Kisa cha Kweli: Mimi na Baba tutamsamehe vipi Mama? Nami nitawezaje msamehe Mzazi wangu?

Sodoku

JF-Expert Member
Feb 3, 2016
1,095
2,429
Mimi ni kijana wa miaka 39 nina mke na mtoto mmoja. Ni mwanaume pekee katika familia ya Mzee yenye watoto 4. Mimi ni mtoto wa mwisho kwetu. Dada zangu wawili wameolewa na mmoja anaishi mwenyewe akiwa na mtoto mmoja. kisa ninachosimulia ni cha kweli ambacho hakina wiki mbili mpaka tarehe hii toka kitokee. Leo nimeamua kukisimulia ili angalau nivue vazi hili zito nililovaa.

Mzee na Mama wapo nje kidogo ya Mji sehemu ambayo waliamua kupumzika baada ya kustaafu.

Jumatatu iliyopita mzee alipigiwa simu kwa namba mpya. Anasema alijivuta sana kupokea sababu ulikuwa ni muda ambao yeye hupenda kupumzika kujisomea vitabu.

Mzee wangu ana miaka 79 sasa. Muda mwingi hupenda kuhudumia ng'ombe kuangalia na kutengeneza mazingira kisha hupumzika akisoma vitabu.

Aliamua kupokea simu kwa unyonge na kusikia sauti toka pande ya pili.
Simu : " Hallow. Habari za jioni??
Mzee: "Salama"
Simu: Naongea na Mzee xxxxxx?
Mzee: Ndiyo nani mwenzangu?
Simu: Mimi ni Mzee xxxxx nilitafuta sana namba yako hatimaye nimeipata. Naomba sana tuonane kesho nipo Hospital ya xxxx Chumba namba xxxx.

Mzee anasema hakuwa tayari kwenda kesho yake hiyo hosp sababu alikuwa na ratiba nyingine. Lakini hakutaka kubishana na mhusika. Alihisi huyo atakuwa tapeli kama walivyo matapeli wengi hapa mjini. Hivyo akamua tu kupuuza.

Kesho yake hakwenda na hakupiga simu. Jioni akapigiwa tena simu, mara nyingi sana kwa ile namba. Mwishowe ikaja meseji.

"Tafadhali mzee mwenzangu. Nahitaji sana kuonana nawe maisha yangu yamefika ukingoni nahitaji kuonana nawe mzee mwenzangu nikuage kwa amani.hata dakika 10 tu nakuomba sana unipunguzie mateso."

Mzee anasema aliamua kupiga simu kwa ile namba. Ikapokea tena sauti hafifu ikimsihi sana kesho asikose kufika. Ikiomba kwa kusihi sana kuwa anaomba aruhusiwe kwenda kupumzika.

Mzee hakuweza elewa nini hasa alichokuwa akiombewa kwenda kukifanya. Usiku ule anasema aliota ndoto mbaya. Amepanda mahindi yameota vyema na kunawiri lakini karibia na kuvuna yakashika moto. Akagundua mmoja ya watu waliokuwa wakimsaidia kupalilia aliunguza mahindi yale kwa moto wa sigara.

Mzee ni msiri sana. Huwa hapendi kuzungumzia mambo yake. Mara nyingi hunyamaa tu anapokuwa na mawazo. Kesho yake asubuhi akaamua kwenda Hosp tajwa. Anasema hakuwa akijisikia vizuri so akaamua kutumia usafiri wa Umma.

Ana gari yake ya muda mrefu sana Toyota Hilux double cabin. Ni gari ambayo huwa haendeshi mtu yeyote isipokuwa yeye. Alituambia siku moja. Ikitokea amefariki ile gari nichukue mimi. Ila nisije iuza. Nikae nayo miaka yote but angalau kama nipo karibu nayo nisiache iendesha hata mara moja kwa mwezi. Isipokuwa kama imekufa.

