Namna ya kuchangia faini ya Tsh. Milioni 350 waliyohukumiwa kulipa Viongozi wa CHADEMA

Hujalazimishwa kutoa

I know. Ila sio kwa kutuchutama huko kwa diaspora aka wapiga box kwenye baridi kali with no life.

Kwa kujua umuhimu wao mkiinue kilio chao cha uraia pacha kwenye sera zenu kama wao watavyowanyanyua kwenye michango ya kuwatoa viongozi jela.
 
Kama mtakumbuka ni kwamba mnamo tarehe 10/3/2020, viongozi wa waandamizi walihukumiwa kwenda Gerezani kwa muda wa miezi mitano au kulipa faini kwa ujumla wake shilingi 350,000,000.00.

Ninachotaka kuongelea ni utozwaji wa faini batili ambao unafanywa kati ya mahakama na jeshi la magereza.

Adhabu yao ilikua ni aidha kulipa faini au kwenda jela miezi mitano.

Kwa uelewa wangu kama kumbukumbu ziko sawa ni kwamba watuhumiwa wote walikwenda jela tangu siku ya kwanza na kuanza kutoka siku yapili na wengine siku ya tatu na wengine bado wako gerezani.

Kwa msingi huo basi,wafungwa hao tayari watakua wametumikia sehemu ya adhabu yao kwa kuwepo gerezani kwa siku zaidi ya moja na kuendelea.

Ilikua ni matarajio yangu kwamba viwango vya faini vilitakiwa kupungua kwa kutegemea siku ambazo muhusika alikua ametumikia sehemu ya adhabu.

Kuendelea kuwatoza kiwango kilekile cha faini kana kwamba wafungwa hao walikua uraiani sio sahihi. Na mara zote wanaotakiwa kupiga hesabu hizi ni Jeshi la Magereza na sio mahakama.

Lakini kingine kilichonishangaza katika zoezi hili ni lile la msigwa kulipiwa faini mara mbili. Ina maana mahakama zetu haziweki kumbukumbu zake vizuri?

Mwenye uelewa zaidi tafadhali
 
Kama DPP mwenyewe anakuja mbele ya kamera na vitisho na mikwara mingi unategemea bado tuna mahakama huru.

Mahakama zinaendeshwa kwa maagizo maalumu anzia ofisi ya DPP mpaka mahakamani.

Ni aibu sana kwa msemaji wa Ikulu kushadadia faini ya Msigwa angalia Mwenezi wa CCM Pole pole alivyo poteza uelekeo mpaka Segerea anaonekana anavyoshadadia mambo unafikiri hii ni tafsiri nzuri.
 
Mh.. Sipo kwenye siasa..ila nadhani kati ya kifungo na faini wao walichagua faini... ina maana wangelipa faini ata mda ule ule wangetoka ..ila kwakuwa walikuwa hawana pesa kwa haraka ndio maana waliendelea kubaki adi pale pesa itakapotolewa

Elimu yangu ni form four
 
Ccm inaogopa kuruhusu uraia wa nchi mbili sababu inawaogopa diaspora watawaamsha watz waliolala,kumbuka kazi ya moshi wa mwenge ni kuwaroga watz wasizinduke sasa diaspora hawapitiwi na ule moshi akili zao ziko fresh.
 
Kama DPP mwenyewe anakuja mbele ya kamera na vitisho na mikwara mingi unategemea bado tuna mahakama huru.

Mahakama zinaendeshwa kwa maagizo maalumu anzia ofisi ya DPP mpaka mahakamani.

Ni aibu sana kwa msemaji wa Ikulu kushadadia faini ya Msigwa angalia Mwenezi wa CCM Pole pole alivyo poteza uelekeo mpaka Segerea anaonekana anavyoshadadia mambo unafikiri hii ni tafsiri nzuri.
Mkuu, ukiamua kufanya kazi na shetani ndio matokeo yake unajikuta unafanya mambo ya kijinga na ya aibu tupu! Angalia wamechukua magari ya serikali kwenda nayo segerea na kubeba watu wao na wamerudi kwa aibu kuu! hao ndio ccm walioamua kufanya kazi na shetani badala ya Mungu.
 
We’ve got great news for you: Lazaro Nyalandu has received your money to their Mobile money account!

