mwankuga
JF-Expert Member
- Aug 30, 2010
- 334
- 120
Nampenda sana Samweli Sitta.Sitta mara nyingi huwa hafichi mawazo yake na uchu wa madaraka aliyonayo.Mwaka 2009 kulikuwa na tishio la kumfukuza Sitta uanachama wa CCM.Mara moja nikapenda move hiyo,na nikawaambia CCM kwamba haraka wamfukuze Sitta.Nilikuwa napenda Sitta afukuzwe uanachama wa CCM ili wananchi waone sura halisi ya Samwel Sitta.Na hata alipoenguliwa katika kinyang'anyilo cha Uspika,nilifurahi kwa sababu nilitaka kumwona Sitta mwenye madaraka na Sitta asiye na madaraka.
Lakini kwa kuwa Sitta ni mroho wa madaraka na kupenda kujikweza akashawishiwa kupewa uwaziri,naye akakubali kwa kuwa anajua kuwa bila madaraka hawezi kuwa Sitta wa sasa.Sasa anataka kukwea kileleni,na wala hana break.Amekuwa akitoa kauli mbalimbali ambazo zinaonyesha kuikosoa serikali ya CCM ambayo yeye ni miongoni mwao.Rudisha hisia zako nyuma kumbuka Sitta alivyoendesha suala la Richmond lililopelekea Lowassa kujiuzuru uwaziri mkuu,lakini mwisho wa siku hakuna kilichofanyika.
Sitta alikuwa anaongoza kundi la Mitume Kumi na Mbili wakati huo,ambalo ndilo lililoibuka tena(Sitta,Mwakyembe,Sendeka,Anna Kilango,Lazaro Nyarando,Stella Manyanya n.k) wanataka kutuaminisha kwama wao ni tofauti na wana CCM wengine.Wanataka kutuaminisha kuwa wao wapo kwa ajili ya masilahi ya Watanzania.Kundi hili limeibuka huko Mbeya na kutoa kauli za kuipinga serikali yao na kuwaunga mkono wapinzani,huku hoja kama hizo zinapotolewa na wabunge wa CHADEMA NA NCCR-MAGEUZI zinapingwa.
Kundi hili la mitume ni hatari sana kama wananchi hawatakuwa makini.Wote hao wanaongozwa na uchu wa madaraka,na sasa wanaona kuna nafasi ya kupenyeza mgombea wao katika uchaguzi wa 2015 kwa kuwa Kikwete hatagombea tena.Sitta anajua anachotaka.Wakati wa uchaguzi wa 2005,Sitta alikuwa upande wa mtandao uliomsaidia Kikwete kupata urais.Leo hii wana mtandao hao hawapatani,mulizeni Sitta nini kilichowagombanisha.
Kama Sitta atakuwa Rais au hata Waziri Mkuu ni hatari sana kuliko hata Pinda.Muda aliokaimu uongozi wa Shughuli za Bunge wakati Pinda hayupo,matamshi yake yameonyesha kuwa ni hatari sana,hasa walipowaita wapinzani kuwa ni wanafiki,huku akisahau kuwa Sitta ni mnafiki namba moja katika nchi hii.Matamshi aliyoyatoa jana Mbeya yanatofauti gani na wanayoyatoa wakina Dr.Slaa.CCM ni CCM tu.Sitta na wenzake ni walewale.Kama tutawapa nafasi nchi itavurugika zaidi ya hali ya sasa.