Namna ya kudhibiti Nguruwe Pori kwa uharibifu shamba la Mihogo

Wadau,

Kama mada husika hapo nina shamba kubwa la mihogo changamoto kubwa niliyonayo ni nguruwe usiku wanafanya uharibufu.

Naomba mawazo na maarifa ya kuwadhibiti

Ahsanteni
Tafuta mafuta ya simba mkuu pakaza vitambaa vifunge maeneo mbalimbali randomly shambani hasa pembezoni, hutaona nguruwe wala nyani shamnani kwako unless uvitoe hivyo vitambaa.
Wanamuogopa simba sn, watafungia break chalinze, it works but mtihani ni wapi utapata hilo wese la mfalme wa pori
 
Hii mbinu inaweza kumfanya aone fursa kwa kuuwa ndege wawili kwa jiwe moja.

Biashara ya mihogo na kitimoto.
Walaji huku sio wengi ilaha wameanza kuongezeka kuna jirani Yangu alikaa muda mrefu sana bila Kula nyama, usiku akawa anaota anakula nyama kumbe akawa anatafuna godoro
 
Nashukuru kwa mtizamo wako.Nafikiri kuchanganya Miti ya mbao na ya matunda mfano parachichi ILI niwe nafaidi kidogo kidogo kabla ya kuvuna mbao. Nahitaji kukosolewa
Hapo sawa na michungwa, miembe, mipapai n.k. ila hao ngedere hutakuwa umewakimbia
 
Hapo sawa na michungwa, miembe, mipapai n.k. ila hao ngedere hutakuwa umewakimbia
Umesema ukweli ILA katika miaka 4 ijayo kutakuwa tayari na watu wengi wamehamia eneo hilo hivyo hao wanyama nao watakimbia nami nitakuwa nimeanza kuvuna kuliko kuicha ardhi ikae bure kwa kuogopa wanyama pori.
 
Mkuu kama bado unahitaji njia rahisi ya kuzuia Nguruwe ni kuchimba Msingi wa upana kama Futi moja kwenye upande ule wanaoingilia au kuzunguka Shamba hapo hawawezi kupita tena coz Miguu yao ya mbele ni mifupi na hawawezi kuikunja hivyo utamkuta asubuh akihangaika hapo. Aidha kwa Nyani ni kuripua baruti iwe kwenye Gobole etc hapo hawawezi kurudi tena mana wanaogopa Bunduki sana.., ikishindikana nunua redio halafu uwe unaiwasha muda wao ule wanaokuja, iwashe sauti ya juu basi watajuwa mwenyewe yupo hivyo hawata ingia shambani.
Nb:
Hii ya Redio inabidi ujiridhishe na aina ya Nyani unayodeal nao kama ni wa Porini haswa itafanikiwa, ila wakiwa hawa wanaokula Mikate kama huyo kwenye avator yangu, ndugu yangu utawakuta wamemaliza Shamba lote huku wamebadili na stesheni wameweka Bongofleva wanaserebuka kwa furaha!!!
na radio wataibeba
 
Utajiri huo ndugu, tafuta kibali maliasili uweke mitego ukamate uuze nyama. Hiyo mboga ni tamu kuku atasubiri mno...
Yani hadi nimekuonea wivu, aliyesema kwenye miti hakuna wajenzi hakukosea
nimewala sana urambo vijijini aisee, uzuri wa huyu mnyama hana mafuta kama wale wa kufugwa,
 
Mkuu dog atafurukuta mbele ya hao u must be kidding
Mkuu huyo Mbwa Zengwe la Nyani tu linamtosha., huwa kuna Nyani wanatembeaga wawili hawa wanatabia ya kumrubuni Mbwa ili awafate, wakishamsogeza kwenye Kipori kidogo wanamkamata then wanamkata Makofi ya haja, huo ukunga atakaopiga hapo akiachiliwa ni mbio plus kujikojolea hadi home!
 
Nashukuru mkuu manake shughuuli ya nyani c mchezo wanafanya reasoning kubwa kumrubuni mbwa
 
Nashukuru mkuu manake shughuuli ya nyani c mchezo wanafanya reasoning kubwa kumrubuni mbwa
Ni kweli Mkuu., Nyani ni miongoni mwa Wanyama wanaotumia Ubongo vizuri kufanya matukio.., nje ya Mada, Hivi Mgunga si ule wenye miba?
 
Ndio huo mkuu tena unapatikana zaidi sehem zenye asili ya ukame
Ni kweli Mkuu naukumbuka sana, kuna Jamaa enzi hizo Kijijini tumekwenda kuwinda, Jamaa akachepuka kidogo kujisaidia hamadi Mbwa Mwitu wakamtoa mbio basi huwezi amini huo Mti aliupanda akiwa uchi hadi kileleni tena ndani ya Sekunde, cha ajabu baada ya wale Mbwa kupotea ameshindwa kushuka mwenyewe eti ule Mti una miba!!!
 
Ndio hvyoo uhai kwanza mengine baadae mkuu
 
Hello..... Karibuni Sana Katika group linalohusu ufugaji wa nguruwe

Karibu Sana wewe mtaalamu wa mifugo, mfugaji, mnunuzi, pamoja na Wale wenye kiu ya kujifunza zaidi kuhusu ufugaji huu wenye tija na kipato cha uhakika.....

Click link ifuatayo kujiunga......

Zingatia kujitambulisha pindi tu uingiapo katika group hili
ZINGATIA KUJITAMBULISHA PINDI TU UINGIAPO KATIKA GROUP HILI... JINA, MKOA, SHUGHULI

TSA- PIG FARMING
 
Back
Top Bottom