Nampenda boss wangu aliyeniajiri

Nampenda boss wangu aliyeniajiri

Habari za jioni guys,

Tafadhari naomba mnisaidie katika ili, naomba niseme wazi mimi siyo timbulo.

Miezi mitatu iliyopita nimeajiliwa na kampuni moja hivi hapa mjini, hiyo kampuni ni ya wahindi na huyo dada ndo HR wa hii kampuni. Baada ya kuajiliwa nilimtumia ujumbe (txt) kumshukuru kwa kuona mimi naweza kufanya nao kazi, akanijibu kwa text akinileza ni jambo la kawaida katika maisha kikubwa ni focus kwenye kazi.

Katika mazingira ya kawaida nimejikuta naanza kumpenda kimapenzi na ninahisi hata yeye ananipenda pia, kwanini nasema na yeye ananipenda pia? Kuna siku tulikuwa na event hapa ofini kwetu mialiko ikatolewa kwa watu mbalimbali na nikamwalika rafiki wangu mmoja wa kike siyo mpenzi wangu wakati wa hafla ikiendelea nilikuwa na huyo rafiki yangu muda mwingi akanifata na kuniuliza mbona umemganda sana huyu dada, kuna mfanyakazi mwenzangu wa kike akamjibu ni wifi yetu huyo, akajibu muwe mnasema jamani akaondoka.

Kesho yake ofisini ikawa story kuhusu mimi na huyo wifi yao waliyenipatia.

Siku nyingine ikatokea safari nje ya mjini ya siku mbili tukatoka mimi, yeye na dereva jioni sasa wakati wa kutafuta hoteli ya kulala, bahati mbaya hotel tulipoenda tukakuta nafasi moja tu yeye akaichukua mimi na dereva tukaenda kutafuta mahali pengine tukaagana turudi pale tukishapata ili tukale chakula pamoja tukakubaliana hivyo.

Muda mchache akanipigia simu akakuta simu inatumika naongea na mtu, baada ya kukata akanipigia tena na akaniuliza ulikuwa unamuaga wifi nini? Na siyo mara moja kuniuliza hivyo nikamjibu mimi nipo single akacheka akaniuliza mmepata room nikamwambia yah! Akasema mje basi.

Nisiwachoshe ni mambo mengi sana, naomba mnisaidie ni jinsi gani ya kumfikishia ujumbe kuwa nampenda maana naogopa maana naweza kumweleza hilo jambo likazua mambo mengine mabaya maana natafuta maisha, niliwahi kumwalika chakula cha jioni akaniambia amechoka siku hiyo ana kazi ya ufuaji hivyo haitowezekana kwa siku hiyo

Uwa nachat nae na kumpigia simu nikitaka kuongelea hayo mambo uwa ananirudisha kwenye maswala ya kazi hata kama hamko kazini

Kuna siku nikamtext wasup kuwa kuna zawadi nimekununulia akataka kuijua zawadi nikamwambia no utaijua siku nikikupatia akasema poa!

Na uwa ananiambia anajua kupika sana, nikamuomba apike siku moja anialike akasema atapika siku ya kuzaliwa kwake na atatualika staff nzima nikamuuliza itakuwa lini? Hakuniambia akasema ni suprise, sasa nikawaza niifanye siku hiyo ya kumweleza hisia zangu kwa kumpelekea zawadi itakayokuwa inasema hisia zangu kwake je ni ipi wadau nisaidieni nampenda sana.
Hamna kitu hapo.
Na wewe hamna kitu kichwani kumbe kadashiani by weusi
 
Mkuu piga kazi mapenzi potezea tu hata kama "mbuga inavutia watalii" na yeye anakuelewa potezea kabisa unless kama umepata au huwa unapata kazi kwa urahisi
 
Unakaribia kufukuzwa kazi kijana, subiri siku umfate mkiwa kazini ndio utajua kuna sheria na kazi utaiacha nyuma.

Anaonekana anakupima tu kwa analolijua yeye, shauri zako.
 
Nafikiri kama yumo humu atakuwa kapata ujumbe tayari.
Fanya kazi achana na mambo hayo.
 
Wabongo bwana.. amekubeba mpaka ukapata kazi umegeukia upande mwingine na papuchi nayo wataka? Khaa sio kila msichana akipita mbele yako lazima awe mpnz... !! Kweli mtu mweusi ni budi tutawaliwe tena kama trump anavyosema. Focus na kazi jombaa papuchi zipo nying sana
 
Wabongo bwana.. amekubeba mpaka ukapata kazi umegeukia upande mwingine na papuchi nayo wataka? Khaa sio kila msichana akipita mbele yako lazima awe mpnz... !! Kweli mtu mweusi ni budi tutawaliwe tena kama trump anavyosema. Focus na kazi jombaa papuchi zipo nying sana
Aya mkuu kwa ushauri wako
 
punguza hisia na kamata kazi yako na angalia maisha, ikiwa ni riziki mtajikuta pamoja lakini usitake kulazimisha sana au utaharibu mambo. Kazi ni adimu na mahisiano kazini huwa yana complication zake.
 
punguza hisia na kamata kazi yako na angalia maisha, ikiwa ni riziki mtajikuta pamoja lakini usitake kulazimisha sana au utaharibu mambo. Kazi ni adimu na mahisiano kazini huwa yana complication zake.
Mkuu, ujumbe wako nimeupata vyema, ila nimevumilia sana huu ni mwaka sijawa kwenye mahusiano hiyo hali pia inaweza kuwa inachangia.
 
Ingawa umeshauriwa sana humu lakini ngoja nami nikushauri. Kwanza yaonesha kuwa wewe ni mgeni wa mahusiano ktk mapenzi, usilipinge hilo. Pili bado una akili za kitoto ndo mana mdau mmoja humu ameuliza miaka, hata mimi nilitamani kujua umri ili nikupe dozi kulingana na umri wako. Mwisho sijaona dalili yoyote ya huyo unayehisi kukupenda kwamba anakupenda. Hayo ni mambo ya kawaida sana kazini, piga kazi acha uboya.
 
Piga kazi ndugu yangu. . Huiwaze sana hiyo mambo, kama ipo ipo tu
 
Achana na maisha ya kimovie movie ya kichina, hakuna maisha hapo... tafuta mwanamke mwingine uoe ufanye maisha... hapo hakuna kitu..
 
mwe mwe mwe!dogo acha kabisa huo mchezo,kama kuna wakati unaingizia masuala ya mapenzi yeye anakurudisha kwenye masuala ya kazi jua kwamba,havutiwi kuongea na wewe mambo hayo,cha kukusadia usije ukamwambia chochote kuhs kumpenda,ila tumia sana lugha ya vitendo,bila maneno yoyote yale,mjali mdhamini,msaidie kazi zake,mpe kipaumbele,kuwa nae karibu,ila usije kuonyesha kuwa unamtaka,hlo ni kosa kubwa,mwache yeye akuhisi kwamba unampenda,ipo siku ataanza stori za ajabu ajabu,utajua sasa anaanza kunasa,
 
Back
Top Bottom