Nampinga Robert Heriel kuhusu dhana ya umasikini

Nampinga Robert Heriel kuhusu dhana ya umasikini

Mkuu Kwanza Nashukuru Kwa kunipinga na kutoa Mtazamo wako dhidi ya mtazamo wangu.

Turudi kwenye Mjadala.

Topic ya Poverty ipo Kidato cha tatu Kwa waliofika elimu ya Upili.
Maana ya umasikini inafahamika Kwa waliofika madarasa hayo.
Individual level umasikini ni kitendo au Hali ya mtu kukosa mahitaji yake ya msingi Kama chakula, mavazi, makazi. Ingawaje yapo nahitaji mengine ya ziada yaliyoongezeka ambayo nayo yanachukuliwa Kama sehemu ya basic needs mfano Sex, mawasiliano ya simu n.k.
Tubakie katika maana hiyo ya msingi..

Ukishakuwa masikini upo katika kundi la wenye Laana ukubali au ukatae.
KIVIPI?

LAANA ni neno ambalo moja Kwa moja linahusu suala la kiimani, miungu, supernatural power,.
Mtu yeyote ukimsikia anasema kuhusu Laana basi ujue anaamini katika miungu.
Hakuna miungu hakuna laana.

Kisayansi hakuna laana. Ila kiimani Laana Ipo.
Kinyume cha Laana ni Baraka.
Unaposema baraka pia unazungumzia mambo ya kiimani, miungu na mambo dhahania.
Kisayansi hakuna kitu inaitwa Baraka

LAANA NI NINI?
Laana ni tamko, Kauli anayotamkiwa mtu au kikundi cha watu iliyodhamiria kudhuru au kuleta madhara, maangamizo, baada ya mtu au watu hao kuvunja kanuni au amri Fulani.
Laana inahusu zaidi miungu na mara nyingi hutolewa Kwa nguvu za miungu, au Kwa jina la miungu.

Kwa mujibu wa maandiko, laana za awali zilizotamkwa binadamu ni Kama ifuatavyo;
1. Kifo au mauti
2. Njaa( ardhi imelaaniwa hivyo mwanaume atakula Kwa jasho)
3. Mwanamke kuzaa Kwa uchungu Ile ni laana.

Kwa kifupi Laana no adhabu huku Baraka ni Zawadi.

Sasa kivipi umasikini uwe ni laana? Na iweje Masikini wawe wamelaaniwa?

Ili mtu aitwe masikini kuna viashiria, vifuatavyo ni baadhi ya viashiria kuwa mtu au jamii Fulani ni masikini

1. High mortality Rate/kiwango kikubwa cha wanaokufa.
Vifo vya watoto wachanga kuwa vingi na watu kufa mapema kabla ya uzee kutokana na sababu nyingi tuu ikiwemo Huduma duni za Afya, njaa, elimu ndogo n.k.

Kumbuka kifo ni laana na umasikini unapelekea vifo kuwa vingi. Biblia inaeleza wazi kuhusu Hilo.

2. Makazi duni na maisha duni/ poor living conditions.
Mtu anaishi makazi mabovu, mazingira hatarishi ni moja ya viashiria kuwa mtu au jamii Fulani ni masikini.
Ni laana kuishi makazi Duni. Tafsiri ya moja Kwa moja ni adhabu kuishi makazi duni, machafu, mbavu za mbwa.

3. Kiwango kikubwa cha wajinga/ High Illiteracy rate.
Kukosa elimu pia ni Dalili ya Masikini, yaani kukosa elimu ni sehemu ya laana.
Biblia inasema, watu wangu wanaangamia Kwa Kukosa Maarifa.
Laana kumbuka ndio kuangamia kwenyewe.
Ukiwa huna elimu utashindwa kuishi maisha mazuri, utakuwa mjingamjinga.
Sasa hapo kwenye elimu ndio kuna Formal, non-formal and Informal education.

Yaani kuwa mjinga tuu ni laana tosha, maana ukiwa na akili huwezi kuwa Masikini.

4. Njaa/Hunger
Kula Mlo mmoja, utapiamlo, kukosa kabisa Kula chakula ni Dalili za umasikini.
Kumbuka Njaa ni laana kama unabisha nitakuleta vifungu vyakutosha tuu! Kumbuka Ardhi ililaaniwa ili watu wafe njaa😂😂.

