Nampenda sana Mhe,Samwel Sitta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nampenda sana Mhe,Samwel Sitta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwankuga, Jul 17, 2011.

 1. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Nampenda sana Samweli Sitta.Sitta mara nyingi huwa hafichi mawazo yake na uchu wa madaraka aliyonayo.Mwaka 2009 kulikuwa na tishio la kumfukuza Sitta uanachama wa CCM.Mara moja nikapenda move hiyo,na nikawaambia CCM kwamba haraka wamfukuze Sitta.Nilikuwa napenda Sitta afukuzwe uanachama wa CCM ili wananchi waone sura halisi ya Samwel Sitta.Na hata alipoenguliwa katika kinyang'anyilo cha Uspika,nilifurahi kwa sababu nilitaka kumwona Sitta mwenye madaraka na Sitta asiye na madaraka.

  Lakini kwa kuwa Sitta ni mroho wa madaraka na kupenda kujikweza akashawishiwa kupewa uwaziri,naye akakubali kwa kuwa anajua kuwa bila madaraka hawezi kuwa Sitta wa sasa.Sasa anataka kukwea kileleni,na wala hana break.Amekuwa akitoa kauli mbalimbali ambazo zinaonyesha kuikosoa serikali ya CCM ambayo yeye ni miongoni mwao.Rudisha hisia zako nyuma kumbuka Sitta alivyoendesha suala la Richmond lililopelekea Lowassa kujiuzuru uwaziri mkuu,lakini mwisho wa siku hakuna kilichofanyika.

  Sitta alikuwa anaongoza kundi la Mitume Kumi na Mbili wakati huo,ambalo ndilo lililoibuka tena(Sitta,Mwakyembe,Sendeka,Anna Kilango,Lazaro Nyarando,Stella Manyanya n.k) wanataka kutuaminisha kwama wao ni tofauti na wana CCM wengine.Wanataka kutuaminisha kuwa wao wapo kwa ajili ya masilahi ya Watanzania.Kundi hili limeibuka huko Mbeya na kutoa kauli za kuipinga serikali yao na kuwaunga mkono wapinzani,huku hoja kama hizo zinapotolewa na wabunge wa CHADEMA NA NCCR-MAGEUZI zinapingwa.

  Kundi hili la mitume ni hatari sana kama wananchi hawatakuwa makini.Wote hao wanaongozwa na uchu wa madaraka,na sasa wanaona kuna nafasi ya kupenyeza mgombea wao katika uchaguzi wa 2015 kwa kuwa Kikwete hatagombea tena.Sitta anajua anachotaka.Wakati wa uchaguzi wa 2005,Sitta alikuwa upande wa mtandao uliomsaidia Kikwete kupata urais.Leo hii wana mtandao hao hawapatani,mulizeni Sitta nini kilichowagombanisha.

  Kama Sitta atakuwa Rais au hata Waziri Mkuu ni hatari sana kuliko hata Pinda.Muda aliokaimu uongozi wa Shughuli za Bunge wakati Pinda hayupo,matamshi yake yameonyesha kuwa ni hatari sana,hasa walipowaita wapinzani kuwa ni wanafiki,huku akisahau kuwa Sitta ni mnafiki namba moja katika nchi hii.Matamshi aliyoyatoa jana Mbeya yanatofauti gani na wanayoyatoa wakina Dr.Slaa.CCM ni CCM tu.Sitta na wenzake ni walewale.Kama tutawapa nafasi nchi itavurugika zaidi ya hali ya sasa.
   
 2. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,056
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Mmmh! Japo ya moto ngoja ninywe maji kidogo. Umeme hakuna huku,...! Nitarudi na maoni punde!
   
 3. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Nampenda Sitta!!!!
   
 4. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kuna vilaza watakuja kukupinga
   
 5. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,798
  Likes Received: 36,830
  Trophy Points: 280
  Kuhusu swala la unafiki wa Sita liko wazi kabisa, Ni mtu anayependa kuonekana jeshi la mtu mmoja, anapenda kuonekana anauwezo zaidi ya wengine wote, Anapojitokeza mtu yoyote mwenye kasi sawa na Sita, yeye humchukia na kutaka jamii imuone ni mtu exception sana. Yuko tayari kuonyesha ubabe ili mradi jamii imuone mchapa kazi, CCJ itaendelea kumtafuna.
   
 6. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  nimaono yako mkuu..:A S thumbs_up:
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Ni fisadi yule mzee tena wa nguvu na mwepesi kulia kilia .Anajiita mtaji wa Urais kesha isha na hali ya juzi ndiyo kajimaliza kabisa kabisa .Sitta ni kibaka mwingine na hana uchungu na Taida hata mara moja .
   
 8. data

  data JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,787
  Likes Received: 6,559
  Trophy Points: 280
  mimi sijui
   
 9. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  i write what i like..
   
 10. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  sijamsikia MS siku mingi natamani kumsikia anasemaje
   
 11. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #11
  Jul 17, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,222
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Not so fast...

