Nakusudia kumshtaki baba yangu

Nakusudia kumshtaki baba yangu

mzee mbona hii thread ilishaletwaga humu nakumbuka kama si mwaka juzi ni mwaka jana

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani ni huyu lakini ile thread ilikuwa ya kutafuta namna ya kuishi na baba yake vizuri pamoja na visanga alivyokuwa anaifanyia familia, naona Kama yamemshinda Sasa anataka waende mahakamani. Hakika huyo mzee inaonekana ni kisanga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo ni mjomba, Hapa unamzungumzia baba mzazi... Huwezi jua nan atakua upande wake kipind cha kufungua kesi....

Inawezekana akashinda kesi akapata hyo milion 16 ila maisha yake na familia yake baada ya hapo yasiwe the same.....

Atafute namna nyengne ya kusaidia familia yake bila kumshirikisha mzee wake... na siku nyengne vitu muhimu avihifadhi nyumbani kwake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hebu pitia comment hapo nimeona kaandika Kuna 28m + 30m +12m +24m ni pesa nyingi hizo mkuu usichukulie poa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ulipaswa kimsahau huyu dingi kitambo sana, alipowatenga wakati anakula bata hiyo ilitosha kutokuwa karibu naye tena..wazungu husema "first choice normally counts" ... Baba yako tangu awali alionesha kuwa hawajali, hivyo hastahili huruma ya kirafiki zaidi ya kumheshimu kama mzazi.
Pia unafeli kushirikisha ndugu hasa wazazi katika mali zako, hii ipo hivi.. mzazi anahesabu kuwa watoto wote ni wake, hivyo mali yako itakuwa yenu na mbaya zaidi anaweza itumia kwa nduguze au kuwekeza kwa vimada wake zaidi.
Ukimshitaki hata hao ndugu zako uliobebeshwa zigo watakuona mbaya kwani hao ni watoto wa huyo baba. Pia kaka jifunze kuwa msiri wa mali zako kama mshua wako ila lazima utambue kuwa wanao ndio warithi wako, jambo ambalo mshua wako alishindwa kutambua na kuamua kutowaamini nyote.
Mshua wako ni dhahiri kuwa ni mpenda hanasa na asiyejitambua but ingekuwa mimi ningesitisha misaada ya elimu kwa wanawe kwani hata iweje yeye ndio mzazi wao.
Ningelipa kisasi kwa style ambayo hata Mungu singeniadhibu kwakuwa singeyaacha majukumu ya baba ambayo si lazima kutekelezwa na mimi ambayo ni kutoa msaada kwa uzao na familia yake.
Kuhusu kumlipa gharama zake, hapo ningemwambia asihofu ila twende kikaandikishiane mahakamani hayo malipo, angenilipa vyote navyo mdai na nilivyowahi kumsaidia kisha naye ningemlipa na kamwe isingekuwa laana kwangu kwani yeye ndiye anayehitaji nifanye hivyo.
Mwisho... Tambua kuwa hata hao ndugu zako ni uzao wake na ng'ombe kamwe hazai chui, kuwa makini nao kaka, ipo siku utanikumbuka kaka. Wekeza kwa ajili ya wanao bila ya nduguzo kujua.
Nimepitia mengi sana kuhusu ndugu, na sasa naishi kwa rafiki Mkoa mwingine, home ni matusi na manyanyaso kisa mlo! Dharau na kejeli kisa sina kazi, but nilipokuwa na kazi nilithaminika na kuwa Mtoto but now ni Mjinga.
Nimeapa kutomuamini binadamu hata awe mzazi wangu, ninayemuamini 100% ni Mungu tu! Kwani yeye hajawahi kuniacha kamwe!
Hatma ya wanao ipo kwako kaka, thamini ndugu uje uteseke uzeeni kwa kuwaacha wanao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kaka pole sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sina neno zuri la kutumia zaidi ya kusema nimebahatika kuzaliwa na baba mpumbavu sana, mjinga na asiyejielewa, sina mantiki ya kumdharau baba yangu lakini mpaka hapa nilipofika Sina budi kusema ni mjinga na imefika hatua namchukia kwelikweli Kuna misemo mingi ya wahenga kuhusu wazazi lakini wengine ni gundu, Mimi pia ni baba wa watoto 4 lakini huyu mzazi wangu hafai kuigwa na mzazi yeyote aliye smart.

Stori ni ndefu sana hapa naifupisha kidogo, Huyu baba yangu hana maisha ya dhiki ni mtu mwenye uwezo wa kufanya chochote anachotaka pamoja ya kuwa na miradi hajawahi kuishirikisha familia na hakuna anaejua miradi yake ilipo hata Mimi pamoja na kusikia tu kwa watu sijawahi kumuuliza na wala hilo halijawahi kuwa tatzo kwangu na wadogo zangu.

