safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,170
- 15,851
Wakuu naomba kufupisha historia yangu ya kuanzisha biashara nilipokuwa kwenye kibarua fulani nina imani hata wewe itakusaidia sana pengine kama sio wewe ni mwingine.
Miaka kadhaa nyuma nilipokuwa nimepata kibarua fulani nilikuwa nimekaa mda mrefu nikiwaza biashara kichwani ila nilikuwa naogopa sana kuanza kwa kuhofia kufeli aisee.
Nimekaa kama miaka mitatu hivi nawaza tu nina mshahara sina kitu kingine cha kuniingizia pesa,basi mpaka nikaoa iko hivyo,siku moja nikajitoa ufahamu tu nikasema acha niingie tu.
Nikaanza utafiti wa kujua bidhaa ninayoitaka kwa maeneo yangu inauzwaje,je ni kama yangu? Nipunguzaje ili niwavute wateja kwangu?
Baada ya kutafiti nikajua kuwa nataakiwa nipunguze bei kidogo ili niwavute,basi nikaanza.
Nakumbuka nikaenda ilala kuchukua tisheti za mtumba kwa mdau mmoja hivi kwa bei ya jumla ya tsh 3,000 tishert kali quality nilichukua kama 20 hivi ikawa kama jumla tsh 60,000.
Basi nikasafirisha mpaka sehemu nilipo,nikatafuta sehemu ya jamaa flani alikuwa anauza kanzu na vitu vingine,nikaongea nae nikaweka tshirt zangu 20. Jamaa akaniambia kwa kuwa ndo unaanza we angalia upepo then utaangalia unanipozaje kibanda hiki.nikamwambia ok.
Ile sehemu ilikuwa ni barabarani kwa pembeni kidogo,watu wanapita wanaona biashara, nikasema tishert watu wanavaa acha nijiripue tu.
Nilipoziweka zile tshirt siku ya kwanza niliuza 8 @ 7000 = 56000.
Siku ya pili nikauza 6 @ 7000 = 42000.
Siku ya tatu nikauza tena 6 @ 7000 = 42000.
Jumla kwa siku tatu nikapata 140000 ukitoa na pesa ya mtaji 60000 basi ikabaki 80000 nzima ni mtaji.nikasema aisee kumbe mambo yako hivi.
Nikaenda tena kuchukua mzigo pisi kama 30 hivi kwa uoga uoga @ tsh 3000 ambazo ikawa jumla 90000.
Kumbuka kuwa nilikuwa nachukua kwa mdau ambaye yeye ni mzoefu kwa hiyo nikawa nachaguliwa zile tsheti zenye ubora kidogo nikaona sio kesi tupate wote.
Safari hii niliuza mzigo huu kwa siku 7. Nikaounguza bei kidogo ili watenga wawe wengi na pesa izunguke sana kwa sababu kuwa na buku inayozunguka kwenye biashara kwa mwezi mmoja ikazalisha ni bora kuliko kuwa na alfu kumi mfukoni isiyozalisha.
Basi kwa siku saba nikauza mzigo wa pisi 30,pisi 10 @ kwa 6000 na pisi 20 @ 7000. Nikapata jumla 200,000.
Sasa hapo nikatoa na tsh 90,000 nikapata faida 110,000.
Hapo nikaanza kuwa sirias rasmi katika biashara,nikagundua kuwa biashara inataka utafiti na sehemu husika rafiki then mtegemee Mungu tu mambo yataenda.
Sitaki kuweka hesabu za nauli na chakula hapo na mavazi kwa sababu hayo yote nilikuwa nayafanya na nayapata kabla ya hii biashara kwa hiyo siwezi kutoa pesa ya kwenye biashara wakati hata kabla ya hii biashara pesa hiyo ilikuepo,sitaki kuitia mzigo biashara ikiwa bado ni changa.
Formuila yangu ni kuwa Biashara changa inakutegemea wewe,biashara iliyokomaa wwwe ndo unaitegemea.
Hii biashara ni changa kwa hiyo mimi ndo natakiwa niiiramishe kwa kuiwekeza zaidi,lakini sasa nikisema niitegemee hii biashara kuniimarisha mimi kwa wakati huu nitafeli.
Ikishakomaa sasa ntaanza kuagana rasmi na mshahara na kuuweka saving wote huku pesa yote ya malazi ikitoka kwenye biashara wakati huo imeshakomaa.
Biashara changa ni kama mtu anayeanza maisha,asibebeshwe majukumu mengi ataporomoka na kuishia patupu asione wapi anaelekea.
Kwa wale wanaoamini kuwa biashara ni lazima uwe umesoma sana masomo ya biashara darasani na ukaenda chuoni ukafuzu kwq ma GPA makubwa makubwa basi nawaambia tu kuwa wanachokisoma kilianza kufanywa kwanza kwa vitendo.
Kabla ya kuwepo masomo ya biashara basi vilianza vvitendo vya hiyo biashara yenyewe,watu walianza kufanya biashara mtaani wakaona hali zinavyokwenda wakaona elimu hiyo waihamishie kwenye makaratasi,so asili ya mambo ni vitendo hapo,makaratasi huja baadae kwa ajili ya kuhifadhi ujuzi usipotee.
Hata fani ya upasuaji ili uusome upasuaji lazima iwe kuna mtu aliufanya kwa vitendo kisha aliyoyaona ndo akayaandika sasa ili wengine wasiokuwepo na wengi wapate elimu.
Kwa hiyo kumbuka kuwa mafanikio katuka biashara ni kuifanya na sio kuisoma tu bila kuifanya,ubapozidi kufanya utasoma mengi zaidi kwa mujibu wa mazingira yalivyo.