Namna nilivyoanza biashara kwa uoga mpaka kufikia hapa nilipo, nilichogundua biashara haihitaji elimu nyingi ya darasani

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
11,161
15,835
Wakuu naomba kufupisha historia yangu ya kuanzisha biashara nilipokuwa kwenye kibarua fulani nina imani hata wewe itakusaidia sana pengine kama sio wewe ni mwingine.

Miaka kadhaa nyuma nilipokuwa nimepata kibarua fulani nilikuwa nimekaa mda mrefu nikiwaza biashara kichwani ila nilikuwa naogopa sana kuanza kwa kuhofia kufeli aisee.

Nimekaa kama miaka mitatu hivi nawaza tu nina mshahara sina kitu kingine cha kuniingizia pesa,basi mpaka nikaoa iko hivyo,siku moja nikajitoa ufahamu tu nikasema acha niingie tu.

Nikaanza utafiti wa kujua bidhaa ninayoitaka kwa maeneo yangu inauzwaje,je ni kama yangu? Nipunguzaje ili niwavute wateja kwangu?

Baada ya kutafiti nikajua kuwa nataakiwa nipunguze bei kidogo ili niwavute,basi nikaanza.

Nakumbuka nikaenda ilala kuchukua tisheti za mtumba kwa mdau mmoja hivi kwa bei ya jumla ya tsh 3,000 tishert kali quality nilichukua kama 20 hivi ikawa kama jumla tsh 60,000.

Basi nikasafirisha mpaka sehemu nilipo,nikatafuta sehemu ya jamaa flani alikuwa anauza kanzu na vitu vingine,nikaongea nae nikaweka tshirt zangu 20. Jamaa akaniambia kwa kuwa ndo unaanza we angalia upepo then utaangalia unanipozaje kibanda hiki.nikamwambia ok.

Ile sehemu ilikuwa ni barabarani kwa pembeni kidogo,watu wanapita wanaona biashara, nikasema tishert watu wanavaa acha nijiripue tu.

Nilipoziweka zile tshirt siku ya kwanza niliuza 8 @ 7000 = 56000.

Siku ya pili nikauza 6 @ 7000 = 42000.

Siku ya tatu nikauza tena 6 @ 7000 = 42000.

Jumla kwa siku tatu nikapata 140000 ukitoa na pesa ya mtaji 60000 basi ikabaki 80000 nzima ni mtaji.nikasema aisee kumbe mambo yako hivi.

Nikaenda tena kuchukua mzigo pisi kama 30 hivi kwa uoga uoga @ tsh 3000 ambazo ikawa jumla 90000.

Kumbuka kuwa nilikuwa nachukua kwa mdau ambaye yeye ni mzoefu kwa hiyo nikawa nachaguliwa zile tsheti zenye ubora kidogo nikaona sio kesi tupate wote.

Safari hii niliuza mzigo huu kwa siku 7. Nikaounguza bei kidogo ili watenga wawe wengi na pesa izunguke sana kwa sababu kuwa na buku inayozunguka kwenye biashara kwa mwezi mmoja ikazalisha ni bora kuliko kuwa na alfu kumi mfukoni isiyozalisha.

Basi kwa siku saba nikauza mzigo wa pisi 30,pisi 10 @ kwa 6000 na pisi 20 @ 7000. Nikapata jumla 200,000.

Sasa hapo nikatoa na tsh 90,000 nikapata faida 110,000.

Hapo nikaanza kuwa sirias rasmi katika biashara,nikagundua kuwa biashara inataka utafiti na sehemu husika rafiki then mtegemee Mungu tu mambo yataenda.

Sitaki kuweka hesabu za nauli na chakula hapo na mavazi kwa sababu hayo yote nilikuwa nayafanya na nayapata kabla ya hii biashara kwa hiyo siwezi kutoa pesa ya kwenye biashara wakati hata kabla ya hii biashara pesa hiyo ilikuepo,sitaki kuitia mzigo biashara ikiwa bado ni changa.

Formuila yangu ni kuwa Biashara changa inakutegemea wewe,biashara iliyokomaa wwwe ndo unaitegemea.

Hii biashara ni changa kwa hiyo mimi ndo natakiwa niiiramishe kwa kuiwekeza zaidi,lakini sasa nikisema niitegemee hii biashara kuniimarisha mimi kwa wakati huu nitafeli.

Ikishakomaa sasa ntaanza kuagana rasmi na mshahara na kuuweka saving wote huku pesa yote ya malazi ikitoka kwenye biashara wakati huo imeshakomaa.