5. Maradhi
Maradhi husababisha umasikini, na umasikini husababisha Maradhi. Yaani Maradhi na umasikini ni marafiki Pacha ukimjumlisha na ndugu Yao ujinga.
Kumbuka Maradhi pia ni laana, na Biblia inaeleza

Pia kumbuka Yesu alitoa Laana yake pia kuwa asiyefanya kazi Kula na asile yaani afe kwanjaa.
Na njaa ni moja ya indicator muhimu ya umasikini.

Soma kumbukumbu la Torati 28
Utaona ni Kwa namna gani Umasikini ni laana.

Masikini wasaidie lakini wenye uhitaji/watakaokuomba msaada Ila kujipendekeza Kwa masikini wasiohitaji msaada wako nakuhakikishia matokeo yake utayapata na yatakuwa mabaya zaidi

Umasikini ni laana.
Masikini wamelaaniwa.

Kumbuka zipo laana za watu wote na zipo laana za kundi Fulani. Kifo ni laana ya kila kiumbe kilichozaliwa na Mwanamke, umasikini ni laana ya kundi Fulani la watu.

Kama ilivyo zipo baraka za watu wote na zipo baraka za watu wakundi Fulani. Nuru ya jua au mvua au hewa ni baraka Kwa watu wote, lakini madini, uzuri, Utajiri, nguvu ni baraka Kwa kundi Fulani la watu.

Huo ndio ukweli.

Umasikini ndio ushetani wenyewe, ndio laana, ni mauti.
Unakosea sana na hamna kitu unajua umeenda Chaka kabisa, kusema umaskini ni laana ...Kuna vitu hujui maana hata wewe wazazi wako wameshindwa kuamua wewe ungezaliwa mke au mume.Bahati nzuri umekuwa mwanaume .

Unapoongea Kuna vitu fikiria sana kwanza then ndo uandike.
 
Kama bado hujajua umasikini ni laana basi unasafari ndefu katika Kujifunza.

Maisha ya mwanadamu yanaongozwa na Mungu. Na Mungu katika kuongoza viumbe wake amewawekea Njia kadhaa za kuchagua au ambazo watazipitia.

Kama ukijua Kama kuna umasikini popote pale jua IPO laana hapohapo.

Umasikini ni kifungo ni adhabu. Sasa Kama mpaka Jambo Hilo hujui mpaka uambiwe utakuwa unashida
 
Ukishakuwa masikini tayari unalaana huwezi ishi vizuri ukiwa masikini wewe. Acha kudanganya au kujidanganya hapa.

Mkeo habari vizuri,
Kila siku mlo mmoja,
Makazi mabovu,
Watoto wanasoma Kwa tabu, bado useme unaishi vizuri Kwa Amani?

Ukishakuwa masikini tayari unalaana unachopaswa kukifanya ni kukabiliana na laana hiyo.

Matajiri wenye laana wapo lakini sio katika kipengele cha Pesa au Mali.

Laana ni adhabu,
Ndio maana nikataja indicators umasikini hapo na kuzifungamanisha na zinavyoingiliana na laana.

Sijawahi ona Masikini anayeishi Vizuri.
Umasikini wako sio laana

Na km unachukulia umasikini ulionao ni laana basi itakua umejilaani wewe mwenyewe

Na kwa sababu wewe ni masikini unajiona na kujihisi umelaaniwa kumbe umejilaani mwenyewe basi sio kila unaemuona ni masikini ukadhani amejilaani km wewe

Kwa hio km wewe unaona umasikini ni laana basi hio laana umejipa wewe km wewe usiseme kila ambae ni masikini basi amelaaniwa na nani? Una uthibitisho gan?

Wewe kwa sababu unajijua ni kwa sababu gani umeishia kua masikini basi unajua laana yako ulipoitoa ndio maana umeishia kua ulivyo masikini means umejilaani wewe mwenyewe

Hivyo basi usihisi wala usiseme kwamba kila unaemuona ni masikini basi ana laana km uliyonayo wewe sababu wewe laana hio ya umasikini umejipa mwenyewe
 
Kama bado hujajua umasikini ni laana basi unasafari ndefu katika Kujifunza.

Maisha ya mwanadamu yanaongozwa na Mungu. Na Mungu katika kuongoza viumbe wake amewawekea Njia kadhaa za kuchagua au ambazo watazipitia.

