Namna mchawi sugu alivyouawa

KAKA NASOKI

Senior Member
May 25, 2016
191
212
Kuna mchawi mmoja katika kijiji kimoja, jina la Kijiji limehifadhiwa. Huyu mchawi aliua vijana wengi sana, kwa mfano Kijana akija mjini siku akirudi nyumbani na kupeleka zawadi kwa wazazi wake, asipo mpelekea na yeye, ni kosa unastahili kufa au hata ukipeleka zawadi kwa wazazi inayozidi ya kwake pia ni kosa, unaondoka.

Sasa vijana wakawa wanaogopa kurudi kwao kwa kumhofia huyo mzee. Siku moja vijana wa kijiweni walikaa wakafikiri cha kufanya, basi katika wale vijana mvuta bangi mmoja akasema mimi najitoa nitajaribu kumuua nikifa basi.

Kwa bahati yule mzee alikuwa anakaa peke yake pembezoni mwa Kijiji, kwa hiyo hana choo. Akitaka kujisaidia anaenda kichakani. Yule Mvuta bangi akaenda akamvizia , mzee alipoenda kujisaidia, jamaa akachukua jani akabeba kile kinyesi hadi mlangoni kwa mzee akatupa.

Mzee kutoka akakutana na kinyesi, akapita mtaani akitangaza aliyejisaidia mlangoni kwake, ajitokeze la sivyo kesho saa nane anazikwa.

Basi kwa vile alivyoogopwa yule mzee kila mtu akawauliza watoto wake kama kuna aliyefanya jambo hilo, wote wakakataa na kwa bahati nyingine yule Mvuta angi pia hakusem kuwa yeye ndiye, basi watu wakalala, kukakucha, kufika mchana mzee hoi, saa nane akafa, Kijiji kikaingia amani na vijana wakaanza kwenda kijijini kusalimia bila woga.

Baada ya mwaka ndipo Mvuta bangi aksema alichokifanya ila akasema aliogopa kusema wakati ule akihofia mrithi mikoba asimdhuru.

Nimesimuliwa na Kinyozi aliyekuwa ananinyoa pale Gomz au Gongo la Mboto.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom