Nampinga Robert Heriel kuhusu dhana ya umasikini

Mkuu Kwanza Nashukuru Kwa kunipinga na kutoa Mtazamo wako dhidi ya mtazamo wangu.

Turudi kwenye Mjadala.

Topic ya Poverty ipo Kidato cha tatu Kwa waliofika elimu ya Upili.
Maana ya umasikini inafahamika Kwa waliofika madarasa hayo.
Individual level umasikini ni kitendo au Hali ya mtu kukosa mahitaji yake ya msingi Kama chakula, mavazi, makazi. Ingawaje yapo nahitaji mengine ya ziada yaliyoongezeka ambayo nayo yanachukuliwa Kama sehemu ya basic needs mfano Sex, mawasiliano ya simu n.k.
Tubakie katika maana hiyo ya msingi..

Ukishakuwa masikini upo katika kundi la wenye Laana ukubali au ukatae.
KIVIPI?

LAANA ni neno ambalo moja Kwa moja linahusu suala la kiimani, miungu, supernatural power,.
Mtu yeyote ukimsikia anasema kuhusu Laana basi ujue anaamini katika miungu.
Hakuna miungu hakuna laana.

Kisayansi hakuna laana. Ila kiimani Laana Ipo.
Kinyume cha Laana ni Baraka.
Unaposema baraka pia unazungumzia mambo ya kiimani, miungu na mambo dhahania.
Kisayansi hakuna kitu inaitwa Baraka

LAANA NI NINI?
Laana ni tamko, Kauli anayotamkiwa mtu au kikundi cha watu iliyodhamiria kudhuru au kuleta madhara, maangamizo, baada ya mtu au watu hao kuvunja kanuni au amri Fulani.
Laana inahusu zaidi miungu na mara nyingi hutolewa Kwa nguvu za miungu, au Kwa jina la miungu.

Kwa mujibu wa maandiko, laana za awali zilizotamkwa binadamu ni Kama ifuatavyo;
1. Kifo au mauti
2. Njaa( ardhi imelaaniwa hivyo mwanaume atakula Kwa jasho)
3. Mwanamke kuzaa Kwa uchungu Ile ni laana.

Kwa kifupi Laana no adhabu huku Baraka ni Zawadi.

Sasa kivipi umasikini uwe ni laana? Na iweje Masikini wawe wamelaaniwa?

Ili mtu aitwe masikini kuna viashiria, vifuatavyo ni baadhi ya viashiria kuwa mtu au jamii Fulani ni masikini

1. High mortality Rate/kiwango kikubwa cha wanaokufa.
Vifo vya watoto wachanga kuwa vingi na watu kufa mapema kabla ya uzee kutokana na sababu nyingi tuu ikiwemo Huduma duni za Afya, njaa, elimu ndogo n.k.

Kumbuka kifo ni laana na umasikini unapelekea vifo kuwa vingi. Biblia inaeleza wazi kuhusu Hilo.

2. Makazi duni na maisha duni/ poor living conditions.
Mtu anaishi makazi mabovu, mazingira hatarishi ni moja ya viashiria kuwa mtu au jamii Fulani ni masikini.
Ni laana kuishi makazi Duni. Tafsiri ya moja Kwa moja ni adhabu kuishi makazi duni, machafu, mbavu za mbwa.

3. Kiwango kikubwa cha wajinga/ High Illiteracy rate.
Kukosa elimu pia ni Dalili ya Masikini, yaani kukosa elimu ni sehemu ya laana.
Biblia inasema, watu wangu wanaangamia Kwa Kukosa Maarifa.
Laana kumbuka ndio kuangamia kwenyewe.
Ukiwa huna elimu utashindwa kuishi maisha mazuri, utakuwa mjingamjinga.
Sasa hapo kwenye elimu ndio kuna Formal, non-formal and Informal education.

Yaani kuwa mjinga tuu ni laana tosha, maana ukiwa na akili huwezi kuwa Masikini.

4. Njaa/Hunger
Kula Mlo mmoja, utapiamlo, kukosa kabisa Kula chakula ni Dalili za umasikini.
Kumbuka Njaa ni laana kama unabisha nitakuleta vifungu vyakutosha tuu! Kumbuka Ardhi ililaaniwa ili watu wafe njaa😂😂.

5. Maradhi
Maradhi husababisha umasikini, na umasikini husababisha Maradhi. Yaani Maradhi na umasikini ni marafiki Pacha ukimjumlisha na ndugu Yao ujinga.
Kumbuka Maradhi pia ni laana, na Biblia inaeleza

Pia kumbuka Yesu alitoa Laana yake pia kuwa asiyefanya kazi Kula na asile yaani afe kwanjaa.
Na njaa ni moja ya indicator muhimu ya umasikini.

Soma kumbukumbu la Torati 28
Utaona ni Kwa namna gani Umasikini ni laana.

Masikini wasaidie lakini wenye uhitaji/watakaokuomba msaada Ila kujipendekeza Kwa masikini wasiohitaji msaada wako nakuhakikishia matokeo yake utayapata na yatakuwa mabaya zaidi

Umasikini ni laana.
Masikini wamelaaniwa.

Kumbuka zipo laana za watu wote na zipo laana za kundi Fulani. Kifo ni laana ya kila kiumbe kilichozaliwa na Mwanamke, umasikini ni laana ya kundi Fulani la watu.

Kama ilivyo zipo baraka za watu wote na zipo baraka za watu wakundi Fulani. Nuru ya jua au mvua au hewa ni baraka Kwa watu wote, lakini madini, uzuri, Utajiri, nguvu ni baraka Kwa kundi Fulani la watu.

Huo ndio ukweli.

Umasikini ndio ushetani wenyewe, ndio laana, ni mauti.
Kwanza hakuna laana, swala la laana linabaki kuwa katika mtizamo binafsi na sio uhalisia
 
Andiko lako linaonesha kuwa umasikini ni ujinga.
Na mimi pia nimeamua Kuona hivyo ...
Ujinga waweza kuondoshwa,

Kama uko na resources karibu unaweza kutupatia maana mbali mbali za laana/curse ujinga/ignorance.

Kama vile umechanganya mada mkuu Heriel Umemix science Pamoja na dini Andiko lako linaleta mkanganyiko
 
Itapendeza zaidi kama mijadala utafanyika KWA muktadha wa kielimu zaidi/Kusini Kuzingatia Kutoa maana binafsi pia kutoka KWA watu wengine Ili kuleta uwiano sahihi na maana , mijadala huu uwe wa Kusini zaidi.
 
Umaskini sio laana
Kuna maskini wa kipato ila ana utajiri wa roho na mawazo.

Kuna tajiri wa kipato kwa sababu sio wote wenye pesa wanatafuta kwa nguvu zao na akili zao lakini ni maskini wa roho na akili.

Huyu mwenye utajiri wa maarifa pamoja na akili hata akizaliwa familia maskini anachance kubwa ya kutoboa na wakati huyu mwenye pesa na ni maskini wa akili na maarifa ana chance kubwa ya kufilisika.

Umaskini na utajiri wa mtu huanzia kwenye fikra zake .
 
Hivi hakuna aina za umaskini, maana wote mmejikita kwenye uchumi tu. Mfano nikisema maskini wa roho, afya, elimu, nitakuwa sahihi
 
Andiko lako linaonesha kuwa umasikini ni ujinga.
Na mimi pia nimeamua Kuona hivyo ...
Ujinga waweza kuondoshwa,

Kama uko na resources karibu unaweza kutupatia maana mbali mbali za laana/curse ujinga/ignorance.

Kama vile umechanganya mada mkuu Heriel Umemix science Pamoja na dini Andiko lako linaleta mkanganyiko

Soma vizuri uelewe.
Hakuna sehemu nimechanganya Sayansi na Dini.
Soma, tafakari, elewa
 
Umaskini sio laana
Kuna maskini wa kipato ila ana utajiri wa roho na mawazo.

Kuna tajiri wa kipato kwa sababu sio wote wenye pesa wanatafuta kwa nguvu zao na akili zao lakini ni maskini wa roho na akili.

Huyu mwenye utajiri wa maarifa pamoja na akili hata akizaliwa familia maskini anachance kubwa ya kutoboa na wakati huyu mwenye pesa na ni maskini wa akili na maarifa ana chance kubwa ya kufilisika.

Umaskini na utajiri wa mtu huanzia kwenye fikra zake .

Umenipuuza. Fresh
 
Pesa unazo ni wewe, hoja haijadili mtu mmoja mmoja…. umaskini [kwa maana halisi ya masikini] ni laana.

Okay tuachane na notes za darasani, sijui kukosa chakula, mavazi na malazi. Umasikini ni nini? Maana naona hata hapa kuna masikini wa hoja na fikra ni mimi na watu wachache sana ndo matajiri.

Hivi Robert Heriel na Mo Dewj nani ana laana na nani ana baraka? Na vp tukimlinganisha huyu rafiki yetu Tanzania na Marekani, nani ni nani?

Nataka kusema hivi kuna mtu kukosa chakula, mavazi na malazi (notes), kwa kusababishiwa, mipango mibovu ya baba au mama mwenye nyumba, hapa nyumba nazungumzia ka-Tz ketu. Watu wengi sana huwa tunakosa hayo mahitaji sema tu kuna wachache ni wajanja, wanajua kuiba, hawa ukiwakuta kwenye ofisi zao na nyumba zao utasema wamebarikiwa kumbe wamelaaniwa vibaya sana.

Hebu tutulize akili wakati tunaendelea kujadili hii mada ili tusijichanganye tukakubaliana kwamba laana ni baraka kumbe baraka ndo laana.
 
Na hii imekaaje? "Kuzaliwa masikini sio kosa ila kufa masikini ni kosa".

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo kaka ni nguvu ya upambanaji,Mtoto anapozaliwa hapa duniani Alitakiwa afurahi kwa kuletwa katika mazingira haya rakini badala yake Hulia kwa uchungu kunakomaanisha Mwanzo wa mapambano ya either kuwa Tajiri au afanye mchezo umaskini umuvae,

Kufa Maskini kunaepukika fanya kazinkwa juhudi,mtangulize Baba Mungu wa Mbinguni utafanikiwa
 
Tafsiri ya umasikini utofautiana kulingana na Jamii
Umasikini umasikin tu. Asikudanganye mtu yoyote ILA una levo. Mwenye ngo'mbe wa2 anamuona mwenzie mwenye mbuzi 6 masikini. Mwenye mbuzi sita anamuona mwenye kuku ishirini masikini. Mwenye kuku nae at asema Kuna mwinzie hana kuku. Asie na kuku atakwmbia Kuna mtu hata PA kulala hana. Mlala nje nae atakwmbia Kuna mwenzie a nalala nje hata hela Y kula amekosa 😂. Umaskini wa maisha ya kisasa 'moderniity' au mfumo wa kikapitalist ni umasikin wa KUTOMILIKI
 
Kuna kitu naomba nikiweke Sawa hapa. Umaskini na utajiri SIO mipango ya mungu. Unasababishwa na mfumo wa maisha tunaoishi. Nitatoa mfano mmoja mzuri Sana, jamii zile za kijima 'foragers' Kwa watAnzania tunawajua wahadza au sandawe. Wale jamaa hawanaga maskin wala tajiri. Mifumo ya maisha yao Ina njia za umiliki wa watu wote 'SOCIALISM' ambao hakuna anaemiliki kitu. Vyote Kuanza ardhi, nyama, silaha, nguo mpaka watoto ni vya watu wote. (mf. Mtot wao kule anaitwa jina moja tu 'han' g-a' au 'duduqwe' halina baba wala babu). Mfumo ule wa maisha hauzalishi masikini wala tajiri wote wanafanana tu.
Nb: nimetumia nadharia ya kisosholojia kuelezea hili. JAMENI NATAFUTA SEHEM Y INTERN ACHENI SIASA 😊
 
Back
Top Bottom