Kama ukijua Kama kuna umasikini popote pale jua IPO laana hapohapo.

Umasikini ni kifungo ni adhabu. Sasa Kama mpaka Jambo Hilo hujui mpaka uambiwe utakuwa unashida
Hamna kitu kama icho sio kweli ... Umepotea kabisa katika uchumi wa dunia Tena unaotegemea speculation ya fedha ni lazima pawe na maskini hyo sio laana unaweza kuwa tajiri ukawa na laana hata ya wazazi..

Siamini ivyo izo ni kauli za motivational speakers hazipo katika real life
 
Habari ndugu zangu, imenilazimu kuandika kupinga dhana iliyotolewa na member mwenzetu tajwa hapo juu

Hili Ni bandiko linalolenga kukosoa mtazamo wake juu ya dhana fikirishi ya umaskini ambayo aliieleza Kama "Laana" Jambo ambalo si sahihi

✓Kwanza ameshindwa kuonesha ya kwamba binadamu awe na Nini au akoswe Nini ndo awe maskini hii Ni kwasababu dhana ya umaskini Haina maana moja, Maskini wa Dar yaweza kuwa Tajiri Tarime

✓Biblia na vitabu vingine vya kiroho vinatambua dhana ya umaskini na vimeshauri tuwasaidie kwa kuweka hazina zetu juu Yao kwa kuwapa mavazi na chakula kwakuwa tupo nao siku zote
✓Umaskini siyo Laana Kama anavyohisi mwenzetu,Binadamu anaweza zaliwa maskini,yeye kuwa tajili Ni juhudi zake binafsi

Naomba kuwasilisha ndugu zangu
UMASIKINI ni LAANA
 
Scientifically Kila mtu anapata riziki kulingana na thinking capacity yake Mwenye uwezo mdogo wa kufikiri ataangukia vibarua vya kwenye mkonge wakati mwingine aliekaa darasani due to his high intelligence anaangukia BOT.
God, science and religion depend on one another to finalize findings.
Hamna kitu kama icho sio wote Kuna watu Wana akili ila wapi na kufikiria sana watu washaandaa ma projects kibao ila wameangukia pua
 
Umaskini sio laana kama unabisha soma vitabu vyenye historia ya uchumi wa fedha utakuja nielewa...Dunia ya sasa tunatumia pesa ndo kila kitu lazima wengine wanyonye ili kuweza kuwa juu wale mabillionea wakubwa kabisa ndo wanamiliki share za wadogo.

Mataifa makubwa yenye maskini wachache ndo yananyonya huku Africa kweny maskini wengi... Ukienda India Kuna maskini kwa sababu wapo wengi na matajiri wengi Wana mafedha wamerundika tu Kuna watu hawana hata msosi hali mbaya..
 
Umasikini wako sio laana

Na km unachukulia umasikini ulionao ni laana basi itakua umejilaani wewe mwenyewe

Na kwa sababu wewe ni masikini unajiona na kujihisi umelaaniwa kumbe umejilaani mwenyewe basi sio kila unaemuona ni masikini ukadhani amejilaani km wewe

Kwa hio km wewe unaona umasikini ni laana basi hio laana umejipa wewe km wewe usiseme kila ambae ni masikini basi amelaaniwa na nani? Una uthibitisho gan?

Wewe kwa sababu unajijua ni kwa sababu gani umeishia kua masikini basi unajua laana yako ulipoitoa ndio maana umeishia kua ulivyo masikini means umejilaani wewe mwenyewe

Hivyo basi usihisi wala usiseme kwamba kila unaemuona ni masikini basi ana laana km uliyonayo wewe sababu wewe laana hio ya umasikini umejipa mwenyewe

Endelea kujifariji hapo.
Ila jua Kama wewe ni masikini jua Unalaana na upo kwenye Laana.

Nilishatoa maelezo kutetea hoja hii kiimani,

Wewe Jipe Moyo 😂😂
Sio kosa kujifariji na kufarijiwa.

Ila Wenye Akili na wanaoelewa Dunia ilipotoka, ilipo na inapoenda Wanajua Umasikini ni Laana.
 