Tatizo ni hili,Kuna kipindi baba yangu alifirisika alichoka sana kiuchumi, kipindi hicho Mimi nilikuwa vizuri kiuchumi baada ya kumaliza chuo wajomba zangu waliniwezesha nikawa nina miradi ambayo ilikuwa inatoa profit nzuri kipesa na kiutafutaji nilikuwa mkoa tofauti na wazazi na tulikuwa karibu sana kimawasiliano. Siku moja Baba alinipigia simu akiniomba tuongee kwa kina , yalikuwa maongezi marefu lakini kikubwa alikuwa ananiambia amefirisika na gari zote alizokuwa nazo ameuza na alihitaji msaada wangu wa kuinua uchumi wake. Ilibidi nifunge safari kurudi nyumbani kwa wazazi ili tuzungumze vizuri sikutaka kufanya maamuzi nikiwa mbali nikiwa sijui ukubwa wa tatzo.

Na hii ndio ilikuwa mara ya kwanza kuongea na baba yangu kwa kina hakuwahi kunishirikisha kwenye mambo yake yoyote yale, tulizungumza kwa kina na ilikuwa siku nzuri sana kwetu na familia kiujumla tulifika muafaka kwa ustawi wa familia na wadogo zangu ambao walikuwa bado wako shule ambao walihitaji msaada zaidi kufika malengo yao na kwa vile pesa aliyoomba ilikuwa ndani ya uwezo wangu nilimpa mara 2 ya kile alichoomba nikamnunulia na gari la kutembelea, na hapa niseme ukweli pamoja na kwamba nyumbani kulikuwa na magari baba yangu alikuwa hataki kuona watoto tunajua kuendesha lakini kwa vile mjomba alikuwa na gari na mwanae alikuwa anajua aliweza kunifundisha na nikawa najua na sikuwahi kuendesha gari la baba alikuwa haruhusu mpaka anafirisika, Sasa kulingana na ufinyu wangu wa mda kuna nyumba ilikuwa inauzwa huo mkoa anaoenda kuwekeza nikampa pesa zingine ili akamilizie kunilipia na achukue document zote kwa niaba yangu na aninunulie viwanja kadhaa ambavyo tayari nilikuwa kwenye mawasiliano na wauzaji.

Kipindi chote tukawa tunawasiliana na kumuweka karibu na wale wauzaji na nyumba na viwanja ili kuhakikisha anavinunua na kuhusu maendeleo ya miradi yake aliyofungua. Sikujua chochote ndani ya mwaka mzima mpaka pale mdogo wangu aliyekuwa anaingia kidato cha 2 na mwingine cha 4 kunipigia simu kwamba wamefukuzwa shule kwa sababu ya ada Ikabidi nishtuke kumpigia mzee kutaka kujua nini kimetokea maana moja ya makubaliano yetu ni watoto kulipiwa ada, bila matarajio alinijibu kiukali sana na kunitaka nilipe gharama zake za matunzo yangu alivyonilea, ikanibidi nianze kufuatilia kupata hati za nyumba na viwanja nilivomtuma aninunulie kufika pale kwenye nyumba na viwanja vyote vishauzwa na yeye amejenga nyumba nyingine ambayo anaishi na mwanamke mwingine na tayari Wana mtoto mzee kweli ni mhuni lakini sikutegemea atafikia kiwango hiki. Nilihisi kuchanganyikiwa, ilileta mgogoro kidogo kati yangu na yeye lakini niliradhimika kusamehe. Mzigo wa pale nyumbani watoto wa5 wote wako shule private baba yangu akawa hana mda nao tena.

Nikaingia kwenye majukumu mazito na magumu lakini mungu akanifungulia riziki kipato nilichokuwa nakipata kikawa si haba nikapambana nao mpaka wengine leo wako chuo na kuweza kujenga nyumba nzuri zaidi kwa ajili ya familia na nikafungua miradi pale nyumbani ili kuwezesha kupata pesa za matumizi madogo na kujikimu kwa familia, wakuu sikujua lengo la baba kwa kweli yaani alichukua kirikuu akasomba vitu vyote dukani mpaka leo haijulikani alipeleka wapi na mtaji wote wa biashara za mobile money transaction akachukua.

