Nampenda sana Mhe,Samwel Sitta

[SUP]Mbeya. Cabinet minister Samuel Sitta said yesterday that people who have plunged the country into the current power crisis must bear full responsibility for their actions."It's not enough to apologise to Tanzanians for the suffering they are going through… it must be said that all those who caused this misery must be held responsible," he told a forum organised by CCM members from universities in Mbeya Region.

Mr Sitta, who is also East African Cooperation minister and former National Assembly Speaker, said Tanzania was blessed with abundant resources that could be used to generate power for domestic consumption and export. "It is due to sheer greed that the nation is now in darkness," he said without mentioning names.[/SUP]

Unampendea nini huyo uoga na unafiki? CCM walitaka kumnyang'a kadi hakawa mpole na kulalia upande wa chama na kututosa wananchi.

Hili la mgao wa umeme kama yeye anajua kuna watu wametutia gizani si aseme sio kutafuna maneno tu, mbona hajawahi kupinga bungeni wanaposema tatizo ni kina cha maji na ufundi? Kumbe kuna anayoyajua.

Kama ni mgao wa billioni 15 anazopata kikwete kila mwezi hilo mbona tunalifahamu na yeye ana ubavu, mnafiki sana huyu mzee mtata
 
Sitta alikuwa anaongoza kundi la Mitume Kumi na Mbili wakati huo,ambalo ndilo lililoibuka tena(Sitta,Mwakyembe,Sendeka,Anna Kilango,Lazaro Nyarando,Stella Manyanya n.k) wanataka kutuaminisha kwama wao ni tofauti na wana CCM wengine.Wanataka kutuaminisha kuwa wao wapo kwa ajili ya masilahi ya Watanzania.Kundi hili limeibuka huko Mbeya na kutoa kauli za kuipinga serikali yao na kuwaunga mkono wapinzani,huku hoja kama hizo zinapotolewa na wabunge wa CHADEMA NA NCCR-MAGEUZI zinapingwa.

Matamshi aliyoyatoa jana Mbeya yanatofauti gani na wanayoyatoa wakina Dr.Slaa.CCM ni CCM tu.Sitta na wenzake ni walewale.Kama tutawapa nafasi nchi itavurugika zaidi ya hali ya sasa.

Sometimes wahandishi wa habari uwa wana-mislead sana wananchi...

Jana Sitta na wenzake hawakuipinga CCM wala serikali yake, na wala hakumshutumu Ngereja wala kiongozi yeyote wa serikalini ya CCM zaidi ya mafisadi...

Alichosema ni kuwa CCM ilikuwa imelala usingizi, wenye fedha waliingia, wabadhirifu wakaingia, wakatumia nafasi zao kujinufaisha binafsi na kuishia kuingia mikataba mibovu isiyo na manufaa kwa nchi kwa ajili ya matumbo yao, matharani kwenye umeme.., wakawasahau wanyonge na kupoteza itikadi na misingi yake.

Akaomba msamaha kwa wananchi kwa niaba ya serikali kwa madudu yote yaliyotokea huko nyuma na kupelekea nchi hii yenye rasilimali nyingi ishindwe kukidhi matakwa ya wananchi wake na kuingia kwenye mgawo wa umeme, aliahidi kuwa ndani ya CCM iliyojivua gamba, haya hayatavumiliwa tena na hatua stahiki zitachuliwa.

Alisema kupitia Mwenyekiti wa CCm, Rais Kikwete, chama kimejitathimini na kuanza jitihada mahsusi za kujisafisha ili kirudi kwenye misingi yake,misingi ya Mwl Nyerere na Karume, misingi ya kuwatumikia wananchi kwa nguvu na kwa unyenyekevu mkubwa, na kuwa serikali hii sasa itakidhi matarajio ya watu wake, na kuahidi kumalizwa kwa tatizo la umeme ndani ya miaka 4 hii...

Hakuonyesha/hawakuonyesha ubinafsi kama ilivyoandikwa, japo alidokeza kuhusu changamoto walizopitia kwenye harakati za kupambana na maovu ndani ya CCM(iliyokuwa usingizini/kabla ya uamuzi wa kujivua gamba) na kukaribia kunyang'anywa kadi, lakini walipambana ndani ya chama na sasa CCM mpya imezaliwa chini ya Jemedari wao Mkuu Kikwete, na kuwa serikali ya CCM hii sasa itakayowajibika kwa wananchi kwa nguvu sana na sikuzote itaweka maslahi ya wananchi mbele, wanaojali maslahi ya tumbo hawatakuwa na nafasi.

