Namtafuta baba yangu mzazi mzee Jovin Machumu

Wakuu habari zenu,

Namtafuta mzee wangu. Mama na mzee waligombana kipindi mimi nazaliwa kwa hiyo mzee aliondoka na mama akakata kabisa mawasiliano naye.

Ni miaka zaidi ya 25 imepita, mimi simfahamu mzee hata kwa picha, baada ya mahojiano na mama akanipa maelezo yafuatayo
- Jina lake ni Jovin Machumu
-Mara ya mwisho mama alisikia anaishi Shinyanga na alikuwa anafanya kazi Tanzania National Miling
-kabila lake ni Muhaya
- Hawafahamu kabisa ndugu wa mzee

Kwa yeyote ambaye anamjua mtu ambaye alifanya kazi national milling Shinyanga naomba aniunganishe. Sina maelezo mengine zaidi ya hayo kwa hiyo naomba msaada wenu wakuu. Mwenye nia ya kunisaidia anitumie meseji pm.
Pole sana, mimi nilikuwa namtafuta Mzee wangu humu humu, bahati mbaya au nzuri nimeweza kuwapata ndugu zangu, japo mzee alishakufa muda. Utampata tu.
 
Kwa hiyo ya kufanya kazi national milling ilikuwa lini kwa mara mwisho? Maana NMC zilikufa siku nyingi sana. Yale ma-godown pale SHY huwa yanakodishwa kwa watu kwa ajili ya kutunzia mizigo, sasa sidhani kama utapata mtu wa kukuelekeza pale!
Kama mleta mada anasema Baba na mama yake waliachana wakati yeye anazaliwa na imeshapita miaka 25 toka waachane kuna mwanga kua Baba yake alikua akifanya kazi hapo NMC mwaka 1991, japo sio rahisi kujua kua alikua hapo NMC mpaka mwaka gani kwa mara ya mwisho.
 
Ni kweli mkuu ..shukran kwa kufafanua
 
Wakuu habari zenu,

Namtafuta mzee wangu. Mama na mzee waligombana kipindi mimi nazaliwa kwa hiyo mzee aliondoka na mama akakata kabisa mawasiliano naye.

Ni miaka zaidi ya 25 imepita, mimi simfahamu mzee hata kwa picha, baada ya mahojiano na mama akanipa maelezo yafuatayo
- Jina lake ni Jovin Machumu
-Mara ya mwisho mama alisikia anaishi Shinyanga na alikuwa anafanya kazi Tanzania National Miling
-kabila lake ni Muhaya
- Hawafahamu kabisa ndugu wa mzee

Kwa yeyote ambaye anamjua mtu ambaye alifanya kazi national milling Shinyanga naomba aniunganishe. Sina maelezo mengine zaidi ya hayo kwa hiyo naomba msaada wenu wakuu. Mwenye nia ya kunisaidia anitumie meseji pm.
KUNA MTU ANAMTAFUTA JOVIN SILAYIO CHEKINAE MNA UNDUGUU???
 
Mimi ni jirani sana na wakima machumu hapa bukoba,tafadhali njoo nikuunganishe nao pengine babako yupp hapa
 
Back
Top Bottom