Kuishi na Mtoto wa kufikia ni jukumu zito sana

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Habari zenu,

Nimeona uzi wa Mdau akilalamika kuwa Mtoto wa Single Mother anadekezwa sana na Mama yake na akitaka kuchukua hatua Mama mtu anasema anamnyanyasa mwanaye.

Kiukweli suala la kuishi na mtoto wa mtu ni jambo gumu sana maana unahitaji kuwa Boya na Pretender ili uonekane una mapenzi kwa mtoto, ni watu wachache sana wanaoweza kuishi maisha ya namna hiyo.

Kama umezaa na kuna uwezekano wa Mtoto kuishi mbali basi ni vyema mkafanya hivyo kuliko kuleteana maneno kwenye malezi ya mtoto wa nje.

USHAURI
KAMA HAUNA MTOTO NI VYEMA UKATAFUTA MWENZA ASIE NA MTOTO ILI KUEPUSHA MANENO KWENYE MALEZI.

- Single mother tumeanza kushindwana na kutishiana maisha kisa mwanaye
 
Kuna dada analea mtoto wake wa kiume,..aisee yule mtoto namuhurumia sana future yake na bora angekua wa kike,..toto linadekezwa hatari,ana miaka 4 sasa,anavunja vitu vya ndani mama anacheka tu,kila anachotaka mama anampa,siku moja nikampa ushauri kua anamuharibu,akasema mwanangu ni huyu huyu mmoja,..nikamwambie bora uzae wa pili kuliko haya malezo ya huyu mume wa mtu mtarajiwa...Mungu awasaidie wadada wanaolea watoto wakiwa wenyewe.
 
Hatari sana
 
Ukitanguliza upendo inakuwa na wepesi wala huoni kuelemewa wala kung’ang’ana ktk kuishi nae.

Imeandikwa: “ Upendo husitiri wingi wa makosa”

Ukimpenda mtu kwa penzi la kiMungu hutaona
Mabaya wala madhaifu yake bali utakuwa unaona mazuri yake tu na kuchukuliana nae kirahisi.
 
Mnakuza tu mambo!
La hasha. Huo ndo ukweli. Mtoto wa kufikia, kwanza unajua (Huwezi kujitoa ufahamu kwenye hili) kwamba huyo mtoto 100% sio damu yako kabisa. Ndo mana jamaa hapo juu katumia neno la unajipa uBOYA ili mambo yaende.
Halafu cha Pili unajua fika kwamba "hicho unachofanya" na huyo mama mtoto ndicho kilifanyika na mtoto akapatikana. Kwa mantiki hiyo wewe ni sawa na unakula makombo. Je, kilichomfanya huyo mama asiendelee na huyo aliyemzalisha wewe utakiweza/utamudu?
Tatu: Matendo ya "mwanamke mjinga" huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe. Hili hujitokeza sana pale unapomrudi mtoto lakini yeye mama bila kujua nia yako njema, anakimbilia kumlinda mwanaye kwa maneno chokozi eti unamnyanyasa mtoto - yani anakukumbusha points no.1&2 simultaneously na hafikirii nini matokeo
 
Back
Top Bottom