Ila biashara bwana

Mmea Jr

JF-Expert Member
May 20, 2016
551
1,222
Okay habari zenu wakuu ??. Natumaini wote mnafurahia kuuona mwaka 2024 . Na wale tunaokimbiza na ada tusijali wakuu tutatoboa tu .

Sawa tusipoteze muda leo ngoja niwapeni kisa fulani ambacho nimewahi kukutana nacho hapo nyuma katika mambo ya biashara .
Mkoa ninaoishi ni miongoni mwa mikoa yenye wafugaji wazuri sana wa mbuzi katoliki( nguruwe ) na walaji wakutosha . Sasa bwana katika kujitafuta mwenzenu nikaona ngoja nijaribu hii biashara ya kuuza mbuzi katoriki maana jamaa yangu fulani yeye alikuwa kafungua gori pande za katikakati ya mji na aliniambia hii biashara inalipa sana plus kunifundisha mbinu mbali mbali za kuibia wateja ilimradi tu mwisho wa siku itokee faida . Huyu jamaa huamini kwenye biashara yeyeto ile ukiona faida inakuja tu basi ujue kuna sehemu unakosea yeye usema " siku zote faida inabidi itafutwe faida haiji yenyewe "

Basi bwana nikatafuta sehemu na mimi nikajenga banda langu nunua ndizi mzuzu , katakata kachumbari , agiza nyama ya mbuzi katoliki (nilianza na kilo 7 ) . Mafuta ya kupikia lita 3 plus kabati fulani kubwa tu la vioo kwa ajili ya kuhifadhia nyama ili isiguswe guswe na nzi . Ili kipunguza gharama za kuendeshea nikachukua mkaa kwenye lita 10 ( wale waishio sehemu zinazochoma mkaa nadhani watanielewa hapa vizuri ).

Lakini pia nikapata wazo kwamba ili nipate maokoto ya kutosha vizuri kukang'aa nyama ya nguruwe pekee na kuuzia watu inaweza isinipe faida sana nikajisema " hata ikitokea mteja anataka kitimoto nitamuuzia tu " hivyo nikatafuta mzani . Yes, lakini kauli ya jamaa yangu ikanijia kichani. " faida haiji tu lazima uitafute " basi nikamcheki jamaa na kumpa wazo langu , mimi huyo kwenye simu " halo master sasa nimeona badala ya kuuza nyama pekee yake nimeonelea si vibaya pia nikawa nauza pia kwa kupimisha ili niwateke wateja wote wa mbuzi katoliki wa hili eneo " jamaa huyo anajibu sasa " safii sana master unaakili sana na ndiyo maana kila siku mimi huwa nakwambia wewe ni kichwa cha biashara ila sasa hebu lete huo mzani nikifundishe kitu " .

Basi bwana mimi huyo na mzani mbaka kwa kiongozi wangu wa biashara tukaenda kwa mshikaji wake ukaurekebisha vizuri mzani " lengo, ni ili mzani uwe unawaibia kidogo wateja ( wale wanaofanya biashara za kipima pima watakuwa wananielewa vizuri hapa juu ya huu uhuni ). Basi bwana siku hazigandi biashara ikaanza .

Siku ya kwanza nilipiga maokoto vizuri kwani nilisukuma kama kilo 5 hivi plus watu kibao kuulizia ulizia ( moyoni nikajisema mambo si haya ) siku ya pili sukuma kilo zote 7 , ya tatu sukuma kilo 5 tena . Nikajisea " sasa hii biashara nshaijua vizuri hapa ili nikimbizane vizuri na hawa wateja ngoja nilete kilo 10 sasa, eehh hili eneo linataka kilo 10 " . Baada ya kuleta kilo 10 siyo mbaya nilisukuma kama kilo 6 hivi.

Lakini sasa balaa lilianza wiki ya pili toka nianze biashara eneo lile . Uwezi amini jumatatu ya wiki ya pili toka nilipoanzisha kijiwe nikiwa nimeweka kilo kumi kwenye kabati langu la kuhifadhia nyama . Alikuja bibi mmoja akipiga "" hodi hodi mwanangu , mimi sijambo bibi shikamoo bibi marihaba mwanangu . Mimi karibu bibi asante . Mwanangu nilikuwa naulizia kama nyama ipo ??."
Mmmhh mimi nikaguna nakujiuliza swali inamaana nyama yote hii kwenye kabati bibi haioni ??. Nikahitimisha kwa kujisemea mmhh japo wote tutazeka ila uzee mbaya sanaa. Oky bibi nyama ipo yakutosha kabisa kwani ulikuwa unaitaji kiasi gani bibi yangu ??. Bibi hapana nilikuja kwanza kuulizia kama ipo . Nakuondoka zake , nikiwatafakari kilichotokea tena kwenye saa sita vijana wawili kwa mbali wakiwa wanapita " oyii mwanangu,,,,,,,,,, vipi ?? Mie oiiii!! oiiii !!! oiiiii!!! poa wakuu vipi leo huna mzigo nini ?? Eehh nikayarudisha macho chap sandukuni kujilidhisha kama nyama ipo au haipo maana sielewi kwanini watu wananiuliza vile .. kucheki mzigo upo sasa kwanini naulizwa vile ??. Mzigo hupo tena wakutoshaaaa wazee huku nikitumia kidole changu kuwaoneshea mali iliyopo kabatini . Hinakwelee usiwaze jombaa tukipata mafekechee basi tutakuja kuchangamsha kijiwe . Amani amani wazee ntafurahi sana mkija.


