Zero IQ
JF-Expert Member
- Dec 21, 2016
- 13,941
- 24,816
Mwanzo mkuu The bond nilikuwa Nakuelewa sana, ulivyokuwa unachambua mada zako hapa jukwaani kwa weredi mkubwa hakika ulionekana utaifanya JF ionekane ni ya magreat thinkers wa ukweli.
Ile siku yako ya kwanza kutoa Andiko lako hapa kwa mbwembwe na huku ukisindikizwa na makamera mengi, kilichonifanya nikuone wewe ni mtu wa tofauti kuliko yule aliyepita, ukatoka kwenu kwa miguu mpaka Office ya JF na kukagua kama kuna Chochote kilibaki kwenye hazina.
Haikuishia hapo ukatutangazia wana JF wote tukutane tufanye usafi na wewe mwenyewe The bond ukawa mstari wa mbele siku ile, na hapo ndipo nyota yako iliendelea kung'aa.
Ukajipa Muda wa kuchagua wasaidizi wako kwa kuchambua Ugreat thinker wao ili wafanane na wewe mwenyewe katika utendaji wao. Hakika ulichagua Vyema lakini mwisho wa Yote ukamchagua mmoja asiyefaa Anaitwa Mshana Jr na ukamfanya awe ni mmoja ya watu unayempenda sana;
Mshana Jr mwanzo alikuwa anaonekana ni mtenda kazi mzuri sana tena sana Ndani ya Jf kwa kuandika Mada zake zenye Ugreat thinker ndani yake, Lakini Tamaa ikamponza Mshana Jr, akaanza kutaja Majina ya watu wazito kwenye Maandiko yake na kuwatuhumu ili mradi mwisho wa siku anaomba Chochote kitu.
Member wengi walitoa maoni yao kwamba umtoe katika nafasi yake huyu Mshana Jr kwa sababu anakuaribia wewe The Bond na atakufanya uonekana mbaya mbele ya members wengine. Lakini ukatoka na kauli yako moja Matata nanukuu "Mimi sipangiwi Cha kupost" mwache achape kazi.
Ukweli ukamuacha afanye kazi na member ukawaacha na Swali sijui huyo Mshana Jr anakupa nini licha ya Madudu Mengi aliyofanya ukizingatia wewe ni muumini mzuri wa kutumbua watendaji wako wabovu kama ulivyo Fanya kwa miss Chaga alivyotangazia humu JF Ule ugonjwa hatari waZika. (Habari njema ni kwamba ulimtumbua miss Chaga kwa kutetea taaluma yake na sasa kaula kwa Maboss).
Mungu si athumani Akakupa Mtihani wewe The bond kwa kuwapa baadhi ya Member humu Jf Matatizo ili kupima wema katika Roho yako .
Ukatangaza utaratibu wa kuwasaidia, kweli member na baadhi ya forum walitoa Mchango wao,
Mfano jirani zetu Kenya forum walikuwa nasi bega kwa bega kwenye yale matatizo.
Lakini mwisho wa siku ukafanya kitu ambacho hakikutegemewa na wengi sanasana na wale walioona Ule uchungu ulio nao kwa member wa humu Jf.
Ukachukua michango yote na kusema utaitumia kurekebisha Jamii forum yetu na Member wote wa Jf waliopata matatizo wajisaidie wenyewe.
Cha kushangaza zaidi na kunifanya niseme hayo The bond ni juzi hapo Humu Jf yalivyotokea Yale Matatizo ya watoto na kuyafanya ya kitaifa kuna tetesi kwamba zilitumika hela za michango ya waliopata matatizo kwenye shughuli nzima na baadhi ya Michango umeweka kibindoni.
Ni tetesi lakini sijui kama kweli.
Mwisho the bond Na Mshana Jr msitufanyie hivi sisi member wenu wa humu Jf forum kwani na sisi tuna Damu na mioyo inatuuma japo tunashindwa kusema..!