Namsikitikia, He was my boyfriend

Namsikitikia, He was my boyfriend

Nazjaz

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
7,775
Reaction score
9,203
Leo nimemkuta Posta Mpya, ni mchafu anadandia mabasi. Anawahi siti kupitia madirishani ili wenye kuhitaji siti wampatie ujira wa sh. 500.

Tulikutana naye mwaka 2004 tukiwa form 5.

Tulipendana naye napenzi ya dhati, kama gari na matairi ndivyo tulivyokuwa.

Form six tulipoingia, kuna dada mrembo sana, kwa kuwa boyfriend wangu huyu alikuwa na uwezo sana darasani wasichana wengi wakawa wakimfuata ili awafundishe huku moyoni wakiwa na yao. Miongoni mwa waliokuwa wakimfuata boyfrend wangu ni pamoja na mgeni huyu aliyehamia. Sijui alitumia mbinu gani, akamnyakuwa wangu wa moyo. Nilipigwa kibuti assemble, my boyfriend was head prefect. Akautangazia umma wa wanafunzi kuwa ameniacha. Niliumia sana, nikamwachia Mungu.

Tukiwa kwenye likizo ya kusubiri majibu, nikasikia eti my ex boyfriend kapelekwa jela kwa wizi. Sista duu alikuwa anahitaji mambo makubwa, ambayo ili my ex ayamudu ilimbidi aibe na kukwapua. Bahati mbaya za mwizi arobaini, akakamatwa na kufungwa kifungo cha miaka mitatu. Majibu yakatoka, alikuwa amefaulu vizuri sana, one ya point nne PCB.

Sikuwahi kumuona tena ndio namuona leo akiwa ni teja, hana mbele wala nyuma.
 
inasikitisha sana...haya ndio maisha na hayana formula.
 
Duh kwa kweli pole sana
Ila kuna kitu kimeniingia juu ya hii story........... hivi wattoto wetu wanapokuwa shule wanaelewa wako pale kwa sababu gani? Najaribu kuwaza mtu aliyekuwa na akili kiasi cha kupata Div 1.4 form six anashindwaje kutambua kuwa kuiba kunawezamharibia future yake (kama alikuwa anaitambua??)

Pole sana........kama bado una mapenzi ya kweli juu yake angalia namna ya kumsaidia......atakuwa amejifunza !
 
Dada Nazjaz kumbuka, teja habebeki, mpige chini mazima, usije haribu uhusiano wako wa maana na mla unga, utalia tena mara ya pili kwani utakuwa umepoteza mwana na maji ya moto.
 
Akome!Hakukustahili kamwe!

Dada Nazjaz kumbuka, teja habebeki, mpige chini mazima, usije haribu uhusiano wako wa maana na mla unga, utalia tena mara ya pili kwani utakuwa umepoteza mwana na maji ya moto.

Si vema kuendelea kumpiga mtu ambaye ameshaanguka, pia tenda wema uende zako.....,
Kumsaidia haimaanishi arudiane nae, bali anaweza kumsaidia kwa mawazo au kumwelekeza kwenye mstari ulionyooka, maybe hawezi kupata kazi sababu ya historia yake ya kuwa jela lakini huenda anaweza akaanzisha miradi ambayo itamsaidia
 
maana kila ushauri una positives na negatives zake. Lakini naamini mwishoni ntapata neno jema, maana penye wengi hapaharibiki kitu
 
Nazjaz, msaidie rafik yko hta kdogo, unajua kna njia nyingi za msaada, naamin unampenda ila wakat umempita, mpe kamsaada hata kadogo hata kwa kupitia mgongo wa mtu, na si kumpita km humjui. N ushaur wangu, ila msaada huo usipitilaze ukakuharibia.
 
Leo nimemkuta Posta Mpya, ni mchafu anadandia mabasi. Anawahi siti kupitia madirishani ili wenye kuhitaji siti wampatie ujira wa sh. 500.
Tulikutana naye mwaka 2004 tukiwa form 5.
Tulipendana naye napenzi ya dhati, kama gari na matairi ndivyo tulivyokuwa.
Form six tulipo ingia, kuna dada mrembo sana, kwa kuwa boyfriend wangu huyu alikuwa na uwezo sana darasani wasichana wengi wakawa wakimfuata ili awafundishe huku moyoni wakiwa na yao.
Miongoni mwa waliokuwa wakimfuata boyfrend wangu ni pamoja na mgeni huyu aliyehamia.
Sijui alitumia mbinu gani, akamnyakuwa wangu wa moyo. Nilipigwa kibuti assemble, my boyfriend was head prefect. Akaungazia umma wa wanafunzi kuwa ameniacha. Niliumia sana, nikamwachia Mungu.
Tukiwa kwenye likizo ya kusubiri majibu, nikasikia eti my ex boyfriend kapelekwa jela kwa wizi. Sista duu alikuwa anahitaji mambo makubwa, ambayo ili my ex ayamudu ilimbidi aibe na kukwapua.
Bahati mbaya za mwizi arobaini, akakamatwa na kufungwa kifungo cha miaka mitatu. Majibu yakatoka, alikuwa amefaulu vizuri sana, one ya point nne PCB.
Sikuwahi kumuona tena ndio namuona leo akiwa ni teja, hana mbele wala nyuma.

i dont know why, ila wewe huaminiki na mimi sikuamini..... utunzi mwema
 
Kama una uwezo msaidie,mpeleke hata kwenye huduma za kidini kama maombezi,just do a favor na sio kumrudia kimapenzi,ikitokea akarudia hali yake ya kawaida anaweza akakufaa huko mbeleni kwa ajili ya msaada uliompatia,ila sisemi atakufaa kimapenzi.
 
attention seeking disorder (ASD)

there is no treatment for such diseases at the moment, researches suggest that frequent sex may be useful, alcohol exacerbate the problem especially when the subject is horny and didnt get boned!!
 
A Friend in Need is a Friend Indeed....
Sasa kama huwezi kumsaidia kwenye matatizo wewe utakuwa na faida gani kwake, kumbuka mlipendana before....
 
hahaha! sasa na ww ni zamu yako kutoa huo msada. can u? afu frequency hujaisema ni 2 bd ama?kwenu watoa ushauri: mnataka asaidiwe kwa vile alikuwa bf wa form ? angekuwa ni ex-hubby ama ex-bf wakati anafanya kazi mngemshauri the same?kwako nazjaz, i wld say dont get involved. bf/mume ulienae leo,ukimuona anamsaidia ex wake wa utotoni utajiskiaje? usifanyie wengine usiyopenda kufanyiwa. pili, kumsaidia teja ni kazi sana na inahitaji commitment ya hali ya juu. jasiri haachi asili. ila ukiyavulia nguo mtoto wa kike shurti uyaoge,all the best.
attention seeking disorder (ASD) there is no treatment for such diseases at the moment, researches suggest that frequent sex may be useful, alcohol exacerbate the problem especially when the subject is horny and didnt get boned!!
 
Jamani naomba tupunguze jazba!
Teja hajaomba msaada kwa mtu yeyote. Na wewe Nazjaz usidhani asingekuacha kipindi kile basi maisha yake yangekuwa tofauti (maana wabongo ndiyo zenu hizo). Ni teja kwa kuwa si kinyume chake. Pengine angeendelea na wewe angeuawa wakati akifanya ujambazi wa kutumia silaha. Yote ya Mungu hayo. Mateja wataendelea kuwapo pasipo kujali walikuwa na tabia gani kabla hawajaanza kubwia. Mnafikiri wale Wa-Afghan wa unga wataishije huyu jamaa akiacha kutumia unga? Hata hivyo pole kama ni kweli unajisikia machungu kumwona hivyo!
 
Back
Top Bottom