Siku hiyo hakuenda nayo. Akatumia usafiri wa umma. Mpaka hospital iliyotakiwa aende. Alipofika hospital walimkatalia kuingia sababu muda ulikuwa umeisha. Wakamtaka asubiri mpaka mchana.

Akiwa anajaribu kujieleza kwa Mlinzi ambaye alikuwa anaonekana naye ameshachoka kuombwa ombwa na watu kuingia wakati usio sahihi alikuja daktari mmoja akamsalimia kwa bashasha sana.

Daktari akamshika mkono na kumwamkia huku akimtizama sana usoni kwa mshangao. Akamwambia mlinzi anaondoka na huyu mzee anamhitaji. Mzee anasema alishangaa tu lakini akahisi pengine ni moja ya vijana aliowahi wafundisha chuo. Mzee alikuwa ni lecturer mstaafu chuo flani nchini.

Yule daktari akamchukua mpaka ofisini kwake. Akamkaribisha kwenye kiti. Akachukua simu akawa anatafuta kitu. Kisha akasema unaitwa Mzee xxxx?
Mzee : Ndiyo.
Daktari: Haya ni maajabu. Nashindwa kuelewa.
Mzee: Sielewi kijana kuna nini na umejuaje jina langu?
Daktari: Nimekuota usiku wa kuamkia jana, mazingira ni yale yale kama leo nilivyokukuta na ulivaa hivi hivi. Ulijitambulisha jina kwa mlinzi ukitaka hilo jina likatajwe kwa mgonjwa wodi na xxxx mwenye jina xxxx.

Mzee: Sielewi hata moja unayoyasema hebu nifafanulie, maana mimi sijataja jina kwa mlinzi lakini uliloniambia ndiyo jina langu.

Yule daktari anasema aliota kuwa siku hiyo ameenda kazini akachelewa kutokana na foleni iliyosababishwa na mvua kitu ambacho kweli kilitokea. Na alipofika mlangoni kuingia wodini alikutana na mzee ambaye amevaa kama alivyovaa mzee. Kitu ambacho amekikuta kweli.

Mzee hakuwa akielewa nini kinaendelea. Akasema kuna mgonjwa alitamani kumuona ila sasa amechelewa. Yule daktari alimwambia wataingia wote akamwone. Kavaa koti jeupe la kidaktari juu ya shati lake na kuchukua vifaa kadhaa akamwambia mzee amfuate.

Mzee anasema walipita pita korido kadhaa na hatimaye wakaingia wodi iliyokuwa na vitanda viwili. Kimoja hakina mtu na kimoja kina mtu. Akamwambia akamsalimie mgonjwa wake pale.

Mzee alisogea huku moyo ukimdunda, hakuwa akijua anaenda kuonana na nani. Aliona kiumbe kimelala kikiwa kimempa mgongo na kujiviringa shuka la hosp. Kikawaida muda ule ilikuwa ngumu kwa mtu mzima kujifunika kutokana na joto la hapa jijini.

Mzee anasema alisogea huku moyo ukionekana kupoteza mapigo yake ya kawaida. Akasimama kwanza akavuta pumzi, akageuka, hakumwona Daktari na mlango ulikuwa umerudishwa. Akajongea tena kitandani na kuita kwa sauti Mzee xxxx kama ambavyo alitajiwa jina. Akaita mara ya pili, ya tatu......


Nitaendelea (naandika nikiwa nimejawa na hasira, majonzi na huzuni ni kipindi kigumu sana kwangu) ....
 
Kawaida ya binadamu hupenda kulipa kisasi ndio moyo wake utulie na awe na amani ,kisasa unaweza kutokutekeleza wewe ila ukisikia yule mlengwa wako amepatwa na jambo baya huwa ni furaha sana.

So mleta mada kama ni mama yako mzazi jitahidi sana kusamehe, hiko kisasi muachie baba yako tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom