Nampinga Robert Heriel kuhusu dhana ya umasikini

"Masikini wasaidie lakini wenye uhitaji/watakaokuomba msaada Ila kujipendekeza Kwa masikini wasiohitaji msaada wako nakuhakikishia matokeo yake utayapata na yatakuwa mabaya zaidi"

Ahsant kwa kulegeza msimamamo ndugu yangu ROBERT HERIEL Naamini Sasa Kwa ufaraguzi wa Members wenzangu wa Jf Kuna haya nimejifunza
✓Kumbe hata utajiri waweza kuwa laana iliyoboreshwa,rejea wanaopata utajiri kwa matendo ya hovyo Kama vile mauaji,rushwa,kafara nk kwa nje unaweza kudhani Wana amani lakini kinyume chake Ni sahihi
✓Laana Ni dhana binafsi,ukiamini kuwa umelaaniwa hakika itakuwa hivyo,ukiamini pia umebarikiwa pia maisha yako yatakuwa hivyo,
✓Maskini wengi wanaamini kuwa wamelaaniwa na wameumbwa wawe hivyo(Babu,baba woote Maskini)Hivyo huacha kujishughulisha kwa bidii yenye ubunifu ili waweze kujikwamua katika Hali waliyonayo
✓Taifa letu na watu wake Ni Maskini ,Taifa halina laana maana Lina utajiri wa kila namna,tatizo Ni suala la mda tu

Kwa mantiki hiyo bhasi,Kuna umaskini wa vitu,fikra,umaskini wa kiroho nk,vyote hizi hazihusiani na laana Bali Ni utashi wa mtu binafsi katika kupambana na kuboresha mazingira yake
 
Laana ipo Kama unaamini katika Dini au miungu.

Kama hauamini basi laana hakuna.
Kwamba kuna vitu usipo viamini, uhalisia wake unapotea?

Laana ni perception na interpretations ya mtu binafsi, hata katika wigo wa kidini bado laana haiko universal

Ni makubaliano tu ya watu kuwa jambo fulani lichukuliwe kama laana na jambo fulani lionekane baraka
 
Umasikini ni umasikini tuu.
Hata ukiu-classify.

Masikini anajijua yeye ni masikini hata kama atajifanya hajui Ila nafsini anajua yeye ni masikini. Hasa anapokuwa mhitaji zaidi.
 
Kwamba kuna vitu usipo viamini, uhalisia wake unapotea?

Laana ni perception na interpretations ya mtu binafsi, hata katika wigo wa kidini bado laana haiko universal

Ni makubaliano tu ya watu kuwa jambo fulani lichukuliwe kama laana na jambo fulani lionekane baraka

Nimejibu kimtazamo.
Laana kimtazamo Kama unadhani haipo basi haipo lakini kiuhalisia IPO hata ukiwa na mtazamo wa kivyovyote.

Laana sio perception na interpretation ya mtu ni Jambo halisi na lipo kwenye jamii zote Duniani.
 
Naungana na @robertheriel KUWA UMASKINI NI LAANA.
Kwa kuwa ni kipimo kuwa baraka hazijakufikia.
Kama unalaana hakuna kitu utafanya kikafanikiwa maana kazi za mikono yako hazijabarikiwa.
Katika Biblia Kitabu Cha Isaya kinasema ,"Mwanangu Umebarikiwa mashambani na mijini pia".
Tofautisha walemavu wa viungo vya mwili wanaohitaji msaada wetu na mtu aliyekamilika na nguvu zake ila ni fukara wa kutupwa.
Na maliza kwa kusema UMASKINI ni roho kamili + Ni LAANA
 
Watu hatupendi ukweli.

Tunashindwa kuelewa kuwa kuna laana tunaweza kuziondoa hata kama tumezikuta.
Kwa kuomba toba ya makosa yetu na Wazee wetu.
Na kufanya kazi Kwa juhudi na maarifa
 
Naungana na @robertheriel KUWA UMASKINI NI LAANA.
Kwa kuwa ni kipimo kuwa baraka hazijakufikia.
Kama unalaana hakuna kitu utafanya kikafanikiwa maana kazi za mikono yako hazijabarikiwa.
Katika Biblia Kitabu Cha Isaya kinasema ,"Mwanangu Umebarikiwa mashambani na mijini pia".
Tofautisha walemavu wa viungo vya mwili wanaohitaji msaada wetu na mtu aliyekamilika na nguvu zake ila ni fukara wa kutupwa.
Na maliza kwa kusema UMASKINI ni roho kamili + Ni LAANA
Ndo mana umetumia bible. Hapa labda tungechagua Nn kitu Mike kuelezea hili tatizo la umasikin. Ukitumia dini majibu ya laana na yanayofanan yatameki sensi. Lakin ukitumia sayansi, dini na mungu hatoonekana, na majibu ya laana hayameki sensi
 
Umasikini ni umasikini tu

Watu wanaleta maneno maneno!

Umasikini ni mbaya Sana. Ninauchukia mno.

Ukiujua au kuuguliwa huko Hospitalini unahangaika na mgonjwa hapohapo unahangaishwa na mawazo.

Unawaza chakula cha watoto, kumvalisha na kumtunza mke, unawaza wazazi, unaweza Kodi ya nyumba, yaani!
Inashangaza watu wanajifanya hawajui maana ya Masikini ilhali kila siku wanailaumu serikali Kwa kutoza Kodi masikini 😀😀
 
Ndo mana umetumia bible. Hapa labda tungechagua Nn kitu Mike kuelezea hili tatizo la umasikin. Ukitumia dini majibu ya laana na yanayofanan yatameki sensi. Lakin ukitumia sayansi, dini na mungu hatoonekana, na majibu ya laana hayameki sensi
Scientifically Kila mtu anapata riziki kulingana na thinking capacity yake Mwenye uwezo mdogo wa kufikiri ataangukia vibarua vya kwenye mkonge wakati mwingine aliekaa darasani due to his high intelligence anaangukia BOT.
God, science and religion depend on one another to finalize findings.
 
Umasikini ni mbaya Sana. Ninauchukia mno.

Sawa kabisa, inaonekana unachokichukia ni UMASIKINI sio MASIKINI mpaka kufikia kuwavisha LAANA. Tukubaliane tu kwamba hata MATAJIRI wana LAANA (lakini tusizitaje)

Hakuna mtu anapenda umasikini, wote tunauchukia na tunapambana mno kujikwamua. Walioko BOT wanapambana kujikwamua na sisi huku shambani na mtaani tunapambana haswa.

MASIKINI wengi tunasababishiwa UMASIKINI, umetoa mfano mzuri wa tozo.

Leo hii naamrishwa kulipa tozo zote hizi na mimi bila ihana natii, najinyima katika kila muamala nalipa tozo mwishoni napungukiwa mpaka balance ya kununua kitoweo napiga pasi ndefu mpaka jioni ndo nakula, hivi mimi ni masikini? No thank you, mimi ni tajiri mwenye UMASIKINI (wa kusababishiwa)
 
God, science and religion depend on one another to finalize findings.[/B]

Where is politics? Assuming by science you mean natural science.

Hata hiyo high IQ na BOT,,,, japo simkubali sana mwenda zake alitufumbua kuwa si wote walioko huko wana huo uwezo wa kuwa intelligent,,,wengi ni udugu tu,,,, connection (politics).

SIASA yetu inazalisha UMASIKINI mkubwa wa MWILI na AKILI, matokeo yake tunakuwa MASIKINI na kuanza kulaumiana kwa kushindwa kutofautisha UMASIKINI na MASIKINI.

Tusaidiane kutafuta suluhisho la tatizo - UMASIKINI, wala tusijione kuwa wenye uwezo mkubwa wa kufikiria kwa hivyo vijisenti tunavyomiliki.
 
Nimejibu kimtazamo.
Laana kimtazamo Kama unadhani haipo basi haipo lakini kiuhalisia IPO hata ukiwa na mtazamo wa kivyovyote.

Laana sio perception na interpretation ya mtu ni Jambo halisi na lipo kwenye jamii zote Duniani.
Jamii za ujinga ndio zina hizo imani, katika jamii za wasomi ni ngumu kukuta watu wana jaji jambo katika dhana ya laana wakati jambo hilo linaelezeka vizuri bila laana
 
Jamii gani Kwa mfano?
Wazungu?
Wadachi?
Waajemi?
Wachina?
Wayahudi?
Warusi?
Waarabu?
Waafrika?
Wahindi?

Nitajie hiyo jamii ya wasomi MKUU!
Usiwe ukawa ukadanganywa na Hollywood au filamu hizi za kiutandawazi.

Hakuna msomi au mwenye akili zilizotimia asiyeamini mambo ya Laana na baraka. Hakuna!
 
Sizungumzii race, nazungumzia mtu yeyote aliyeelimika mwenye uwezo wa kufikiria kwa sauti hawezi kujaji jambo katika mizani ya laana ilihali hilo jambo linaelezeka vizuri bila kuweka dhana hizo

Kusema laana inafanya kazi kwa wanao amini huo ni uwongo wa kifikra.

Uwongo kama huo ndio uliosababisha vita ya maji maji watu wafe kijinga.
 
Back
Top Bottom