Kinachonifanya nimfungulie kesi ni hiki, nilinunua kiwanja mwaka juzi kwa 16m na yeye akiwa shahidi hati nikaiacha nyumbani kwa mama na mara kadhaa nimekuwa naisahau kuichukua mwezi January naenda kuweka uzio kwenye uwanja wangu nakuta kumeshajengwa, namuuliza aliyepo anasema ameuziwa na baba na hati anatoa ambayo niliyouziwa mimi mwanzoni kumuuliza mama anasema yeye alitunza kwenda kuangalia alipoiweka haipo, na Mimi nina familia nishachoka nitaka nimburuze mahakamani.

Kuna mda inafika kiwango cha uvumilivu kinaisha, ukisikia watu watu wanauana ni mambo Kama haya na hapa ndipo unapoona Kama Diamond hama mda na baba yake hapaswi kulaumiwa Hawa wazee wengine ni WAPUMBAVU mambo mengi nimeamua kufupisha, maana nahisi kumtwanga hata risasi huyu mke wake amerudisha nyuma sana kwenye uchumi wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtoto wa nyoka ni nyoka...
 
Mkuu hebu pitia comment hapo nimeona kaandika Kuna 28m + 30m +12m +24m ni pesa nyingi hizo mkuu usichukulie poa

Sent using Jamii Forums mobile app
Kinachonifanya nimfungulie kesi ni hiki, nilinunua kiwanja mwaka juzi kwa 16m na yeye akiwa shahidi hati nikaiacha nyumbani kwa mama na mara kadhaa nimekuwa naisahau kuichukua mwezi January naenda kuweka uzio kwenye uwanja wangu nakuta kumeshajengwa, namuuliza aliyepo anasema ameuziwa na baba na hati anatoa ambayo niliyouziwa mimi mwanzoni kumuuliza mama anasema yeye alitunza kwenda kuangalia alipoiweka haipo, na Mimi nina familia nishachoka nitaka nimburuze mahakamani.


Hayo hapo juu yalikua maelezo ya mtoa mada juu ya dhumuni la kutaka kufungua kesi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
yah

nakumbuka tulishamshauri sana mhusika original sasa nashangaa umerudi tena lakini kisa kama amekifupisha
Hapana japo anaweza kuwa ni yeye ila Kuna utofauti kidogo ile ilikuwa ni kuomba ushauri namna ya kuishi na baba pamoja na magumu anayowafanyia, hapa naona Kama yamemfika shingoni kwa hiyo sio ile kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kinachonifanya nimfungulie kesi ni hiki, nilinunua kiwanja mwaka juzi kwa 16m na yeye akiwa shahidi hati nikaiacha nyumbani kwa mama na mara kadhaa nimekuwa naisahau kuichukua mwezi January naenda kuweka uzio kwenye uwanja wangu nakuta kumeshajengwa, namuuliza aliyepo anasema ameuziwa na baba na hati anatoa ambayo niliyouziwa mimi mwanzoni kumuuliza mama anasema yeye alitunza kwenda kuangalia alipoiweka haipo, na Mimi nina familia nishachoka nitaka nimburuze mahakamani.


Hayo hapo juu yalikua maelezo ya mtoa mada juu ya dhumuni la kutaka kufungua kesi

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu huyu jamaa naamini Yuko serious alishawahi kuleta kisa kwa ID ya kuomba namna ya kuishi na baba yake baada ya kuwa anampitisha kwenye magumu mengi haya ya kumpiga pesa anaenda kujengea hawara.

Hapa naona yamemfika, ukiona hapo Kuna mlolongo wa visa kibao huko nyuma mpaka January kikauzwa kiwanja chake pesa zikaenda kufungulia mradi wa hawara wa baba yake ikiwa mama yake Hana mradi. Haya mambo ni magumu ukivaa viatu vya huyo jamaa na mzigo alioachiwa hakika hapaswi kumlaumu hata kidogo kwanza ningekuwa Mimi Aiseee sijui nasema sijui nadhani Kuna mtu angekuwa maiti now

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazee wa namna hii sio wa kutetea kabisa Kama wale baba zake DIAMOND anakutelekeza tangu utotoni ukishawin maisha ndio anajitokeza aisee Mimi nakuwa kauzu zaidi ya DIAMOND , tusitetee ujinga Kuna wazazi baadhi ni Visanga wanatelekeza familia wanahamia nyumba ndogo wanawekeza huko wakiishiwa wanafukuzwa wanarudi kwenye familia zao sasa kazi inakuwa kutoa maneno ya laana kwa watoto lakini kipindi wana nafasi na pesa hawakujali familia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu huyu jamaa naamini Yuko serious alishawahi kuleta kisa kwa ID ya kuomba namna ya kuishi na baba yake baada ya kuwa anampitisha kwenye magumu mengi haya ya kumpiga pesa anaenda kujengea hawara.

