kuna levels kumhudumia Mobetto Siyo sawa na kumhudumia Ebitoke
 
Yaani mimi kuwa na mwanaume ambaye hana pesa naona mzigo kwangu na kwa familia yangu. Mwanaume wangu hana kazi yupo idle tu, mimi nina kibarua changu. Jana nimempigia simu (maana siku hizi anani-text tu mimi ndio huwa nampigia) nikimuuliza kwanini unanitext tu, anasema hana hela ya vocha text kaunga za mwezi, hata pesa ya kula hana na yupo kwa shemeji yake anaumwa yeye ndio anamhudumia, dada yake amesafiri.

Nikamuuliza, unaishije hapo kwa shemeji yako ata mia huna na wewe ni mtu mzima inabidi siku moja moja unachangia? Ananiambia sasa nitachangia nini wakati hela sina na kazi sijapata?

Aisee tangu nianze mahusiano yangu huyu mwanaume ndio hana pesa, wanaume wangu wawili wa nyuma walikuwa na mkwanja ukikohoa kidogo tu M-Pesa yako inasoma muda huo huo, ila huyu nawaza kumuacha kila siku, sioni anachonisaidia.

Amewahi kuninunulia kuku nusu tu wakati mapenzi yanaanza, tangu hapo hamna alichonipa tena zaidi ya neno lake sina pesa. Shida niliconcetrate sana kwenye muonekano wake, shemeji yenu ni li handsome sana, shida halina pesa! Hicho tu yaani dah!
Mvumilie bhn atawini soon tu
 
Back
Top Bottom