Namna ya kudhibiti Nguruwe Pori kwa uharibifu shamba la Mihogo

pamoja na njia zilizoshauriwa hapo juu, vile vile wakati unapanda basi unaweza kuzungushia pembeni kama mistari minne ya mihogo michungu, wakiingia wakaonja wakakuta ni michungu wanadhani shamba zima liko hivyo hawafanyi uharibufu mkubwa... lakini pia ni vizuri ukapanda sehemu ambayo kuna mashamba mengine ya mihogo..ukikuta umepanda mwenyewe lazma uumie
 
95cede877d4b66d71bf0afc8155c2dc4.jpg
0e0a7778db7ca0598b893d77c4ba1bbc.jpg
d8a6069baf7677ca1595fbf3e48b3b0d.jpg
1fdd5ceb3b0c0f6525240eaa490ca776.jpg
 
Utajiri huo ndugu, tafuta kibali maliasili uweke mitego ukamate uuze nyama. Hiyo mboga ni tamu kuku atasubiri mno...
Yani hadi nimekuonea wivu, aliyesema kwenye miti hakuna wajenzi hakukosea
 
Kisarawe hawa wadudu walinifanya nichukie kilimo cha mihogo..... Mchana nyani wanavunja mashina YA mihogo usiku nguruwe wanachimba mihogo... Yaaani we Acha tu nyani kumi ndani y lisaa wanaweza kuvunja mihogo kwenye shmba la heka Tano likawa kama uwanja wa mpira..... Kuna jiran yangu nyani walivuba maembe jamaa akawa anasema anaenda kuwaloga
Ha ha ha anawarogaje sasa umenichekesha mkuu
 
Wadau,

Kama mada husika hapo nina shamba kubwa la mihogo changamoto kubwa niliyonayo ni nguruwe usiku wanafanya uharibufu.

Naomba mawazo na maarifa ya kuwadhibiti

Ahsanteni
Aisee kuna post moja nimeifumania. Jamaa amesema aliwadhiti hao wadudu kwa kuweka taa kadhaa (katika kila pande) shambani. Kwakuwa wale jamaa hawafanyi shughuli zao mchana/kwenye mwanga, kwahiyo ukiweka taa hawatafanya yao.
 
Hiyo avatar yako na hayo maneno uliyoyaandika kwenye bold yanatia shaka na ukakasi.
Allah hawezi kunihukumu kwa Kula nyama labda kama sikumshukuru kwa neema hiyo aliyo kuruzukia waja wake! Labda Mwenzangu mjuzi niwekee ushahidi ilipopigwa ban..
 
Allah hawezi kunihukumu kwa Kula nyama labda kama sikumshukuru kwa neema hiyo aliyo kuruzukia waja wake! Labda Mwenzangu mjuzi niwekee ushahidi ilipopigwa ban..

إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةَ وَالدَّمَ وَلَحْمَ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ بِهِ لِغَيْرِ اللّهِ فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلاَ عَادٍ فَلا إِثْمَ عَلَيْهِ إِنَّ اللّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

Yeye amekuharimishieni mzoga tu na damu na nyama ya nguruwe na kilicho tajiwa, katika kuchinjwa kwake, jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu. Lakini aliye fikiwa na dharura bila ya kutamani wala kupita kiasi, yeye hana dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
 
Wee mbona unachekesha unaelewa dharula bro? sasa ikikufika uteme au ule? mbona hujaambiwa ukishikwa na dharula uikurubie zina? Na ukila kupitia kiasi wee ni mlafi...Kula tu bro chaumbile Imulungu ni cha kumemena
 
Mkuu kama bado unahitaji njia rahisi ya kuzuia Nguruwe ni kuchimba Msingi wa upana kama Futi moja kwenye upande ule wanaoingilia au kuzunguka Shamba hapo hawawezi kupita tena coz Miguu yao ya mbele ni mifupi na hawawezi kuikunja hivyo utamkuta asubuh akihangaika hapo. Aidha kwa Nyani ni kuripua baruti iwe kwenye Gobole etc hapo hawawezi kurudi tena mana wanaogopa Bunduki sana.., ikishindikana nunua redio halafu uwe unaiwasha muda wao ule wanaokuja, iwashe sauti ya juu basi watajuwa mwenyewe yupo hivyo hawata ingia shambani.
Nb:
Hii ya Redio inabidi ujiridhishe na aina ya Nyani unayodeal nao kama ni wa Porini haswa itafanikiwa, ila wakiwa hawa wanaokula Mikate kama huyo kwenye avator yangu, ndugu yangu utawakuta wamemaliza Shamba lote huku wamebadili na stesheni wameweka Bongofleva wanaserebuka kwa furaha!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom