Habari ndugu zangu,imenilazimu kuandika kupinga dhana iliyotolewa na member mwenzetu tajwa hapo juu
Hili Ni bandiko linalolenga kukosoa mtazamo wake juu ya dhana fikirishi ya umaskini ambayo aliieleza Kama "Laana" Jambo ambalo si sahihi
✓kwanza ameshindwa kuonesha ya kwamba binadamu awe na Nini au akoswe Nini ndo awe maskini hii Ni kwasababu dhana ya umaskini Haina maana moja,Maskini wa Dar yaweza kuwa Tajiri Tarime
✓Biblia na vitabu vingine vya kiroho vinatambua dhana ya umaskini na vimeshauri tuwasaidie kwa kuweka hazina zetu juu Yao kwa kuwapa mavazi na chakula kwakuwa tupo nao siku zote
✓Umaskini siyo Laana Kama anavyohisi mwenzetu,Binadamu anaweza zaliwa maskini,yeye kuwa tajili Ni juhudi zake binafsi
Naomba kuwasilisha ndugu zangu
Mkuu Kwanza Nashukuru Kwa kunipinga na kutoa Mtazamo wako dhidi ya mtazamo wangu.
Turudi kwenye Mjadala.
Topic ya Poverty ipo Kidato cha tatu Kwa waliofika elimu ya Upili.
Maana ya umasikini inafahamika Kwa waliofika madarasa hayo.
Individual level umasikini ni kitendo au Hali ya mtu kukosa mahitaji yake ya msingi Kama chakula, mavazi, makazi. Ingawaje yapo nahitaji mengine ya ziada yaliyoongezeka ambayo nayo yanachukuliwa Kama sehemu ya basic needs mfano Sex, mawasiliano ya simu n.k.
Tubakie katika maana hiyo ya msingi..
Ukishakuwa masikini upo katika kundi la wenye Laana ukubali au ukatae.
KIVIPI?
LAANA ni neno ambalo moja Kwa moja linahusu suala la kiimani, miungu, supernatural power,.
Mtu yeyote ukimsikia anasema kuhusu Laana basi ujue anaamini katika miungu.
Hakuna miungu hakuna laana.
Kisayansi hakuna laana. Ila kiimani Laana Ipo.
Kinyume cha Laana ni Baraka.
Unaposema baraka pia unazungumzia mambo ya kiimani, miungu na mambo dhahania.
Kisayansi hakuna kitu inaitwa Baraka
LAANA NI NINI?
Laana ni tamko, Kauli anayotamkiwa mtu au kikundi cha watu iliyodhamiria kudhuru au kuleta madhara, maangamizo, baada ya mtu au watu hao kuvunja kanuni au amri Fulani.
Laana inahusu zaidi miungu na mara nyingi hutolewa Kwa nguvu za miungu, au Kwa jina la miungu.
Kwa mujibu wa maandiko, laana za awali zilizotamkwa binadamu ni Kama ifuatavyo;
1. Kifo au mauti
2. Njaa( ardhi imelaaniwa hivyo mwanaume atakula Kwa jasho)
3. Mwanamke kuzaa Kwa uchungu Ile ni laana.
Kwa kifupi Laana no adhabu huku Baraka ni Zawadi.
Sasa kivipi umasikini uwe ni laana? Na iweje Masikini wawe wamelaaniwa?
Ili mtu aitwe masikini kuna viashiria, vifuatavyo ni baadhi ya viashiria kuwa mtu au jamii Fulani ni masikini
1. High mortality Rate/kiwango kikubwa cha wanaokufa.
Vifo vya watoto wachanga kuwa vingi na watu kufa mapema kabla ya uzee kutokana na sababu nyingi tuu ikiwemo Huduma duni za Afya, njaa, elimu ndogo n.k.
Kumbuka kifo ni laana na umasikini unapelekea vifo kuwa vingi. Biblia inaeleza wazi kuhusu Hilo.
2. Makazi duni na maisha duni/ poor living conditions.
Mtu anaishi makazi mabovu, mazingira hatarishi ni moja ya viashiria kuwa mtu au jamii Fulani ni masikini.
Ni laana kuishi makazi Duni. Tafsiri ya moja Kwa moja ni adhabu kuishi makazi duni, machafu, mbavu za mbwa.
3. Kiwango kikubwa cha wajinga/ High Illiteracy rate.
Kukosa elimu pia ni Dalili ya Masikini, yaani kukosa elimu ni sehemu ya laana.
Biblia inasema, watu wangu wanaangamia Kwa Kukosa Maarifa.
Laana kumbuka ndio kuangamia kwenyewe.
Ukiwa huna elimu utashindwa kuishi maisha mazuri, utakuwa mjingamjinga.
Sasa hapo kwenye elimu ndio kuna Formal, non-formal and Informal education.
Yaani kuwa mjinga tuu ni laana tosha, maana ukiwa na akili huwezi kuwa Masikini.
4. Njaa/Hunger
Kula Mlo mmoja, utapiamlo, kukosa kabisa Kula chakula ni Dalili za umasikini.
Kumbuka Njaa ni laana kama unabisha nitakuleta vifungu vyakutosha tuu! Kumbuka Ardhi ililaaniwa ili watu wafe njaa😂😂.
5. Maradhi
Maradhi husababisha umasikini, na umasikini husababisha Maradhi. Yaani Maradhi na umasikini ni marafiki Pacha ukimjumlisha na ndugu Yao ujinga.
Kumbuka Maradhi pia ni laana, na Biblia inaeleza
Pia kumbuka Yesu alitoa Laana yake pia kuwa asiyefanya kazi Kula na asile yaani afe kwanjaa.
Na njaa ni moja ya indicator muhimu ya umasikini.
Soma kumbukumbu la Torati 28
Utaona ni Kwa namna gani Umasikini ni laana.
Masikini wasaidie lakini wenye uhitaji/watakaokuomba msaada Ila kujipendekeza Kwa masikini wasiohitaji msaada wako nakuhakikishia matokeo yake utayapata na yatakuwa mabaya zaidi
Umasikini ni laana.
Masikini wamelaaniwa.
Kumbuka zipo laana za watu wote na zipo laana za kundi Fulani. Kifo ni laana ya kila kiumbe kilichozaliwa na Mwanamke, umasikini ni laana ya kundi Fulani la watu.
Kama ilivyo zipo baraka za watu wote na zipo baraka za watu wakundi Fulani. Nuru ya jua au mvua au hewa ni baraka Kwa watu wote, lakini madini, uzuri, Utajiri, nguvu ni baraka Kwa kundi Fulani la watu.
Huo ndio ukweli.
Umasikini ndio ushetani wenyewe, ndio laana, ni mauti.