Namkumbuka Prof. Kighoma Malima

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,184
30,530
NAMKUMBUKA PROF. KIGHOMA MALIMA

Siku kama ya leo tarehe 5 August 1995 mida ya kama saa nne asubuhi mpwa wangu akitokea Makao Makuu ya NRA Kariakoo alinifahamisha kuwa Prof. Malima amefariki mjini London usiku.

Simanzi na majonzi yangu hayasemeki.

Nilijuana Prof. Malima katika mwaka wake wa mwisho duniani na tukizungumza mengi.

Kwa muda mfupi wa kujuana kwetu nilijifunza mengi kama kumbukumbu yangu kwake kukumbuka kifo chake nataka In Shaa Allah kukumbuka yale yaliyopitika miezi ile ya mwisho ya maisha ya Prof. Malima katika siasa za Tanzania wakati taifa likijiandaa kwa uchaguzi mkuu wa kwanza baada ya kurejeshwa vyama vingi.

Siku ya Jumapili tarehe 17 July, 1994 Prof. Malima alihutubia mkutano mkubwa sana Viwanja Vya Uyui Tabora.

Hotuba hii ilikuja kupewa jina, ‘’Usia wa Malima,’’ na casette zake zilinunuliwa sana baada ya kifo chake.

Kabla Prof. Malima hajapanda jukwaani alitanguliwa na Bilal Rehani Waukela akiwa amavaa nguo zake alizokuwa amevaa mwaka wa 1964 alipowekwa kuzuizini Jela ya Uyui.

Kosa la Waikela ilikuwa ‘’kuchanganya dini na siasa.’’

Uhuru ulikuja na changamoto nyingi sana mojawapo ilikuwa nafasi ya Uislam katika Tanganyika huru.

Hili katika miaka ile ya mwanzo lilikuja kuwa tatizo kubwa kiasi kupelekea kuvunjwa kwa Baraza la Wazee wa TANU chini ya Mwenyekiti Mzee Iddi Tulio.

Katika hotuba yake Waikela alisema kuwa anarudi tena kwenye siasa kumuunga mkono Prof. Malima katika kuleta haki na usawa kwa wanachi wote wa Tanzania ambazo ndiyo vilikuwa vitu villivyopiganiwa na TANU wakati wa kudai uhuru.

Prof. Malima alipopanda jukukwaani alisema kuwa CCM imjitoa katika kupigania haki na wa usawa kwa wananchi wake wote na kujenga tabaka linalohodhi fursa zote.

Prof. Malima akaeleza kuwa kwa ajili hiyo anajitoa CCM siku hiyo ya Jumapili tarehe 7 July 1994, na kujiunga na chama cha upinzani National Construction Alliance (NRA) kuleta haki na usawa kwa raia wote wa Tanzania.

Siku ya pili wajumbe wa Mkutano Mkuu wa NRA walipofika Tabora Railway Station ambako walikuwa wamekodi mabehewa na kuyalipia kuwarejesha Dar es Salaam walikuta hawakupangiwa mabehewa yoyote.

Prof. Malima magazeti yalikuwa yametangaza kuwa atajitoa CCM kutoka Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Tabora siku ya pili walikuwa na fursa ya kusahihisha kuwa Prof. Malima hakujitoa CCM msikitni bali kwenye Viwanja Vya Uyui lakini wahariri hawakuona haja ya kufanya hivyo.

Wahariri hawa ambao walikuwa na chuki kubwa na Prof. Malima walikaa kimya wakitaka watu waamini kuwa Prof. Malima alishindwa kujitoa CCM msikitini Tabora kwa kuwa Waislam wahakumruhusu ‘’kuchanganya dini na siasa.’’

Prof. Malima akatanganza kugombea urais kupitia chama cha National Reconstruction Alliance (NRA).

Joto la siasa lilikuwa linapanda kwa kasi kubwa sana.

Benjamin Mkapa alikuwa anapambana na Jakaya Mrisho Kikwete na Cleopa Msuya ndani ya CCM na alijizatiti vyema kwa kuwa na wachapaji magazeti wakubwa nchini ndani ya kamati yake ya kugombea urais, Ferdinand Ruhinda na Jenerali Ulimwengu.

Augustine Mrema alikuwa anamwaga vumbi jingi nchini ndani ya NCCR Magaeuzi.

Mrema alikuwa na jeshi kubwa la watu wa mtaani ambao wakati mwingine waliamua ‘’kumbeba kiti kiti cha mfalme.’’

Hili liliwakera sana CCM kiasi Mwalimu Nyerere akaingilia kati kumtetea Mrema akasema kama kuna watu wanapenda kumbeba acheni wambebe.

Prof. Malima alikuwa na nani?

Lilikuwapo kundi kubwa lililodhamiria kumuunga mkono Prof. Malima na kundi hili lilitia hofu wengi kwani siasa za Tanzania ghafla zikageuka zikarudi nyuma na kuchukua sura ya wakati TANU inapigania uhuru wa Tanganyika.

Kidogo hali ilikuwa inatisha wachambuzi wa siasa wakijiuliza kuna agenda gani inayotaka kuwekwa na Prof. Malima katika uchaguzi ulio karibu?

Mkutano Maalum wa Halmashari Kuu ya CCM ulioitishwa kuchagua mgombea mmoja wa CCM kupeperusha bendera yake ilimchamgua Jakaya Mrisho Kikwete katika duru ya kwanza ya kupiga kura Mkapa akifuatilika nyuma kwa karibu na Msuya akiwa wa mwisho.