Okay kumalizia tu wiki ile ilienda vile kwa kuulizwa kama nyama ipo na hata kwenye kuuza nyama ningeuza sanaa ni kilo 3 tu . Wiki ya tatu nilipoona hali imezidikuwa tete na tayari nimeshaingiliwa na hasara nusu ya mtaji wangu . Nikajisemea " bora nusu shari kuliko shari kamili acha nifikirie biashara nyingine huenda walimwengu wa huu mtaa hawajaipenda biashara niifanyayo nikafunga na kwasasa nipo nauza mafuta ya kupikia mtaa mwingine wale wote wenye connection nzuri ya wapi ntapata mafuta kwa bei chee tuchekiane nilipo dumu 80, 000/= ( huku tunapima kwa kilo na siyo kwa lita ) na lita moja wengi tunafanya 4500/=. Kwasasa
 
Niliwahi fungua banda la chupusi hapo dsm mabibo mwanzoni nilipiga mafaida ila huwezi amini mtaji ulitejetea wote na majiko nikayagawa
Kuna watu lazima walienda kuichezea biashara yako . Kwenye biashara haya mambo yapo sana bahati mbaya hutokuja kaa usikie vijana wetu wakifundishwa vyuoni juu ya kile kinachoendelea mtaani juu ya biashara .
 
Kuna watu lazima walienda kuichezea biashara yako . Kwenye biashara haya mambo yapo sana bahati mbaya hutokuja kaa usikie vijana wetu wakifundishwa vyuoni juu ya kile kinachoendelea mtaani juu ya biashara .
Uchawi kitu kingine, usione wafanya biashara wakubwa jua wamepitia mengi kufika hapo
 
nipo kwenye biashara mwaka wa 18 lakini kuna mengi..wakikushindwa kwa nguvu za giza watatumia midomo....wivu na kukuzulia mambo...yaani umaskini wa wengi ni mzigo sana..akikuona unajenga anawaza tunampa zaidi...nilisoma kitabu kimoja zaidi ya miaka 12 huko nyuma kinaitwa aletter of businessman to his son.....kuna mstari unamwambia don't spend to impress....kwa hio mambo haya yapo sana hata ugaibuni...
 
tupe mkasa
2021 mwanzoni nilikua Kuna mahalo nimefungua Maabara ,Hilo eneo kulikua na gereji kubwa ,wafyatua matofali ,waosha magari na wauza mbao pia karibu na pale kulikua na watengeneza majiko.

Wakati nilipokua pale Ili nipate msosi ilibidi utembee kupandisha kilima ndo Kuna mgahawa na wale wenye mgahawa walikua wanachukua oda chini kwa bondeni. Wazo la baishara ya chakula likanijia nikasema ngoja nimpigie bao na niboreshe zaidi.

Nikakidi frem nikanunua meza na vitu vyote vilivyohitajika na nikatenga bajeti ya sh laki 1 na 50 kama ya chakula. Basi bwana niliweka mbinu kabambe kwenye Kila sahani niliweka na kipande Cha tunda na kwenye supu niliweka na viazi viwili au kipande Cha muhogo kiukweli nilipata wateja mwanzo nikasema yes bingo.

Dada niliyemuweka pale nilimpa masharti yafuatayo nilimpa msingi nilikua nataka hesabu ya sh elfu 10 tu kwa siku na msingi wangu uwe pale pale atajua mwenye akiapata faida hata milioni ila Mimi nataka msingi na 10 yangu viwepo. Pia kwenye ishu ya vinywaji tulikubaliana nitauza Mimi ila nitampa asilimia 10 ya faida.

Yule dada alikua msafi na alijitahidi sana kufanya kazi mara yakaanza mapichapicha anauza chakula ikifika jioni Hela hamna hasara ikaanza sijakaa sawa vyakula vilivyopikwa asubuhi kuharibika,mwanzoni nikajua labda ananiletea ujanja ila nilienda shuhudia mwenyewe mara kadhaa na ghafla wale waliokua wakija mwanzo walipita kama wanaaga mahiti...kiufupi nilipata hasara ya karibu milioni moja. Hilo jambo lilitokea within one month tangu biashara kuanza na yule dada alipokua Kila akija kazini anapata kuumwa kichwa mwenyewe akaacha kazi na biashara ikafia pale.

Baadae kidogo ndo Kuna mtu akanitonya zile frem ziliwahi kukaa miaka 2 bila mpangaji na huko nyuma wapangaji wakija pale wanashindwa na pia yule mama wa juu kule wa chakula Kila aliyekuja kucompete nae alishindwa hivyo ilibidi nijipnage kabla kufungua.
 
Kuna mfanyabiwshara mmoja anamiliki dispensary bas akiona wagonjwa wamepungua anawaita watu wa dawa kuja kufanya tiba usiku wa manane
 
Back
Top Bottom