Mfumo unataka wengine wawe masikini wengine wawe matajiri. Ndio mana hata watu wote tukisoma wapo watakaofanya kazi zinazolet umasikini. Huu mfumo ni piramidi. Lazima Kuna jitu liwe juu zaidi ya wenzie. Suala la umasikin Lita kuwepo mpaka mfumo huu ubadilike. La sivyo tupunguze tu gep Kati ya maskini na tajiri lisiwe kubwa. Manake haiwezekani ELON MUSK awe na hela nyingi kuliko WatAnzania wote duniani
Umasikini ni kushindwa kupata nahitaji yote muhimu ya kila siku na swala hilo , ndiyo la kulitafutia ufumbuzi.(Chakula,Makazi,Makazi) huduma za kiafya Pamoja na elimu.

Swala la kuwa kama elon musk ni swala lingine
 
"Masikini wasaidie lakini wenye uhitaji/watakaokuomba msaada Ila kujipendekeza Kwa masikini wasiohitaji msaada wako nakuhakikishia matokeo yake utayapata na yatakuwa mabaya zaidi"

Ahsant kwa kulegeza msimamamo ndugu yangu ROBERT HERIEL Naamini Sasa Kwa ufaraguzi wa Members wenzangu wa Jf Kuna haya nimejifunza
✓Kumbe hata utajiri waweza kuwa laana iliyoboreshwa,rejea wanaopata utajiri kwa matendo ya hovyo Kama vile mauaji,rushwa,kafara nk kwa nje unaweza kudhani Wana amani lakini kinyume chake Ni sahihi
✓Laana Ni dhana binafsi,ukiamini kuwa umelaaniwa hakika itakuwa hivyo,ukiamini pia umebarikiwa pia maisha yako yatakuwa hivyo,
✓Maskini wengi wanaamini kuwa wamelaaniwa na wameumbwa wawe hivyo(Babu,baba woote Maskini)Hivyo huacha kujishughulisha kwa bidii yenye ubunifu ili waweze kujikwamua katika Hali waliyonayo
✓Taifa letu na watu wake Ni Maskini ,Taifa halina laana maana Lina utajiri wa kila namna,tatizo Ni suala la mda tu

Kwa mantiki hiyo bhasi,Kuna umaskini wa vitu,fikra,umaskini wa kiroho nk,vyote hizi hazihusiani na laana Bali Ni utashi wa mtu binafsi katika kupambana na kuboresha mazingira yake
Umasikini wa fikra.
 
Umasikini ni kushindwa kupata nahitaji yote muhimu ya kila siku na swala hilo , ndiyo la kulitafutia ufumbuzi.(Chakula,Makazi,Makazi) huduma za kiafya Pamoja na elimu.

Swala la kuwa kama elon musk ni swala lingine
Ndio mana jitihada za kupambana nao hazifui dafu. Litazame vizur hili
 
Habari ndugu zangu, imenilazimu kuandika kupinga dhana iliyotolewa na member mwenzetu tajwa hapo juu

Hili Ni bandiko linalolenga kukosoa mtazamo wake juu ya dhana fikirishi ya umaskini ambayo aliieleza Kama "Laana" Jambo ambalo si sahihi

✓Kwanza ameshindwa kuonesha ya kwamba binadamu awe na Nini au akoswe Nini ndo awe maskini hii Ni kwasababu dhana ya umaskini Haina maana moja, Maskini wa Dar yaweza kuwa Tajiri Tarime

✓Biblia na vitabu vingine vya kiroho vinatambua dhana ya umaskini na vimeshauri tuwasaidie kwa kuweka hazina zetu juu Yao kwa kuwapa mavazi na chakula kwakuwa tupo nao siku zote
✓Umaskini siyo Laana Kama anavyohisi mwenzetu,Binadamu anaweza zaliwa maskini,yeye kuwa tajili Ni juhudi zake binafsi

Naomba kuwasilisha ndugu zangu
Changamoto niionayo hapa ni kwamba wote hamjui definition halisi ya LAANA ni Nini.
 
Changamoto niionayo hapa ni kwamba wote hamjui definition halisi ya LAANA ni Nini.
Tiririka..

Laana ni nini?

Kwanini baadhi ya watu akiwamo ROBERT HERIEL na Kalunya wanahusisha laana na umasikini, wakishinikiza kwamba umasikini ni laana

Wewe kwa uelewa wako na vielelezo vyako unaamini

Laana ni nini?

Tupe hio definition halisi ya Laana
 
Back
Top Bottom