Hapa naona yamemfika, ukiona hapo Kuna mlolongo wa visa kibao huko nyuma mpaka January kikauzwa kiwanja chake pesa zikaenda kufungulia mradi wa hawara wa baba yake ikiwa mama yake Hana mradi. Haya mambo ni magumu ukivaa viatu vya huyo jamaa na mzigo alioachiwa hakika hapaswi kumlaumu hata kidogo kwanza ningekuwa Mimi Aiseee sijui nasema sijui nadhani Kuna mtu angekuwa maiti now

Sent using Jamii Forums mobile app
Yeah ni kwel amepitia mengi sana juu yake yeye na mzazi wake ila kwa stage aliyofikia ni bora akakae nae mbali zaid huku akiwahudumia hao ndugu zake wengne na Mama yake,

Maana nnachojiuliza ni kwamba anamshtak ili alipwe ama anashtaki ili kumkomoa mzee wake? But either way kwangu naona haina maana he can move on na maisha mengne bahat nzur Mungu amembariki mpka kufikia hapo alipofika so hatapungukiwa kabisaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umetoa ushauri mzuri sana mengi nakubaliana na wewe, lakini wewe unaweza kuuza Mali za mwanao na kuitelekeza familia ukaenda kumjengea na kumfungulia miradi hawara na ukabeba majukumu ya kusomesha watoto wa mwanaume mwenzio uliowakuta kwa huyo hawara wako ukawatelekeza?

Hapa ilikuwa imebaki point niende huko nikamfumue huyo mwanamke risasi naamini ndiye anayempa haya mashinikizo sio rahisi kaka ni jambo gumu sana

Sent using Jamii Forums mobile app

Jamaa punguza hasira, nenda taratibu utaishinda hiyo game..

Umeshakuwa Mwanaume mtu mzima omba Mungu amnusuru Baba yetu ufahamu umrudie..haya mambo yapo, hii michepuko ya kiAfrica ni hatari sana kwa uchawi, uchawi upo, asikudanganye mtu. Muombe Mungu akulinde umtoe mzee kwenye hicho kibano.. Hapo unakuta Mzee anapigwa mande na ukoo wa huyo Mama maana ndio vile tena mkombozi kaja, Narudia tena muombe Mungu umnusuru Mzee maana kwenye hizo harakati za kumnasua hata wewe unaweza kupigwa vita kali..

Futa hiyo kauli ya kumuita Mzee mpumbavu, mtulize bimkubwa awe mtulivu na ajikite kwenye maombi mumnusuru Mzee maana kuna binadamu mashetani asikwambie mtu. Tambua wanaume wote huwa tunachepuka na ajali kama hizo hutokea kwa kuangukia kwa mashetani yasiyo na utu...take care bro and rescue the father, he is your father and there is no foolish dad..
 
Wazee wa namna hii sio wa kutetea kabisa Kama wale baba zake DIAMOND anakutelekeza tangu utotoni ukishawin maisha ndio anajitokeza aisee Mimi nakuwa kauzu zaidi ya DIAMOND , tusitetee ujinga Kuna wazazi baadhi ni Visanga wanatelekeza familia wanahamia nyumba ndogo wanawekeza huko wakiishiwa wanafukuzwa wanarudi kwenye familia zao sasa kazi inakuwa kutoa maneno ya laana kwa watoto lakini kipindi wana nafasi na pesa hawakujali familia.

Sent using Jamii Forums mobile app

Wanaume tunapitia magumu sana.
 
Maisha ni fumbo la imani...mama pia ni tatizo...
Aliyajua hayo yote akamyuti...wewe kakuzuga...haiwezekani mtu akajenga eneo lako fununu zisifike kwenu...

Ukimpeleka baba mahakamani jua umeanzisha ugomvi na mama pia...

Pesa zinatafutwa na amani utaipata lakini kamwe siyo kwa kuwa karibu na wazazi..
Umeshakuwa umejifunza..kaa nao mbali miaka mi3, kimya utapata amani na pesa utapata na utajenga.

Kaa nao mbali, endesha maisha yako.
Achana nao kabisa, watazidi kukuvuruga..

Everyday is Saturday...................... 😎
 
Wanaume tunapitia magumu sana.
Hakika kaka, Mimi ni mchepukaji sikatai lakini linapokuja suala la familia yangu na wazazi sina mjadala na kweli wazazi wangu sio changamoto.

Lakini nina shuhuda za marafiki zangu wale wazazi wao hawapaswi kuwa wazazi ndani ya hii dunia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom