Huyo hakupendi na yuko busy na mambo yako. Kama mtu anakupenda kila wakati atataka awasiliane na wewe. Na ukiona kila wakati wewe ndiyo ni lazima uanze mawasiliano ya siku jua pia kuna tatizo ni lazima uanze kulifanyia kazi mapema sana. Kwa dalili ulizosema na kwa uzoefu wangu wa miaka kadhaa ya mahusiano huyu mwanamke ana mtu mwingine ambaye anakupima naye katika mizani na inaelekea mzani unaelemea upande ule wa pili zaidi kuliko kwako. Kwa ushauri mwepesi sana ninaomba tulia anza taratibu kupunguza mawasiliano naye. Ninajua huwa inauma sana ila ni bora maumivu haya kuliko kusubiri maumivu yatakuwa makubwa zaidi baadaye. Tena ninakushauri kama una namba zake za simu hebu zifute katika simu yako ili usiweweseke kumchungulia huko whatsApp, instagram, twitter, n.k. Yaani iwe ni kumjibu tu pale atakaposhtuka kukutafuta. Hebu anza taratibu na ndani ya wiki mbili utaanza kupona maumivu na ikifika mwezi unaanza kupata uponyaji na miezi mitatu unapona unaachana naye.