Kibanda,
Mkuu wangu nikuulize.. wewe unasema ni mwandishi wa habari au sio? inakuwaje wewe huyo huyo unakuwa mtetezi wa Mnyika na Mrema dhidi ya Zitto wakati sidhani kama unaelewa hisia za hao watu.
Kama mwandishi mzuri kwa nini suikimbilie kwa Mnyika na Mrema ukawasikiliza wao wenyewe wanasema nini badala ya wewe mkuu wangu kuendeleza tungo zako ambao hazimsaidii mtu yeyote yule. Mkuu enough! unachosha sana yaani kama mimi ningekuwa Mbowe au mhariri wa Daima basi huna kazi!..
Reporter siku zote huandika maelezo ya watu na sio yake yeye kwa jinsi anavyojishirikisha ktk scandal kisha anakuwa mwandishi.. Haya ni matumizi mabaya sana ya madaraka sawa na Fisadi ambaye anatumia vibaya madaraka yake. Kama wewe ni mwandishi bakia kuwa mwandishi na kama unaandika kama Kibanda zungumza kama Kibanda mpinzani wa Zitto na ukubali kukosolewa pia.
Ndugu yangu Mkandara wewe mwenyewe unakiri kuwa mimi ni mwandishi wa habari halafu unaniuliza ninajuaje juaje hisia za Mnyika na Mrema?. Hiyo ni moja ya kazi za mwandishi wa habari. Ninazijua hisia zao kwa sababu nimefanya nao mazungumzo ya ana kwa ana kuhusu suala hili zima akiwamo na Zitto mwenyewe.
Mbowe si dikteta na mbinafsi kama wewe na ndiyo maana katika gazeti lake la Tanzania Daima habari na taarifa nyingi tu zinazoandikwa zinahusu maamuzi mbalimbali ya kiserikali. Si hayo tumeandika kwa kina taarifa kuhusu masuala yanayohusu vyama vingine vya siasa kama CCM, CUF, TLP na NCCR Mageuzi.
Ni kwa sababu tu kwamba hivi sasa ajenda kuu katika vyombo vyote vya habari nchini hivi sasa ni Uchaguzi wa Chadema na sisi kama wana habari tunao wajibu wa kueleza kile tunachokiona na kukifahamu.
Hata hivyo tunatambua kwamba maandishi yetu yanawakera na wakati mwingine kugusa hisia za wasomaji. Inapotokea hali kama hiyo kwa mwanahabari ni jambo la kulifurahia kwani ndivyo inavyopaswa iwe.
Mimi si reporter nilishavuka huko mwaka 1999. Ni mhariri, ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa. Ninao wajibu (nasisitiza wajibu) na haki ya kuchangia masuala yote yanayoweza kuathiri mustakabali wa taifa letu.
Wanahabari tunapoijadili Chadema hapa hatufanyi hivyo kwa sababu ama ni wanachama wa Chadema au maadui wa chama hicho. Tunafanya hivyo tukitambua kuwa chama chochote cha siasa chenye ushawishi mkubwa kama vilivyo vyama vya CCM, Chadema na CUF hivi sasa vinapaswa kuwatumikia wananchi ipasavyo.
Kwa sababu hiyo basi, tunapomjadili Mbowe hapa au Zitto, Mnyika, John Mrema na wengine, tunawaangalia kama viongozi wa kitaifa wenye wajibu wa kuwatumikia si wanachama wao tu la hasha bali pia wananchi. Ndiyo maana hata hoja za ufisadi wa EPA, Buzwagi, Meremeta, Deep Green, Richmond, na mwingine wote ambao umekuwa ukipingwa na akina Mbowe, Slaa, Zitto, Mnyika na Mrema unagusa masuala ya nchi na si ya mtu mmoja mmoja.
Kwa sababu hiyo basi, tunapomhoji na kumbana Zitto au mwingine yeyote tunafanya hivyo lengo likiwa ni kuhakikisha Chadema na kambi ya upinzani inabakia madhubuti. Tunatambua kwa kufanya hivyo tunawakera sana mamluki na CCM yao, ambako vijana wengi (si wote) wanaangalia zaidi madaraka na matumbo yao kuliko mustakabali mwema wa nchi yao.
Ni wazi kwamba, kwa kufanya hivyo tunaweza tukawa tukifanya makosa. Ni kwa kutambua hilo, tuko tayari kukosolewa wakati wowote na huo ndiyo msingi wa kukubali kwetu kwa hiari kujiunga katika JF na kabla ya hapo tulikuwa wafuatilia wa mara kwa mara wa maandiko yake.