Namna ya kujenga uzalendo kwenye taifa

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,271
12,568
Uzalendo hauhubiriwi bali unajengeka wenyewe kwenye mioyo ya watu. How?

Elimu yetu.
1. Shule za msingi: darasa la kwanza, pili na tatu wanafunzi wajifunze TU kusoma, kuhesabu, kuandika na kuimba nyimbo mbalimbali kuhusu nchi yao ukiwemo wimbo wa taifa. Wajifunze kuichora ramani ya Nchi yao, bendara, wanyama wakubwa na kuyatambua makabila yote ya Nchi hii na mikoa yao. Darasa la nne na tano wafundishwe thamani ya mtanzania, haki za mtanzania, na ubaya wa rushwa, ufisadi, ugaidi, ukataji miti na utunzaji wa mazingira kwa lungha nyepesi kabisa. Darasa la sita na Saba wanafunzi wafundishwe sheria na adhabu za makosa mbalimbali hasa kwa Yale makosa ya kawaida kabisa kama kutukana, kupigana, kuiba, makosa kwenye ndoa, pia wafundishwe kwa kina kuhusu haki za binadamu na tunu za taifa.

2. Elimu ya Sekondari: Kwenye sekondari wanafunzi wa form one wasome Yale TU wanayotaka kuyasoma, yaani mtu asibebeshwe masomo ya Art na sayansi kwa wakati mmoja. Ufaulu kwenye mtihani wa darasa la Saba usaidie kuwapangia form one kwenye michepuo ya sayansi au art subjects. Na wote wafundishwe masomo ya lugha vizuri. Hii inasaidia watoto kuipenda shule na kuanza kuipenda taaluma Yao ijayo.
 
Mtoto aanze darasa la kwanza hajui kusoma na kuandika,? hajui kuhesabu? tunaitaji kizazi cha ku hoji na si cha ndiyo mzee tunatakiwa tuwaandae watoto kwenda na mfumo wa mabadiliko ya tehama, tunaitaji watoto watakaokuja kuanzisha viwanda na kuwa wagunduzi na sio tegemezi kwa kila kitu kutoka nje ya nchi uzalendo bila mikakati ya kimapinduzi katika uchumi tutaendelea kuwa masikini tuu.
 
mtotot aanze darasa la kwanza hajui kusoma na kuandika,? hajui kuhesabu? tunaitaji kizazi cha ku hoji na si cha ndiyo mzee tunatakiwa tuwaandae watoto kwenda na mfumo wa mabadiliko ya tehama, tunaitaji watoto watakaokuja kuanzisha viwanda na kuwa wagunduzi na sio tegemezi kwa kila kitu kutoka nje ya nchi uzalendo bila mikakati ya kimapinduzi katika uchumi tutaendelea kuwa masikini tuu.
Hayo yote hayaji kama hakuna amani, na tunahitaji ICT, viwanda na maendeleo yanayolinda Taifa. Vijana wetu Leo wanaiga TU ya wengine na vyawengine. Wanaambiwa eti uzalendo ni kukubali makato makubwa ya miamala ya simu.
 
Mkuu, Uzalendo haupatikani kwa kufundishwa shule ya Msingi na Sekondari tu.
Ni muhimu sana hata ngazi ya Familia na Jamii nao wabadilike.

Zamani kulikuwa na Unyago na Jando huko watoto walikuwa wanafundishwa miiko, uvumilivu na mambo ya kimaisha na familia kulingana na Kabila husika.

Pia Kulikuwa na Mafunzo ya JKT kiasi kwamba viongozi wote ilikuwa lazima wapitie JKT. Chama cha Mapinduzi nacho kilipata viongozi toka ngazi ya Skauti. Hakukuwa na mambo ya kuunga Juhudi kisha unapewa Cheo.

Kwa sasa kunahitajika mpango mkakati wa muda mrefu na wa kibabe ili kuweza kurudi kwenye uzalendo. Au kuwe na katiba inayomlazimisha kila kiongozi aliyepo Madarakani ni lazima afuate misingi fulani na watu wa kitengo lazima waisimamie, iwe hakuna kuvunja Katiba.