Kikwete alikuwa na ‘’Mtandao.’’

Lakini kwa kuwa Kikwete hakupata idadi inayotakiwa ya ushindi ikabidi wajumbe warudie kupiga kura upya kuchagua baina ya Kikwete na Mkapa.

Mkapa akashinda.

Kwenye maombolezo na maziko ya Mkapa, Kikwete katika hotuba yake amesema kuwa yeye alisukumwa kugombea urais na iko siku ataeleza ilikuwaje.

Hakika hili ni moja katika mambo ambayo yamekuwa yakihanganisha sana akili yangu na nimetengeneza fikra juu ya fikra kutaka kujua kulikuwa na nini lakini kwa kuwa Kikwete mwenyewe tena hadharani kasema hili atakuja siku alieleze ni bora tukavuta subra.

Mwaka wa 1992 Malima alipogombea moja katika viti 20 vya nafasi ya Halmashauri Kuu aliposhindwa maadui zake waliimba nyimbo ndani ya ukumbi kwa sauti za chini ndani ya Ukumbi wa Chimwaga Dodoma.

Kuna kundi likimchukia sana Prof. Malima na walimpania kuwa hapiti.

Mwaka wa 1995 Kikwete aliposhindwa na Mkapa nyimbo zile zile zilisikika zikiimbwa vile vile tena kwa sauti ya chini .

Mwanafunzi wa siasa za Afrika inataka utulize sana kichwa chako kuelewa jinsi mchezo huu unavyochezwa na sheria zake.
 
Kikwete mwenyewe tena hadharani kasema hili atakuja siku alieleze ni bora tukavuta subra.

Shk, Mohamed Said.

Tutavuta subira hadi lini? -- subira inatakiwa iwe "time framed" ikizingatiwa kuwa ajuaye kesho ni Mungu tu isitoshe Mwanadamu kaumbwa kwa "haraka" asipopata majibu kwa muda basi "atajitungia majibu".

Nakushauri na kukuomba, kama mwanahistoria, nenda kamkabili JM kikwete na umuulize juu ya jambo hilo ili habari zake zihifadhiwe kama historia.
 
Ndio maana watawala kuuona ufalme wa mungu ni vigumu kiasi ambacho ngamia anaweza kuingia kwenye tundu la sindano kwaulaiisi zaidi yao
 
Ishu ya Malima ilishawekwa hadharani tangu muda mfupi baada ya kufariki. Akiwa waziri wa fedha alifungua account ya Kighoma Malima - Waziri wa fedha huko London; kwa hiyo sehemu ya misaada ya IMF na World Bank iliyokuwa inakuja Tanzania wakati akiwa Waziri wa fedha, ilikuwa inawekwa kwenye account hiyo; signatory alikuwa ni yeye peke yake, wala serikali ya Tanzania haikuwa na taarifa ya uwepo wa account hiyo.

Siku alipoambiwa kujiuzuru na Mzee Mwinyi kutokana na pressure ya World bank, alifanya kirahisi tu kwa vile ile account ya London ilikuwa imeshiba wakati huo. Ndipo ama alianzisha NRA au alijiunga na NRA tena kwa sera ya kuwa Nyerere alionea sana waislamu kwa kuwafelisha mitihani hadi yeye alipokuwa waziri wa elimu ndipo akaweka utaratibu wa kutumia namba- jambo ambalo lilikuwa ni uwongo kabisa kwani utaratibu wa kutumia namba kwenye mitihani ulikuwepo tangu enzi za mkoloni.

Vile vile hiyo ilikuwa ni kukosa fadhila kwa Nyerere kwani wakati Malima anamaliza form sxz alikuwa Katibu wa TANU Rufiji na Nyerere alimpenda kama kijana msomi; ndiye akamtafutia skolarship ya kwenda Marekani ambako ndiko Malima alikopatia digirii zake zote kutokana na hiyo connection ya kwanza ya Nyerere.

Baada ya kuwa ameshaacha nafasi ya waziri wa fedha, akaenda kuhiji na familia yake akitegemea kumtembelea mwanaye mmoja aliyekuwa anasoma London na kujijazilia pesa kidogo kutoka kwenye account yake hiyo ya Waziri wa Fedha za kurudi nazo Tanzania. Sasa alipokwenda Benk kuchukua hela hizo akaambiwa kuwa account iko frozen kwa vile yeye siyo waziri wa fedha tena. Mshituko wa Moyo!!
 
Tawasifu, since two years ago!!!--- my dog is barking, I can't wait.

The Crystal ball is inevitable
Mokaze,
In Shaa Allah tusubiri.

My dog is barking...
Hii sikuwa naijua umenisomesha kaka.

Hii Crystal Ball mie nafungua mlango tukae kwenye chess board.

Nani anaweza kuwa na nguvu ya kuweza kumsukuma mtu kuchukua madaraka ya juu kabisa katika nchi.

The ball is in your court.
 
Mokaze,
In Shaa Allah tusubiri.

My dog is barking...
Hii sikuwa naijua umenisomesha kaka.

Hii Crystal Ball mie nafungua mlango tukae kwenye chess board.

Nani anaweza kuwa na nguvu ya kuweza kumsukuma mtu kuchukua madaraka ya juu kabisa katika nchi.

The ball is in your court.


Sawa kaka.
 
Back
Top Bottom