Namna ya kuchangia faini ya Tsh. Milioni 350 waliyohukumiwa kulipa Viongozi wa CHADEMA

Igweeeee, niende kwenye mada moja kwa moja. Kufuatia kuongezeka kwa kesi za kisiasa nchini kuwakumba wapigania haki mbalimbali ikiwemo haki ya kutoa maoni, kama kesi inayomkabili M.Melo, wafanyakazi wa kituo cha kutetea haki za binadamu pamoja na kesi iliyokuwa ikiwakabili viongozi wa Chadema, kesi ya Zitto nk.

Napendekeza tufungue akaunti maalumu ambayo tutakuwa tunatuma pesa kidogo kidogo ili zisaidie uendeshaji wa kesi pamoja na faini mbalimbali, tukumbuke demokrasia ni gharama.

Karibuni kwa maoni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wote tunajua makosa yaliyowatia hatiani viongozi wa Chadema yalitendeka wakati wakitimiza majukumu ya chama.

Kazi ya ruzuku ni kusaidia kuvipa uwezo vyama vya siasa viweze kukua.

Endapo viongozi 8 wa Chadema watafungwa jela chama " kitasinyaa na kudumaa" na kwa kuwa lengo la ruzuku ni kukiwezesha Chadema kukua, nashauri ruzuku itumike kulipa faini ya mahakama kama sheria inaruhusu.

Maendeleo hayana vyama!
 
Naunga mkono hili, toeni namba tuanze harambee waone NGUVU YA UMMA ILIVYO KUBWA! Ila kuwepo na utaratibu maalumu ili wasitugundue!
 
Back
Top Bottom