Migawanyiko imekuwa mingi na hatupendani, Tunaishi kwa kuchukiana na uadui kama wa Simba na Yanga - Vyama vingi vinatufanya tusiwe wamoja, Majukwaani tunahubiriwa chuki ili tuwachukie watu wa chama kingine, Hakuna ajira wahitimu wanakosa kazi na kuishia kufanya kazi ambazo hawakuzisomea, Hali ngumu ya maisha inasababisha kuwe na Rushwa, Ndoa kuvunjika, Malezi mabovu, watoto kukosa malezi ya Baba na Mama, Jamii nayo kuwa ya Hovyo.
 
Uzalendo hauhubiriwi bali unajengeka wenyewe kwenye mioyo ya watu. How?

Elimu yetu.
1. Shule za msingi: darasa la kwanza, pili na tatu wanafunzi wajifunze TU kusoma, kuhesabu, kuandika na kuimba nyimbo mbalimbali kuhusu nchi yao ukiwemo wimbo wa taifa. Wajifunze kuichora ramani ya Nchi yao, bendara, wanyama wakubwa na kuyatambua makabila yote ya Nchi hii na mikoa yao. Darasa la nne na tano wafundishwe thamani ya mtanzania, haki za mtanzania, na ubaya wa rushwa, ufisadi, ugaidi, ukataji miti na utunzaji wa mazingira kwa lungha nyepesi kabisa. Darasa la sita na Saba wanafunzi wafundishwe sheria na adhabu za makosa mbalimbali hasa kwa Yale makosa ya kawaida kabisa kama kutukana, kupigana, kuiba, makosa kwenye ndoa, pia wafundishwe kwa kina kuhusu haki za binadamu na tunu za taifa.

2. Elimu ya Sekondari: Kwenye sekondari wanafunzi wa form one wasome Yale TU wanayotaka kuyasoma, yaani mtu asibebeshwe masomo ya Art na sayansi kwa wakati mmoja. Ufaulu kwenye mtihani wa darasa la Saba usaidie kuwapangia form one kwenye michepuo ya sayansi au art subjects. Na wote wafundishwe masomo ya lugha vizuri. Hii inasaidia watoto kuipenda shule na kuanza kuipenda taaluma Yao ijayo.
Ujinga mwingine huu. Mtoto anafikaje darasa la kwanza hajui kusoma na kuandika kizazi hiki? Baby class atakuwa anafanya nini? Umeenda shule enzi za kuzungusha mkono kichwani, usitake kuambukiza kizazi hii matongotongo yako. Hii ni karne ingine kwa mawazo haya ulitakiwa uwe ushakufa kwa uzee, siyo maradhi.
 
Mkuu, Uzalendo haupatikani kwa kufundishwa shule ya Msingi na Sekondari tu.
Ni muhimu sana hata ngazi ya Familia na Jamii nao wabadilike.

Zamani kulikuwa na Unyago na Jando huko watoto walikuwa wanafundishwa miiko na mambo ya kimaisha na familia kulingana na Kabila husika.

Pia kwa viongozi. Kulikuwa na Mafunzo ya JKT kiasi kwamba viongozi wote ilikuwa lazima wapitie JKT. Chama cha Mapinduzi nacho kilipata viongozi toka ngazi ya Skauti. Hakukuwa na mambo ya kuunga Juhudi kisha unapewa Cheo.

Kwa sasa kunahitajika mpango mkakati wa muda mrefu na wa kibabe ili kuweza kurudi kwenye uzalendo. Au kuwe na katiba inayomlazimisha kila kiongozi aliyepo Madarakani ni lazima afuate misingi fulani na watu wa kitengo lazima waisimamie, iwe hakuna kuvunja Katiba.

Migawanyiko imekuwa mingi na hatupendani, Tunaishi kwa kuchukiana na uadui kama wa Simba na Yanga - Vyama vingi vinatufanya tusiwe wamoja, Hali ngumu ya maisha inasababisha kuwe na Rushwa, Ndoa kuvunjika, Malezi mabovu, watoto kukosa malezi ya Baba na Mama, Jamii nayo kuwa ya Hovyo.
Ni kweli mkuu, lakini ukumbuke kuwa hawa wa darasa la kwanza Leo ndio hao watakao wazazi kesho, hivyo mbegu hii itakuwa endelevu, mzazi mzalendo atazaa watoto wazalendo pia. Tatizo letu sio watoto wa siku hizi bali ni wazazi wa siku hizi. Kama mama kavaa nguo fupi Leo na mtoto hatavaa nguo ndefu kesho.
 
Ujinga mwingine huu. Mtoto anafikaje darasa la kwanza hajui kusoma na kuandika kizazi hiki? Baby class atakuwa anafanya nini? Umeenda shule enzi za kuzungusha mkono kichwani, usitake kuambukiza kizazi hii matongotongo yako. Hii ni karne ingine kwa mawazo haya ulitakiwa uwe ushakufa kwa uzee, siyo maradhi.
Leo hii kaka hata wewe hapo huwezi kuimba wimbo wa taifa lako wote kwa ufasaha kwakuwa hakukuwa na wakati wa kutakiwa kila mwanafunzi ajue kuuimba kwa ufasaha wote kwa lazima. Hakukuwa na pahala kila mwanafunzi kutakiwa kuifahamu katiba ya Nchi kwa lazima. Sasa kama mwananchi hajawahi kuiona katiba yake na hajui katiba inasema nini atakuwa na ujasiri gani wa kudai haki zake, au atalindaje kitu asichokifahamu?

Watoto wanakaririshwa Quran na Bibilia nzima lakini sio Katiba yake.

Mtoto wa darasa la kwanza badala ya kufundishwa nyimbo za Tanzania Tanzania, Tazama ramani, na wimbo wa taifa anaambiwa aimbe John John ndiyo papaa, huu ni uhuni katika ujenzi wa uzalendo, samaki mkunje akiwa mbichi kabisa.
 
Ni kweli mkuu, lakini ukumbuke kuwa hawa wa darasa la kwanza Leo ndio hao watakao wazazi kesho, hivyo mbegu hii itakuwa endelevu, mzazi mzalendo atazaa watoto wazalendo pia. Tatizo letu sio watoto wa siku hizi bali ni wazazi wa siku hizi. Kama mama kavaa nguo fupi Leo na mtoto hatavaa nguo ndefu kesho.
Mtoto wa Nyoka nae lazima awe Nyoka. Matendo mengi tunayofanya wazazi hujirudia kwa watoto wetu. Zile familia zenye maadili mema pia watoto wao wanakuwa hivyo. Kama Baba aliwahi kufunga Ndoa, utakuta na mtoto nae anatamani kuja kufunga Ndoa. Kama Mama alikuwa mcharuko na watoto wanakuwa zaidi yake.

Ngazi ya Familia inajukumu kubwa la kuandaa maadili mema ya Jamii husika.
Watoto wengine muda mwingi wanakuwa wanaishi Boarging school tangu Nursery na malezi wanayopata ni yale ya Matron na Madam. Hakuna mambo ya uzalendo kule ni kukaririshwa masomo tu ili shule ipate matokeo ya ufaulu mzuri tu.
 
Mtoto wa Nyoka nae lazima awe Nyoka. Matendo mengi tunayofanya wazazi hujirudia kwa watoto wetu. Zile familia zenye maadili mema pia watoto wao wanakuwa hivyo. Kama Baba aliwahi kufunga Ndoa, utakuta na mtoto nae anatamani kuja kufunga Ndoa. Kama Mama alikuwa mcharuko na watoto wanakuwa zaidi yake.

Watoto wengine muda mwingi wanakuwa wanaishi Boarging school tangu Nursery na malezi wanayopata ni yale ya Matron na Madam.

Ngazi ya Familia inajukumu kubwa la kuandaa maadili mema ya Jamii husika.
Taifa lazima liandae wazazi bora, maandalizi ya wazazi bora yanaazia utotoni alivyozaliwa, lishe Bora, chanjo, elimu sahihi, malezi bora, siasa safi, demokrasia safi, mahakama zinazotenda haki, uadilifu wa viongozi, nk.