  Baada ya kuisikiliza hotuba yake jana, na kuuona mwitikio wa wananchi nimelazimika kufikiri upya....
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Jul 17, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  nakupenda sana wewe kwa kuwa muwazi hata kama huna point
   
 13. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #13
  Jul 17, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  naungana na mtoa hoja sitta ni mnafiki na mroho wa madaraka saaana ukifuatilia ktk nasaba zake hilo pia liko ukoo wa chief fundikira wa tbr ni upande wa mamayake yeye kwao ni shinyanga ukoo wa wataalamu wa kurudisha ng'ombe waliopotea ''ng'wana jishosha'' yeye kalowea upande wa mama na anajifanya ukoo wa kichief huku wasukuma ni patrilinial what a shame. Hivi mbona kwenye hako ka umoja kao ''CCJ'' hamna muislamu? Nahisi na ajenda ya dini wanayo afu ukichunguza vizuri wengi ni wakristo wa CCT kuna nini hapo?
   
 14. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #14
  Jul 17, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  mimi nafikiri gama ni gamba tu hata kama angekuwa nani. Wananchi wanatufanya sisi wajinga wanatubadilishia chupa mvinyo uleule. Hili kundi lilokuwa mbeya jana ni ccm mpya au ni magamba yaleyale?

  Hivi wanataka tuamini kwamba ni ccm mpya hivyo tusahau waliyotufanyia?

  Kama wanadhani wanania kujisafisha basi magamba yote yaachie wachague watu ambao hawakuwahi kuwa kwenye hii ccm ya sasa. Haiwezeka sita yulyule toka 60s anataka aendelea eti amejivua gamba. Huu ni ujinga ambao wanaweza kuwandaganya watoto wao na watu waliowasomba kwa maroli na kuwapa sh.5k.

  Yaani sisi tulidhike na geresha ya kuvua gamba halafu hawa wazee waendelee kula?

  Wajinga ndo waliwao kama unaakili huwezi hata kuhudhuria mkutano wa magamba hata kama umelipwa.
  Cdm tunaomba mrudi tena kwa wananchi muwaelezee hii dhana ya kujivua gamba maana watu wanawasikiliza ccm tu cdm hamjawaambia watu kama wanadanywa warudie matapishi yaleyale.

  Watu lazima wajue hawa wazee wanapambana kuendelea kuwafanya wananchi mbumbumbu ili waendelee kula na kipofu.

  Mungu tuasaidie kushinda hizi dhuruma.
   
 15. S

  SwaiMosha Member

  #15
  Jul 17, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Hongera Mkuu kwa kumpenda! Mr 6. Pamoja na kujifanya Mkristo saaaaana na Mapadre kumpamba jee unajua kama ana wake wasiopungua watatu????? Au Samuel siku hizi ni jina la dini gani ile??? Wanayoruhusu wake wengi.
   
 16. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #16
  Jul 17, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  funguka mkubwa.!
   
 17. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #17
  Jul 17, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,557
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  Ni kweli Sitta na kundi lake linaongozwa na chuki dhidi ya watu fulani kwa kisingizio cha maslahi kwa taifa! llishangaza watu pale mjadala wa richmond ulipozimwa bungeni huku maazimio ya kamati yakiachwa yanaelea!

  Kujiuzulu kwa Lowasa ndicho ambacho hawa akina Sitta walikiona kimeridhisha nafsi zao. Sitta ni mnafiki sana yule mzee hana uzalendo wowote anaojivika.

  Nasikitika watu wanavyoenflea kumpa sifa asizostahili huyu mzee. Kama Lowassa asingekuwa waziri mkuu kipindi kile wala huyu mzee asingekubali kuunda kamati ya bunge kuchunguza ufisadi wa Richmond! Kauli yake ndani ya bunge kwamba wapinzani ni wanafiki inamrudia mwenyewe kwakuwa yeye anaongea mambo yaleyale wanayoongea wapinzani ndani ya bunge yeye anayaesma nje ya bunge. Yupi ni mnafiki hapo?

  Natamani watanzania wote tungemuelewa mzee Sitta.
   
 18. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #18
  Jul 17, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  Sitta na nyumba ya milioni 12 kwa mwezi, halafu anajifanya mtetezi wa watanzania. Kama Slaa posho milioni 7 bila kodi huku wananchi sisi hata laki moja inatugonga.

  Sitta mwizi tu ana nyumba zake Dar anapangisha huku yeye anapangishiwa nyumba milioni 12 kwa mwezi.

  Hawa magamba siwapendi ni wezi, magwanda pia siwapendi ni wanafiki.
   
 19. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #19
  Jul 17, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  6 mnafiki nambari 1, akigombea urais ni heri hata nim'support Peter Kuga Mziray
   
 20. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #20
  Jul 17, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kumjadili Sitta ni kupoteza muda kama kumjadili Nape, CCM ni tupu mno.
   
Loading...