Here are the full details again for your records:

Your WorldRemit transaction number: 57171301
You sent: GBP 10.99 to Tanzania
Lazaro received: TZS 28226.00
Mobile money provider: Vodacom M-PESA mobile money account
Mobile money account number: 757929469

Thank you for using our service!



Until next time,
WorldRemit Customer Service
 
Unaniangusha bhn Pound 10 tuu?
We’ve got great news for you: Lazaro Nyalandu has received your money to their Mobile money account!

Here are the full details again for your records:

Your WorldRemit transaction number: 57171301
You sent: GBP 10.99 to Tanzania
Lazaro received: TZS 28226.00
Mobile money provider: Vodacom M-PESA mobile money account
Mobile money account number: 757929469

Thank you for using our service!



Until next time,
WorldRemit Customer Service

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba viongozi wa CHADEMA Taifa watoe Account Namba tusaidiane kuchangia hii Hukumu. Asante

=======

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo jioni makamu mwenyekiti wa Chadema (Zanzibar), Said Issa Mohammed amesema hukumu hiyo ni dhuluma ya demokrasia na wapo tayari kukata rufaa na watanunua haki yao.

"Mtakumbuka tangu 2018 kulikuwa na kesi ya kubambikia viongozi wetu. Baada ya ushahidi tulikwenda mahakamani tukijua tutashinda," amesema Mohammed.

Amesema Chadema wataendelea na mapambano na kwamba hadi leo saa 6 usiku wanataka wawe wamepata fedha hizo.

"Hukumu imetolewa saa 10 wakijua benki zote zimefungwa viongozi wetu wabaki. Ikifika kesho twende tukawatoe viongozi wetu. Tunao mawakili tutakata rufaa. Tutahakikisha tunafikia lengo saa 6 usiku," amesema.

Amewataka wanachama wao kutumia akaunti ya CRDB yenye jina la Chadema M4C 01J1080100600 na namba za mkurugenzi wa fedha, Rodrick Lutembeka 0754275531 na 0655 275 531 kufanikisha mchango huo.

Akihamasisha michango hiyo, Mwenyekiti wa Kanda ya Kati, Lazaro Nyalandu amesema hukumu hiyo ilikuwa ni jaribio la kidemokrasia ambalo wamelishinda.

"Nasimama hapa kwa sababu mwenyekiti wetu hatalala kwake, viongozi wetu hawatalala kwao kwa kupigania haki.

Tutasonga mbele, kufikia kesho saa 2 asubuhi tuwe tumefanikiwa," amesema Nyalandu.

Amewaomba Watanzania wa vyama vyote na wapenda demokrasia kuchangia faini hiyo.

"Wale ambao wamefurahi kwa kuumizwa kwa kina Mbowe na watakwenda kunywa soda na bia wajue tutashinda."

Naibu Katibu mkuu (Bara), Benson Kigaila amesema michango hiyo ina lengo la kuonyesha Serikali mshikamano wao.

"Tuwaonyeshe Serikali waliowaweka viongozi wetu ndani. Tuwaonyeshe, tukalipe hiyo hela, tuchange kila hela. Tunao wanachama milioni saba Kaskazini, Kusini, Kati na Magharibi na Mashariki tuchange. Kesho kabla ya misa ya kwanza wawe wametoka," amesema Kigaila.

Chanzo: Mwananchi


Pia, soma:

Breaking News: - Mahakama ya Kisutu imewatia hatiani Viongozi wa CHADEMA na kuwahukumu kulipa faini Milioni 350 au kwenda jela miezi 5 kwa kila kosa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mm siwez changa ata shiling sababu nikifanya ivyo ntakuwa nawavimbisha kichwa wanaowabambikizia na wao pia sababu kuna makosa mengine wanafanya makusud au kwa bahati mbaya nia kujionhezea umaarufu au wanajua watachangiwa tu mm nahofia mawili moja hizo pesa kutua mikonon mwa wale jamaa nadhan mnawajua ambao watanogewa na kuwaona kumbe chadema ni dili
Km ni kuandamana nchi nzima kupinga io hukumu kwa maandamo halali mm ntaungana nanyi sawa ila pesa sitoi
 
Back
Top Bottom