Biashara changa ni kama mtu anayeanza maisha,asibebeshwe majukumu mengi ataporomoka na kuishia patupu asione wapi anaelekea.

Kwa wale wanaoamini kuwa biashara ni lazima uwe umesoma sana masomo ya biashara darasani na ukaenda chuoni ukafuzu kwq ma GPA makubwa makubwa basi nawaambia tu kuwa wanachokisoma kilianza kufanywa kwanza kwa vitendo.

Kabla ya kuwepo masomo ya biashara basi vilianza vvitendo vya hiyo biashara yenyewe,watu walianza kufanya biashara mtaani wakaona hali zinavyokwenda wakaona elimu hiyo waihamishie kwenye makaratasi,so asili ya mambo ni vitendo hapo,makaratasi huja baadae kwa ajili ya kuhifadhi ujuzi usipotee.

Hata fani ya upasuaji ili uusome upasuaji lazima iwe kuna mtu aliufanya kwa vitendo kisha aliyoyaona ndo akayaandika sasa ili wengine wasiokuwepo na wengi wapate elimu.

Kwa hiyo kumbuka kuwa mafanikio katuka biashara ni kuifanya na sio kuisoma tu bila kuifanya,ubapozidi kufanya utasoma mengi zaidi kwa mujibu wa mazingira yalivyo.
 
Hongera mkuu. Tatizo watu wengine wanadhani mpaka mtu uwe na 5 millions ndo ufungue biashara...

Sent using amfifiro
Mkuu nilikuwa siwazi kabisa kuhusu biashara,ila baadae nikashtuka,na nashukuru nilioa mapema sana baada ya kupata kibarua tu kwa sababu sikuwa mtu wa totoz,nilikuwa domo zege hatari,nikaona solution kuoa,nashkuru nilioa mapema na kwa asilimia kubwa gharama zangu nilizitumia kumhonga mke wangu kuhakikisha sivuki steji ya kuhonga.

Nilipooa nilianza kushtuka kuwa kumbe mshahara hautoshi,nilianza kujua kuwa kumbe i have to do something out of my job.

Bila kuoa ningebweteka sana,ila nikamshirikisha wife kabisa,mpaka leo nachukua tishert mpaka 100 naweka mzigoni,japokuwa natarajia kutafuta kibanda changu mwwnywwe niachane na mshikaji.

Majuzi nilichukua tisheti 100 kila moja tsh 3500,jumla ni 350,000.

Nimeuza 70,50 kwa kila moja tsh 7000 = 350000.na 20 kila moja 8000 = 160,000.

Jumla hapo ni 350000+160000= 510000.
510000-350000 =160000.hiyo 160000 ni faida kabla ya mzigo kuisha.

Zimebaki pisi 30 ambazo nataka niuze kwa 5000 tu kwa maana nipate 150000 nikiongeza na ile 160000 inakuwa 310000.

Hapa faida inakuwa 310000 na pesa ya mzigo 350,000 imerudi.

Nawaza kuongeza mzigo uwe wa 500000 hivi.changamoto kubwa siwezi kuchukua mzigo mwingi kwa sababu sehemu ya kudowea kishkaji.natafuta location nzuri nihame niwe huru japokuwa jamaa hana noma.

Wakati huo kibarua changu bado naendelea nacho wakuu mana ndo kimenifikisha hapa pakuona kuwa mshahara is just for saving.
 
Sijaona hapo;-
>Cost za nauli...

Mimi nina kibarua, kila siku nilikuwa na safari za mjini hivyo hata bila biashara nilikuwa natumia nauli,sasa hivi siweI kutoa pesa ya nauli kwenye biashara kwa sababu nahesabu ni safari zangu za kila siku tokea zamani.

Kuhusu kula natumia mshahara wangu ambaonaupata kila mwisho wa mwezi.

Biashara yangu haina muda mrefu sana.

Jambo kubwa ambalo nililizingatia ni kuwa,mimi nafanya nilisema nafanya biashara sio kama watu wengine,nafanya biashara huku nina kazi nyingine,lengo kupunguza ukali wa maisha yangu.

Nilisema na kuweka nia kuwa biahsra changa haihitaji kutiwa mkono,biashara yangu changa siwezi kutoa pesa ya nauli wakati bado ni changa nauli natoa kwenye mshahara,biashara yangu siwezi kutoa pesa ya kula wakati bado ni changa kula natoa kwenye mshahara,biashara yangu siwezi kutoa pesa ya nguo wakati bado ni changa,nguo nanunua mshaharaa.

Haiwezekani baishara yangu inaanza alafu niibebeshe majukumu makubwa kiasi hicho,biashara hiyo hoyo nipate faida hapo,matumizi ya lazima nifanye hapo,biashara yangu nikaona haitokiwa.

Hapa nakusanya mtaji then nitakapoona imeimarika vilivyo sasa naanza kuachana rasmi namshahara na kuanza kuitegemea biashara.

Biashara changa inakutegemea wewe,biashara iliyokomaa wwwe ndo unaitegemea.

NB ; hii ni formula yangu ambayo inaweza isiwafae wengine.
 
Biashara ni uthubutu, na hakuna anayeyajua yaliyomo katika biashara ila mfanyabiashara.

Shukran kwa kushare nasi uzoefu wako, na mungu akufanyie wepesi katika biashara yako.
Alafu nilichogundua mkuu,ukianza biashara na fursa zaidi za kujiongeza zinakuja.

Kuna kitabu cha dada mmoja anaitwa rhonda byrne kama sikosei kinaitwa "the secret" kuna kitu kikubwa alikizungumza mule nacho ni "the law of attraction"

Alikusudia sana kuwa unapokuwa unafanya mambo basi jua ya kuwa mambo mengine yanayohusu hayo unayoyafanya ndo yanazidi kujivuta kwako.

Lakini yeye alijokita zaidi kwenye kufikiri,ila mimi naona hata katika kufanya kwako mambo basi law of attraction inakuwa ina take place vizuri tu.

Ukianza jambo lolote wepesi unakuja mbele,mwanzo ndio mgumu ndio maana bikira ina maumivu kwa dada zetu.
 
Alafu nilichogundua mkuu,ukianza biashara na fursa zaidi za kujiongeza zinakuja.

Kuna kitabu cha dada mmoja anaitwa rhonda byrne kama sikosei kinaitwa "the secret" kuna kitu kikubwa alikizungumza mule nacho ni "the law of attraction"

Alikusudia sana kuwa unapokuwa unafanya mambo basi jua ya kuwa mambo mengine yanayohusu hayo unayoyafanya ndo yanazidi kujivuta kwako.

Lakini yeye alijokita zaidi kwenye kufikiri,ila mimi naona hata katika kufanya kwako mambo basi law of attraction inakuwa ina take place vizuri tu.

Ukianza jambo lolote wepesi unakuja mbele,mwanzo ndio mgumu ndio maana bikira ina maumivu kwa dada zetu.
Ukianza jambo lolote wepesi unakuja mbele,mwanzo ndio mgumu ndio maana bikira ina maumivu kwa dada zetu.
 
Kabla ya kuwepo masomo ya biashara basi vilianza vvitendo vya hiyo biashara yenyewe,watu walianza kufanya biashara mtaani wakaona hali zinavyokwenda wakaona elimu hiyo waihamishie kwenye makaratasi,so asili ya mambo ni vitendo hapo,makaratasi huja baadae kwa ajili ya kuhifadhi ujuzi usipotee
hapo nimekumanya vyema..
 
hapo nimekumanya vyema..

Mkuu umeamka daku nini.

Kama umenimanya vyema basi habari ndo hiyo mkuu.

Hakuna fani ambayo asili yake ilikuwa maneno matupu,hata falsafa watu walianza kufikiria na kuyatafakari mambo then mawwzo yao ndo wakayahamishia kwenye karatasi.

Ukiwasoma wana falsafa wa hapo mwanzo huoni kuwa kuna sehemu yoyote walienda chuoni wakasoma na kuhitimu,utaona stori za kusoma zimeanza kwao tu
 
Wakuu naomba kufupisha historia yangu ya kuanzisha biashara nilipokuwa kwenye kibarua fulani nina imani hata wewe itakusaidia sana pengine kama sio wewe ni mwingine.

Miaka kadhaa nyuma nilipokuwa nimepata kibarua fulani nilikuwa nimekaa mda mrefu nikiwaza biashara kichwani ila nilikuwa naogopa sana kuanza kwa kuhofia kufeli aisee...
Asante kwa stori yako tamu. Hadithi za Abunuazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nilikuwa siwazi kabisa kuhusu biashara,ila baadae nikashtuka,na nashukuru nilioa mapema sana baada ya kupata kibarua tu kwa sababu sikuwa mtu wa totoz,nilikuwa domo zege hatari, nikaona solution kuoa,nashkuru nilioa mapema na kwa asilimia kubwa gharama zangu nilizitumia kumhonga mke wangu kuhakikisha sivuki steji ya kuhonga...
Fungua hapo hapo pembeni yake tafuta hata banda ama muombe mshee kodi ukihama sasa hivi unakoenda unaanza upya
 
Back
Top Bottom