Namna ya kujua Square meters za eneo

Namche Bazar

Senior Member
Apr 8, 2019
105
152
Heshima kwenu wana jamvi.

Kuna jamaa aliniuzia eneo. Baada ya muda kupita bila mimi kwenda kutembelea eneo nahisi atakuwa amebadilisha mipaka ya eneo.

Naomba mtu anayejua jumla ya hivyo vipimo ambayo vipo kwenye mita je ni jumla ni square meters ngapi kwa eneo langu lote.??

Nataka kuthibisha ukubwa wa eneo langu.

Asanteni sana wandugu.
 
Kutokana na vipimo jinsi vilivyo hapo juu, shape ya kiwanja haikupaswa iwe hivyo otherwise ungeweka na angle katika kila change point ndio ingekuwa rahisi kufanya hizo calculation za eneo

Huo mchezo wa kuhamisha beacon upo sana kwa wauzaji viwanja. Case kama hii nilishawahi kukutana nayo, tulienda site na boss akanipatia sketch ya eneo lake. Sasa kwa sababu nilienda na tape, nikamuambia tuhakikishe tena upya ili niwe na uhakika wa vipimo wakati nadesign ramani. Tulivyopima tukakuta kuna mita 1.5 inakosekana kutoka kulia kwenda kushoto, na mita 2 kutoka mbele kwenda nyuma

Nikamshauri ampigie simu mtu aliyemuuzia kiwanja pamoja na huyu jirani yake wa pembeni aje na sketch ya ramani yake ili wajue shida ilipo. Mara nyingi wanaohamisha mipaka ni majirani, kama ni muuzaji ndio kahamisha basi ujue maeneo ya pembeni bado hajayauza.

Mwisho wa siku ikabainika jirani yake ndio alifukua beacon akasogeza pembeni...ukiweka beacon, tumia zile beacon ndefu za futi 3, chimbia yote juu ibaki hata 20cm halafu mwaga zege
 
Mkuu hizi beacon zinauzwa au zinapatikanaje na wapi??
 
Heshima kwenu wana jamvi.

Kuna jamaa aliniuzia eneo. Baada ya muda kupita bila mimi kwenda kutembelea eneo nahisi atakuwa amebadilisha mipaka ya eneo.

Naomba mtu anayejua jumla ya hivyo vipimo ambayo vipo kwenye mita je ni jumla ni square meters ngapi kwa eneo langu lote.??

Nataka kuthibisha ukubwa wa eneo langu.

Asanteni sana wandugu.
Samahani, he hapo juu kuna ramani uliyo ambatanisha na thread yako,mana kwangu naona maelezo tu.

Ukubwa wa eneo hupatikana kwa kutumia za kutafuta maeneo
Mfano
1.Urefu × Upana ,kama eneo ni mstatili na msambamba
2.Upande × Upande ,kama eneo ni mraba
3. ¹/2 × urefu x upana ,kwa pembe tatu.

Sasa pia eneo linaweza kutafuftwa kwa kuhusisha kanuni mbili au tatu.kwasababu siyo kila kiwanja ni mraba,kuna vyengine vina pembe 5.

Kama,umbo la kiwanja lina pembe nyingi.
Nenda na mtaalam site achukue vipimo au/na coordinates za eneo lako,
Aziweke kwenye computer na atakupa jibu.
 
Heshima kwenu wana jamvi.

Kuna jamaa aliniuzia eneo. Baada ya muda kupita bila mimi kwenda kutembelea eneo nahisi atakuwa amebadilisha mipaka ya eneo.

Naomba mtu anayejua jumla ya hivyo vipimo ambayo vipo kwenye mita je ni jumla ni square meters ngapi kwa eneo langu lote.??

Nataka kuthibisha ukubwa wa eneo langu.

Asanteni sana wandugu.
Mlitumia futi au miguu kupima? Mliweka alama zozote?
 
Kutokana na vipimo jinsi vilivyo hapo juu, shape ya kiwanja haikupaswa iwe hivyo otherwise ungeweka na angle katika kila change point ndio ingekuwa rahisi kufanya hizo calculation za eneo

Huo mchezo wa kuhamisha beacon upo sana kwa wauzaji viwanja. Case kama hii nilishawahi kukutana nayo, tulienda site na boss akanipatia sketch ya eneo lake. Sasa kwa sababu nilienda na tape, nikamuambia tuhakikishe tena upya ili niwe na uhakika wa vipimo wakati nadesign ramani. Tulivyopima tukakuta kuna mita 1.5 inakosekana kutoka kulia kwenda kushoto, na mita 2 kutoka mbele kwenda nyuma

Nikamshauri ampigie simu mtu aliyemuuzia kiwanja pamoja na huyu jirani yake wa pembeni aje na sketch ya ramani yake ili wajue shida ilipo. Mara nyingi wanaohamisha mipaka ni majirani, kama ni muuzaji ndio kahamisha basi ujue maeneo ya pembeni bado hajayauza.

Mwisho wa siku ikabainika jirani yake ndio alifukua beacon akasogeza pembeni...ukiweka beacon, tumia zile beacon ndefu za futi 3, chimbia yote juu ibaki hata 20cm halafu mwaga zege
Mtaalam umeona shape yoyote kwani kwenye uzi wake?
Inawezekana kabisa labda natumia browser ya zaman isiyoonyesha picha, lakin mimi naona bandiko tu.
 
Back
Top Bottom