Niwasimulie kisa cha Babu yangu aliyekuwa kama baba yangu

Beesmom

JF-Expert Member
May 30, 2016
17,221
28,664
Mi ni first born, tumezaliwa wawili. Miaka hiyo ya 90s baada ya mama kutalikiana na baba mzazi aliyeamua kumuoa mwanamke mwingine na kumwingiza aishi nyumba moja na mama(dharau) hivyo mama alishindwa aliamua kurudi home kwao Tukuyu from Magomeni Mapipa DSM. Watoto wawili, hivyo akaona hatoweza kuanza maisha akiwa na watoto wote wawili, so Mimi nikaachwa kwa bibi na babu(ambaye ndo baba kwangu) nikiwa na three yrs old na kuja nichukua nikiwa na 11 yrs old maisha yake yaliposeto(yeye mama aniambiavyo maana nilikuwa ninamuuliza kwanini sasa na siyo vile nikiwa mdogo sana)

Story kuhusu babu sasa(baba yangu). Yeye ni mtoto wa Malafyale(chifu) wa Kinyakyusa, hivyo wanaume wa kichifu enzi hizo walikuwa wana tabia ya kuoa wake zaidi ya mmoja, so baba yake babu(nyanya yangu) kwa mke mkubwa alikuwa na watoto 10(wanawake enzi hizo walikuwa wanafyatua simbilisi akasome). Katika tembea tembea yake akampa mwanamke Mwingine ujauzito huko hivyo kibusara ikabidi amshirikishe bi mkubwa kwamba anataka aongeze mke, bi mkubwa akakataa katukatu hivyo babu alivyozaliwa akawa mtoto wa hawara.

Miaka ikaenda watoto wote 11 yaani pamoja na babu wakawa watu wazima, babu(nyanya) aliwatafutia vitu vya kufanya ili waendelee kuishi na wake zao ila mtoto wa hawara(babu) bi mkubwa alikaza no kumwangaikia mbona ana mama yake na yupo peke yake hivyo haitakuwa ngumu kumsaidia mwanae, na ni kweli mama wa babu yangu akahangaikiwa na ***** hivyo badala ya kurithishwa shamba akarithishwa elimu ambapo akafanikiwa kuwa mgambo anaetambulika. Eeeeh bwana we kutambulika kwa kikosi chao kukawaponza, si akachaguliwa kushiriki vita ya Kagera(1978) kama chambo vile(wale wanajeshi safisha njia wanaotangulizwa mbele) kiufupi walijua ndo imekula kwake lakini babu alirudi(sijui alijificha),ila alirudi na donda kisogoni but baadae alitibiwa alipona.

Kurudi kwa babu sasa ikawa kama amerudi kuja kumuaga baba yake mzazi, hatimaye Malafyale(nyanya yangu) ukongwe ulikuwa umemwandama, akawa anaumwa bila kupona, siku ya kukata moto aliwaita watoto wake wote lakini cha ajabu waliitana wao tu 10 babu wakamwambia hapaswi hata kugusa mazingira Yale, wamekusanyana wasikie mzee anasemaje the last word. Bwana bwana si dingi akogoma siwezi fumba macho kwa amani bila kumwona the last born (babu yangu sasa) akawahimiza mwiteni mwanangu, sijamlea, sijamtunza wala kumpa baraka zozote maishani mwake lakini bado Mungu anampigania. Ikabidi wamwite kivivu hivyo hivyo akaingia chaupole wa watu. Kitendo cha kuingia tu baba yake akamwambia naomba unisamehe mwanangu sina cha kukupa ila naomba wewe ndo urithi home hapa, wewe ndiye utaongoza kaka zako na wanakijiji(balozi). Nduguze na yeye pia wakahamaki....wanataka waanze kuwaka pale mzee akakata moto ikawa imeisha hiyo.

So after that babu akaanza kuishi pale(hadi sasa ndo tunapofikia kama kuna jambo sanasana misiba). Maisha yakaendelee akapata mke akapata watoto 9(wote wako hai)mama yangu ni uzao wa nne kwake lakini vita na ndugu zake haikukoma kutaka kumwondoa eneo lile kwamba hastahili. Kumfukuza hawawezi hivyo ikawa vita ya chinichini mpaka babu alipokufa wakati nduguze 8 wameshazikwa then tukazika babu siku yake(ni msiba ambao nalia mpaka Leo, alitukusanya wajukuu 15 na alitulea bila ubaguzi). Mungu amlaze mahali pema peponi chaupole baba yangu kipenzi, aliyenifundisha kulima, kufuga, kukamua ng'ombe maziwa, na vitu vingi vinavyonisaidia Leo hii

Daa, ndo hivyo katika watoto 11 kabaki bibi mmoja tu ambae ni mzee sana, sana yaani.

Ndo hivyo, karibuni Tukuyu wapendwa
 
Back
Top Bottom