Viongozi wa siasa hawezi kuwa wezi halafu wananchi wawe wazalendo, hiyo haitawezekana
 
Hayo yote hayaji kama hakuna amani, na tunahitaji ICT, viwanda na maendeleo yanayolinda Taifa. Vijana wetu Leo wanaiga TU ya wengine na vyawengine. Wanaambiwa eti uzalendo ni kukubali makato makubwa ya miamala
mbona amani tunayo na wazalendo wapo sema wanapigwa vita sana. mifano michache prof Asad, general Ulimwengu, n.k unasema vijana wetu wanaiga mimi na wewe na wengine wa umri wako tumefanya nini ambacho tunajivunia na hawa vijana tunaweza kuwaambia watuzidi sisis wasiige vya wengine, swala la miamala linaguza rika zote na halijabagua kijana mzee wala mtu mzima na katika makundi umri sijaona kundi linaloweza kujivunia kupiga au lilipinga maswala ya miamala na likabezwa na kundi lingine.
 
..HAKI itendeke kwa kila Mtanzania.

..tuhakikishe kuna FURSA sawa kwa Watz kufikia ndoto zao.

..HAKI na FURSA vitawafanya raia wetu wawe na mapenzi ya dhati na nchi yao, kitu ambacho tunaita UZALENDO.

..Mtanzania anapaswa kuamini kwamba hapa ndio mahali penye haki, usalama, na fursa, kuliko mahali kwingine popote.
 
Mkuu, Uzalendo haupatikani kwa kufundishwa shule ya Msingi na Sekondari tu.
Ni muhimu sana hata ngazi ya Familia na Jamii nao wabadilike.

Zamani kulikuwa na Unyago na Jando huko watoto walikuwa wanafundishwa miiko, uvumilivu na mambo ya kimaisha na familia kulingana na Kabila husika.

Pia Kulikuwa na Mafunzo ya JKT kiasi kwamba viongozi wote ilikuwa lazima wapitie JKT. Chama cha Mapinduzi nacho kilipata viongozi toka ngazi ya Skauti. Hakukuwa na mambo ya kuunga Juhudi kisha unapewa Cheo.

Kwa sasa kunahitajika mpango mkakati wa muda mrefu na wa kibabe ili kuweza kurudi kwenye uzalendo. Au kuwe na katiba inayomlazimisha kila kiongozi aliyepo Madarakani ni lazima afuate misingi fulani na watu wa kitengo lazima waisimamie, iwe hakuna kuvunja Katiba.

Migawanyiko imekuwa mingi na hatupendani, Tunaishi kwa kuchukiana na uadui kama wa Simba na Yanga - Vyama vingi vinatufanya tusiwe wamoja, Majukwaani tunahubiriwa chuki ili tuwachukie watu wa chama kingine, Hakuna ajira wahitimu wanakosa kazi na kuishia kufanya kazi ambazo hawakuzisomea, Hali ngumu ya maisha inasababisha kuwe na Rushwa, Ndoa kuvunjika, Malezi mabovu, watoto kukosa malezi ya Baba na Mama, Jamii nayo kuwa ya Hovyo.
Uzalendo + Njaa = 0
 
Uzalendo + Njaa = 0
Hujasia habari za maskini jeuri na kufa na tai shingoni?

Uzalendo sio kama kanzu ambayo unaweza kuivua wakati wowote bali uzalendo ni Ile hali inayomfanya mtu asihame kabila, ukoo, wazazi au timu yake ya mpira inayooshabikia.

Uwahazabe watabaki kuwa wahazabe hata mkisema nini. Hata hivyo uzalendo ni tunda la haki, yaani kama baba kila siku anakula pilau na kuwaacha watoto wale ugali na mlenda mbele yake watoto watakisa uzalendo kwa baba Yao huo. Kama kiongozi anaogelea kwenye utajiri wakati wafuasi wake wako taabani kwa njaa, kiu, Giza nk, usitarajie uzalendo kuwepo pahala hapo.
 
Uzalendo ni attitude ya mtu kuhusu taifa lake. Kufundisha attitude ni kazi ngumu sana. Siku zote na mara zote watu wanajifunza wenyewe attitude kwa kuiga na kuangalia watu wengine (role model) kuhusu jambo hilo. Kama mzazi, peers, jirani, kiongozi sio mzalendo ni ngumu kijana pia kuwa mzalendo. Kama ataona polisi wanarusha mabomu ya machozi kutawanya watu wasiotenda kosa kwa mujibu wa sheria na Katiba uzalendo haujengeki,
 
Back
Top Bottom