Akaongeza kuwa tofauti kubwa ya CCM iliyojivua gamba na Chadema ni uwezo wa uongozi, kuwa Chadema haina uwezo wa kuongoza nchi kwani ina wigo mdogo sana wa viongozi wenye uwezo, na hivyo hakuna tegemeo nje ya CCM...
 
Ni kweli kabisa Sita ni mnafiki babu kubwa. Hapana ubishi kuwa matamshi yake kuna wakati yanaleta changamoto seriklini. Lakini hiyo haiondoi unafiki wake. Anatumia kila oppotunity kujipendekeza kwa wananchi aoneka kuwa yeye si sehemu ya uozo wa serikali ya CCM, tumhurumie. bahati mbaya hata urais wa 2015 utampita mbali sana, na si ajabu asiambulie hata uwaziri.
 
Nampenda sana Samweli Sitta.Sitta mara nyingi huwa hafichi mawazo yake na uchu wa madaraka aliyonayo.Mwaka 2009 kulikuwa na tishio la kumfukuza Sitta uanachama wa CCM.Mara moja nikapenda move hiyo,na nikawaambia CCM kwamba haraka wamfukuze Sitta.Nilikuwa napenda Sitta afukuzwe uanachama wa CCM ili wananchi waone sura halisi ya Samwel Sitta.Na hata alipoenguliwa katika kinyang'anyilo cha Uspika,nilifurahi kwa sababu nilitaka kumwona Sitta mwenye madaraka na Sitta asiye na madaraka.

Lakini kwa kuwa Sitta ni mroho wa madaraka na kupenda kujikweza akashawishiwa kupewa uwaziri,naye akakubali kwa kuwa anajua kuwa bila madaraka hawezi kuwa Sitta wa sasa.Sasa anataka kukwea kileleni,na wala hana break.Amekuwa akitoa kauli mbalimbali ambazo zinaonyesha kuikosoa serikali ya CCM ambayo yeye ni miongoni mwao.Rudisha hisia zako nyuma kumbuka Sitta alivyoendesha suala la Richmond lililopelekea Lowassa kujiuzuru uwaziri mkuu,lakini mwisho wa siku hakuna kilichofanyika.

Sitta alikuwa anaongoza kundi la Mitume Kumi na Mbili wakati huo,ambalo ndilo lililoibuka tena(Sitta,Mwakyembe,Sendeka,Anna Kilango,Lazaro Nyarando,Stella Manyanya n.k) wanataka kutuaminisha kwama wao ni tofauti na wana CCM wengine.Wanataka kutuaminisha kuwa wao wapo kwa ajili ya masilahi ya Watanzania.Kundi hili limeibuka huko Mbeya na kutoa kauli za kuipinga serikali yao na kuwaunga mkono wapinzani,huku hoja kama hizo zinapotolewa na wabunge wa CHADEMA NA NCCR-MAGEUZI zinapingwa.

Kundi hili la mitume ni hatari sana kama wananchi hawatakuwa makini.Wote hao wanaongozwa na uchu wa madaraka,na sasa wanaona kuna nafasi ya kupenyeza mgombea wao katika uchaguzi wa 2015 kwa kuwa Kikwete hatagombea tena.Sitta anajua anachotaka.Wakati wa uchaguzi wa 2005,Sitta alikuwa upande wa mtandao uliomsaidia Kikwete kupata urais.Leo hii wana mtandao hao hawapatani,mulizeni Sitta nini kilichowagombanisha.

Kama Sitta atakuwa Rais au hata Waziri Mkuu ni hatari sana kuliko hata Pinda.Muda aliokaimu uongozi wa Shughuli za Bunge wakati Pinda hayupo,matamshi yake yameonyesha kuwa ni hatari sana,hasa walipowaita wapinzani kuwa ni wanafiki,huku akisahau kuwa Sitta ni mnafiki namba moja katika nchi hii.Matamshi aliyoyatoa jana Mbeya yanatofauti gani na wanayoyatoa wakina Dr.Slaa.CCM ni CCM tu.Sitta na wenzake ni walewale.Kama tutawapa nafasi nchi itavurugika zaidi ya hali ya sasa.
Asante mkuu kwa posti yako.
Nayaunga mkono mawazo yako haya mazuri.
Kwakweli 6 ni mtu hatari sana, ndani na hata nje ya chama chake. CCM wanapaswa kufahamu hilo. Chadema tunapaswa kufahamu hilo zaidi. Mtu anayetaka daima anyamazishwe kwa kupewa vimadaraka hafai. Kama angekuwa na uwezo wa kuona mbali, angeanza kufikiria hata kuuacha ubunge wa Urambo, sio hadi asubiri kuaibishwa kwa kugaragazwa. Akitaka kuona hivyo asubiri, time will tell. Hata Mzee John Malecela alikuwa mtu maarufu ndani ya jamii, na hasa katika jimbo lake la Mtera, ona sasa yuko wapi.
Tazama mifano mizuri ya watu wasiokuwa na uchu wa madaraka na sasa wanaheshima yao katika jamii ya watanzania: michache tu Cleopa Msuya, Frederick Sumaye.
Samweli 6 ni mtu hatari hata kuliko RA alivyodhaniwa. Ona miaka yote aliyotafuta kodi ya wananchi bado anang'ang'ania hata miposho. Maana yake mwananchi aendelee kukamuliwa hadi itoke damu. Ona anavyong'anga'ania kubaki nyumba ya spika, hadi wanataka kuitungia sheria ya kumpa zawadi. Hawa watu pamoja Anna makinda hawana mapenzi kwa nchi hii. Ubinafisi umewatawala, ndo maana wanahalalisha kila jambo linalohusu ulaji wao wakisema ni haki yao. Haki kivipi. Hata kelele zinazopigwa kuhusu umeme wala haiwagusi. Kwani wao wanakatiwa??? Ndo maana basi wametanguliza matumbo yao. Mungu aiepushe nchi yetu na balaa hili.
 
Sitta hana jipya zaidi ya siasa zake za uchwara..Sitta vs Lowassa, Sitta vs CDM..,Sitta vs CCJ tumweleweje huyu jamaa?
 
Ndugu Butola, hoja ya Sitta kuhusu wigo mkubwa wa uongozi, hata TANU mwaka 1961 haikuwa na uwigo mpana wa uongozi ukilinganisha na wakoloni. lakini haikuwa sababu wa Tanganyika kukosa kuchukua nchi. Wigo huo huo walio nao ndiyo umetufikisha hapa tulipo tukiwa hatuna jambo lolote la kujivunia na kusema kwa tufanikwa kufikia malengo. Sana sana tunazidi kurudi nyumba. Tusiangalie key performance indicators za absolute figures bali tuangalie kwa asilimia: umeme vs. mahitaji, elimu vs. mahitaji & ubora, mipango miji vs. mahitaji, n.k. Au tuangalie tu katika maadui watatu ambo serikali ya TANA (CCM) walivitaja mwaka 1961 na tulipo sasa.
 
Ndugu Butola, hoja ya Sitta kuhusu wigo mkubwa wa uongozi, hata TANU mwaka 1961 haikuwa na uwigo mpana wa uongozi ukilinganisha na wakoloni. lakini haikuwa sababu wa Tanganyika kukosa kuchukua nchi. Wigo huo huo walio nao ndiyo umetufikisha hapa tulipo tukiwa hatuna jambo lolote la kujivunia na kusema kwa tufanikwa kufikia malengo. Sana sana tunazidi kurudi nyumba. Tusiangalie key performance indicators za absolute figures bali tuangalie kwa asilimia: umeme vs. mahitaji, elimu vs. mahitaji & ubora, mipango miji vs. mahitaji, n.k. Au tuangalie tu katika maadui watatu ambo serikali ya TANA (CCM) walivitaja mwaka 1961 na tulipo sasa.

Upo sahihi kabisa, lakini mwaka 1961 wananchi Watanganyika walitaka uhuru hivyo hakukuwa na option ya kutawaliwa na Waingereza, lakini mazingira ya sasa na options zilizopo ni tofauti kabisa na za mwaka 1961...

Can you imagine Baraza la Mawaziri kivuli ndio liwe Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?? kweli kama mwananchi mzalendo unaweza ukawa na imani kabisa na Serikali hiyo?hapa ndipo hoja yake inapopata maana...
 
Not so fast...Baada ya kuisikiliza hotuba yake jana, na kuuona mwitikio wa wananchi nimelazimika kufikiri upya....
Mkuu unapenda sana kutumia neno mwitikio lakini naona hulitendei haki kabisa. Ungesema mwitikio wa wana CCM waliosombwa kwa Malory, Mabasi, landcrizer na Bajaji ningekuelewa japo kidogo maana CCM ni wanafiki si unaona walivyomtosa Mpesya
 
Ahsante sana mkuu kwa kutupa nasaba ya 6!! Kumbe ni msukuma wa shinyanga!!! Na mkewe ni mtu wa zambia
 
Sitta alikuwa anaongoza kundi la Mitume Kumi na Mbili wakati huo,ambalo ndilo lililoibuka tena(Sitta,Mwakyembe,Sendeka,Anna Kilango,Lazaro Nyarando,Stella Manyanya n.k) wanataka kutuaminisha kwama wao ni tofauti na wana CCM wengine.Wanataka kutuaminisha kuwa wao wapo kwa ajili ya masilahi ya Watanzania.Kundi hili limeibuka huko Mbeya na kutoa kauli za kuipinga serikali yao na kuwaunga mkono wapinzani,huku hoja kama hizo zinapotolewa na wabunge wa CHADEMA NA NCCR-MAGEUZI zinapingwa.

.

Ni kauli zipi zilizotolewa zinazopingana na serkali na kuunga mkono upinzani???? Tafadhali tujuze mkuu
 
Mkuu unapenda sana kutumia neno mwitikio lakini naona hulitendei haki kabisa. Ungesema mwitikio wa wana CCM waliosombwa kwa Malory, Mabasi, landcrizer na Bajaji ningekuelewa japo kidogo maana CCM ni wanafiki si unaona walivyomtosa Mpesya

Mkuu, hivi magari yale niliyoyaona uwanjani yangeweza kweli kuubeba umati wote ule?please....

kwenye unafiki, niseme tu kimsingi wanasiasa walio wengi ni wanafiki, wanapenda kuongea yale wasiyoweza kuyatenda, hawai wapo CCM na wapo CHADEMA pia, hakuna tofauti kwenye hilo...

Na ndio maana USIMWAMINI SANA MWANASIASA, walio wengi ni fake...., bahati mbaya sie ni binadamu, hatuwezi kujua kiusahihi ni nani aliye fake, kwamba ni Sitta au ni Dr.Slaa, ni Mwakyembe au Mbowe,sijui... lakini nitawapa benefit of doubt wale waliojaribu kupambana na status guo ata pale vitendo vyao vilipokuwa vinahatarisha maslahi yao ya kisiasa..., bado sijaliona hili kwa upande wa Dr.Slaa...
 
mi na shindwa kumu elewa sitta coz ana tembea na miavuli mi wili mmoja wa kui kosoa serikari ambayo ana itumikia na mwingine kui unga mkono selikali so m namu ona kama ki geu geu na mwenye tamaa ya madaraka angalia, mfano juzi juzi wakati ana changia bajate ali mkejeri el juu ya ma a muzi magumu wakati huo huo jana mbeya yupo ki mbele mbele kuisafisha ccm sasa hii ina maana magamba sasa wame kuwa wa safi? au ndio kutafuta u raisi 2015?
 
Ni kweli Sitta na kundi lake linaongozwa na chuki dhidi ya watu fulani kwa kisingizio cha maslahi kwa taifa! llishangaza watu pale mjadala wa richmond ulipozimwa bungeni huku maazimio ya kamati yakiachwa.
duu kumbe ile kamati ilikuwa na lengo la kumuondoa lowasa tu?
 
Lengo la harakati za Sitaa ni kupata urais kwa njia yoyote,ndiiyo maana anawaponda wapinzani wakati kauli zake ni za upinzani.Nafurahi sana kwamba watanzania wengi wananza kuona sura halisi ya Sitta.
 
Back
Top Bottom