MwanajamiiOne
Platinum Member
- Jul 24, 2008
- 10,470
- 6,588
- Thread starter
-
- #61
...😀 hapo kwenye wekundu Mj'1, wewe si wa kwanza kulitamka hilo wala si wa mwisho. Nishawasikia wanawake wengi wakiyatamka hayo kipindi cha misukosuko, na wengine wachache hata baada ya kuachana na wenzi wao...
Tatizo kila mwanaume (wa kisasa) utayekutana naye ana sifa hizo hizo za 'yai bichi'. Maovu ya mtu ni mwonekano wa tabia za nje, ambapo wewe ukiwa ni dereva wa mawazo yako una hiari ukwepe au uparamie.
Fikiria wewe ni dereva na mbele kuna shimo, ...Ukilikwepa hutaliumiza gari lako, ukiliparamia unajiumiza mwenyewe ilhali shimo linabakia pale pale. Mwache na 'kilema chake', huwezi kumtibu.
Chukulia mazuri yake (uliyompendea) yafunike hicho kilema.
Aksante Mbu maneno yako mazito ila duh ngoja nijaribu maana sina tena nguvu wala uvumilivu.
Nitawezaje kuondoa dhana hiyo wakati unaona kabisa dharau na chuki usoni kwa mwenza? au na haya ni dhana? Mwenzangu huyu haoni vibaya kukwambia 'you know everything that is happening is because of YOU' au unajua wewe ni mfitini ? to me kwa kweli sidhani kama nawezamshutumu mpenzi wangu so direct naona hii- Blaming everything kwake?? tena macho makavu hata kama ninauhakika there is no truth about it?
Ntajaribu Mbu. Nitafuata ushauri wako!
...😀 ngoja nikupe siri, hata ningekuwa mimi katika nafasi yako sasa ningekuwa sina nguvu. I empathize with you Mj1. lakini kiukweli, hayo yote unayoyaona sasa, hata kama utakuwa na mume mpaka kuzikana ipo siku atakuonyesha makucha yake hivyo hivyo!
Hiyo sura ya ndita, majibu makali ya mkato, blames na aggressions zote ni matokeo na mkusanyiko wa hisia za binaadamu ambaye kashindwa kabisa kufikisha ujumbe wako kwako kwa njia nyingine.
Back off!...
Give him a chance to calm down...
japo ni ngumu, usimuonyeshe "ume panic!", usimuonyeshe umenyong'onyea saaana, ... mpe nafasi.... mwanaume anahitaji nafasi kurudisha 'adrenaline' levels zake kwenye hali ya kawaida... mpe nafasi nyingine...
Nakuhakikishia, akisha calm down, hata kama atajifanyisha hataki kuongea (kwa aibu zake), mtaweza kuongea kwa kituo 'palipita shetani gani'...
Mpe muda mwanaume, atapokuwa kwenye hali ya kawaida (as if hakuna lililotokea) ndipo hapo itapokuwa zamu yako kumweleza kero na maamuzi yote yaliyo ndani ya moyo wako!...utaona kama hatakupigia magoti kukuomba msamaha.
Ikiwezekana chukua likizo fupi uende mbali na hapo ulipo ili kumpa muda wa kutulia! Mpe muda wa kutulia ndipo ufikishe kwake uamuzi wako.
Siyo nia yangu kumfanya aonekane mbaya (of which sitaki kuamini ni mbaya) but hata yale niliyompendea hapo mwanzo yamefunikwa. Nilikuwa nampenda alivyoweza kunichekesha kunifurahisha kwa matani yake ila sasa siyapati kwani hata kukusemesha ni tabu.
- Nilimpenda kwa kile nilichodhania ni caring yake- kumbe alikuwa ananibembeleza tu niingie kumi nanane- alishaacha kitambo na badala yake yote nikawa nafanya mimi- kubembeleza mimi, vijizawadi mimi n.k.
Sijui ngoja nivumilie pengine atabadilika !!
Kulala sasa inakuwaje mzungu wa nne nini?
Kulala sasa inakuwaje mzungu wa nne nini?
yani luv we ni mpambe....lol wacha kuingilia watu uvungini mwao.
