Mzee Mwinyi asingekuwa Mcha Mungu hali ya Uchumi aliyoikuta 1985 angeweza kuuza kila kitu, ashukuliwe Prof. Malima na Prof. Lipumba!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,036
142,107
Waliokuwepo zama hizo na wasio Wanafiki watanielewa, mzee Mwinyi aliikuta nchi katika halo Ngumu ya kiuchumi kuliko Rais mwingine yoyote

Kipekee niwashukuru Prof Kighoma Malima aliyekuwa Waziri wa Fedha, Prof Lipumba aliyekuwa Mshauri wa Uchumi Ikulu, Hassan Diria Waziri Mambo ya Nje, Lyatonga Mrema Waziri wa Mambo ya Ndani na Mzee Kitwana Kondo KK Meta wa Jiji la DSM kwa kumshauri ipasavyo Mzee Mwinyi hadi tukatoboa

Mungu wa mbinguni mbariki mzee Mwinyi!
 
Waliokuwepo zama hizo na wasio Wanafiki watanielewa, mzee Mwinyi aliikuta nchi katika halo Ngumu ya kiuchumi kuliko Rais mwingine yoyote...
Prof. Malima alimuingiza Mzee Mwinyi ktk mgogoro na wafadhili.

Ilipelekea mpaka kuundwa kwa tume kuchunguza utendaji wa wizara kuhusu misamaha ya kodi iliyoongozwa na CAG wa wakati huo Bw.Mohammed Aboud.

Mageuzi ya uchumi ya kipindi cha awamu ya pili yalisimamiwa na waziri wa kwanza wa fedha ktk awamu hiyo Bw.Cleopa David Msuya.

Ndio maana wakiwa kule Ngurdoto ktk semina elekezi Mzee Kikwete alimtambulisha Mzee Msuya kama " baba wa mageuzi ya kiuchumi " ya Tanzania.
 
Sasa mwangalie Msuya na Mwanga kisha mwangalie Alhaj Prof Kighoma Malima na Mkuranga

Niishie hapo!

..Malima alikuwa mbunge wa Mkuranga au Kisarawe?

..Mwanga ndiko alikotoka Mtanganyika wa kwanza kupata shahada ya London University, akiitwa Abdulrahman Msangi.

..unapolinganisha Mwanga na Kisarawe / Mkuranga lazima uzingatie HISTORIA.

..Niishie hapo ili tusitoke nje ya mada.

NB:

..Abdulrahman Msangi alikuja kuwa amidi[ dean] wa kwanza mzalendo wa kitivo cha Sayansi Udsm.
 
..Malima alikuwa mbunge wa Mkuranga au Kisarawe?

..Mwanga ndiko alikotoka Mtanganyika wa kwanza kupata shahada ya London University, akiitwa Abdulrahman Msangi.
...
Mkuranga Ndio kwao Malima achilia mbali jimbo Kabla halijagawanywa

Mwanga ilipaishwa kwa ufisadi wa huyo mtanzania wa mwanzo mwanzo kuhitimu Makerere!

Niishie hapo
 
Sasa mwangalie Msuya na Mwanga kisha mwangalie Alhaj Prof Kighoma Malima na Mkuranga

Niishie hapo!
Kuna shida ya msingi na ya kale kwenye jamii kama za Mkuranga, ELIMU DUNI YA KISEKYULA. Hili ndio chanzo cha yote, na yanaendelea hadi leo. Hata Msuya angekuwa mbunge wa Mkuranga, na kuiba na kuwekeza huko mkuranga, na Malima angetoka Mwanga, bado mkuranga ingekuwa duni na mwanga ingepiga hatua.
 
Back
Top Bottom