Namna ya kumsaidia mtoto kukabiliana na msiba wa mtu anayempenda

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Kuwa muwazi na mueleze kile kilichotokea kwa njia rahisi anayoweza kuelewa. Tumia maneno kama 'amefariki', usifunike kwa kumwambia amelala au namna nyingine yoyote. Mtoto akiuliza maswali yajibu kama unaweza na usimdanganye kwa kutunga hadithi ya uongo.

Kubaliana na hisia za mtoto. Mtoto anapofikwa na msiba anaweza akawa na mwenendo wa tabia ambao haukuitegemea, hivyo ni muhimu uwe umejiandaa. Usikasirike mtoto anapokuwa na hasira juu ya kifo cha mpendwa wake.

Jaribu kurudisha mazingira katika hali yake ya kawaida kwa haraka iwezekanavyo. Hii itategemea nani anaishi na mtoto kwa wakati huo. Mtoto atajisikia kuwa yuko salama kama ratiba haitabadilika hivyo jitahidi kufuata zile ratiba za kila siku.

Zungumza nae kuhusu yule mtu anaempenda aliyefariki. Jaribu kukumbuka nyakati za furaha mlizokuwa nazo ila usimlazimishe mtoto kuzungumza habari hizo kama hataki. Kuwa mvumilivu. Kumbuka maumivu huchukua muda kuisha. Jaribu kumsaidia na hata kujibu maswali hata kama atauliza kwa kuyarudia rudia.

Mruhusu mtoto kutumia kitu chochote cha mtu anayempenda amabaye amefariki zikiwemo nguo au kitu chochote mzazi alichopenda kutumia mara kwa mara. Hii humkumbusha mtoto maisha yao ya pamoja, kusahau majonzi na kurudi katika hali ya kawaida.

Msimulie au msomee hadithi za kwenye vitabu vya dini, au hadithi za wanyama zinazohusu kifo. Hadithi hizi humfanya mtoto aone kuwa kifo ni jambo la kwaida katika maisha na kumfanya awe muwazi kuuliza maswali na hata kusimulia kumbukumbu nzuri alizonazo.


Childline Zanzibar
 
Kuwa muwazi na mueleze kile kilichotokea kwa njia rahisi anayoweza kuelewa. Tumia maneno kama 'amefariki', usifunike kwa kumwambia amelala au namna nyingine yoyote. Mtoto akiuliza maswali yajibu kama unaweza na usimdanganye kwa kutunga hadithi ya uongo.
Nimeipenda hii
 
Back
Top Bottom