[/COLOR]
sasa huyo x kama alikuona wa maana sana kwanini hakukununua jumla? mambo ya kwenda mbele na kurudi nyuma c mazuri, huwaga nawashauri ma rnds zangu kama umeamua kufanya kitu ufanye bila kujutia baadae, ndio kama hapo MJO aamua kuchukua maamuzi mengine afanye bila kugeuka nyuma na awe ameridhika kutoka rohoni sio afanye huku rohoni anaumia hiyo itam cost, sipo haya mambo ya kusema "kujikumbushia" hayatakiwi kupewa nafac.
kumbe kuna wanume wapuuzi saana dunia hii? nina uhakika mwajamiione ni shori mkali ila jamaa anachezea bahati....najua una maumivu hebu vumilia kidogo sali sana muombe muumba wako aliondoe hili shetwaini.......
NB:muangalia sana fidel80 anaonekana anataka kuchukua substution....kaa nae mbali.....
labda.....maana naona thread zake zinalalamika tuu.....Pia na muona Mwanajamii ni mlalamishi sana,kila tatizo linalotokea ndani ya ndoa yake,badala ya kulisort out na mumewe ana anakuja hapa na kudai analivua pendo da*n******** mwanamke unapaswa kuwa mvumilivu.
kabla sijaoa nilikuwa nafikiri naijua ndoa sana baada ya kuoa mpwa na ile miezi ya honey moon kupita,mpwa nikagundua sijui kitu na nikahisi ninahitaji kurudi darasani.
Yo Yo aksante kwa ushaurikumbe kuna wanume wapuuzi saana dunia hii? nina uhakika mwajamiione ni shori mkali ila jamaa anachezea bahati....najua una maumivu hebu vumilia kidogo sali sana muombe muumba wako aliondoe hili shetwaini.......
NB:muangalia sana fidel80 anaonekana anataka kuchukua substution....kaa nae mbali.....
Mpwa usimtupie lawama huyu jamaa, maana ujasikiliza kwa upande wake,umesikiliza upande mmoja tu.Unajua wanawake nao saa nyingine wanakuwa na mambo ya ajabu ajabu sana ambayo mwanaume huwezi kuyavumilia.
Pia na muona Mwanajamii ni mlalamishi sana,kila tatizo linalotokea ndani ya ndoa yake,badala ya kulisort out na mumewe ana anakuja hapa na kudai analivua pendo da*n******** mwanamke unapaswa kuwa mvumilivu.
Mwanaume akisema hadhani kama kuna future kati yenu, he mean it!! Kasema hivyo au ka-imply hivyo? Inawezekana ume overeact kutokana na situation ilivyokuja. Lakini kama kasema, najua hilo liko moyoni. Kuna wengine husema hivyo tu ili kulazimisha kitu fulani.
From yoote niliyosoma, MJ1 ni typical woman. Wanawake wengi wako hivyo na hudhani kuwa they are doing too much to keep the relationship. Hawaangalii the fact kuwa mwanaume anawekeza zaidi materially na morally.
Kuwa fair kwako mwenyewe na kuwa fair kwake. Hivi wewe huna makosa? Haiwezekani mtoto wa kiume azuke tu na kusema hana future na wewe. You must be sucking him dry! Kutokana na jinsi ulivyoeleza hapa anaonekana ni mtu mstaarabu ambaye hawezi kukufanyia uovu bila sababu.
Simtetei, lakini kabla ya kurusha mkuki ni lazima ujue unauelekeza wapi. Mapenzi is never smooth. Lakini vile vile too late is bad. Watu huwa wanapata uchizi kutokana na kung'ang'ania penzi lililokwisha.
Narudia kule mwanzoni, tafuta muda uliotulia uconfirm kama he meant what he said. If he mean it, take your time na usianze kubembeleza. He may be tired as well as you are.
NB:muangalia sana fidel80 anaonekana anataka kuchukua substution....kaa nae mbali.....
KipimaPembe aksante kwa angalizo but naelewa tofauti ya kuimply na kusema. Those were the words which came out of his mouth tena I asked him mara mbili akanijibu Boldly yes nimesema hiyo!
Being fair nakubali na ndio maana nimesema inawezekana am the one with makosa (ambayo siyatambui) but is that a way ya kumwambia mpenzi wako ili kumrekebisha? If it is then yes am mlalamishi na msumbufu.
Ninaamini hivyo pia kuwa huyu ni mstaarabu ambaye hawezinifanyia uovu but maumivu niyapatayo kila mara yananifanya niamini vingine! Kama penzi limekwisha inakuwaje anashindwa kusema zaidi ya kuumizana mioyo?
Samahanini ndugu zangu najua mnawezafikiria mengi but kwa kweli ni MUNGU mwenyewe ndiye anayejua kinachoendelea.