Nakusudia kumshtaki baba yangu

Nakusudia kumshtaki baba yangu

Wazazi wanawazaa, wanatafuta mali, wanawasomesha. Mali walizonazo ni kwa ajili yenu, lakini wanapokuwa hai vyote ni vya wazazi, ikiwemo wewe na mali unazodai ni zako. Mpumbavu si baba yako, bali wewe mwenyewe. Una uwezo wa kumlipa mzazi wako? Huna fadhila. Kitendo cha wewe kuzaliwa tu kinatosha kumshukuru baba yako. Huyo baba yako asingekutana na mama yako, siku hiyo na kwa wakati huo ungezaliwa wewe? Mama yako angekutana na mwanamme mwingine, angezaliwa mtu mwingine tofauti na wewe. Umewahi kujiuliza mama yako anahusikaje na tabia ya baba yako? Una mali, imekupofusha. Shukuru milango ya Jf haivunjwi na takukuru, wewe ndio ulitakiwa usimame mahakamani kueleza unakopata mali hizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sina neno zuri la kutumia zaidi ya kusema nimebahatika kuzaliwa na baba mpumbavu sana, mjinga na asiyejielewa, sina mantiki ya kumdharau baba yangu lakini mpaka hapa nilipofika Sina budi kusema ni mjinga na imefika hatua namchukia kwelikweli Kuna misemo mingi ya wahenga kuhusu wazazi lakini wengine ni gundu, Mimi pia ni baba wa watoto 4 lakini huyu mzazi wangu hafai kuigwa na mzazi yeyote aliye smart.

Stori ni ndefu sana hapa naifupisha kidogo, Huyu baba yangu hana maisha ya dhiki ni mtu mwenye uwezo wa kufanya chochote anachotaka pamoja ya kuwa na miradi hajawahi kuishirikisha familia na hakuna anaejua miradi yake ilipo hata Mimi pamoja na kusikia tu kwa watu sijawahi kumuuliza na wala hilo halijawahi kuwa tatzo kwangu na wadogo zangu.

Tatizo ni hili,Kuna kipindi baba yangu alifirisika alichoka sana kiuchumi, kipindi hicho Mimi nilikuwa vizuri kiuchumi baada ya kumaliza chuo wajomba zangu waliniwezesha nikawa nina miradi ambayo ilikuwa inatoa profit nzuri kipesa na kiutafutaji nilikuwa mkoa tofauti na wazazi na tulikuwa karibu sana kimawasiliano. Siku moja Baba alinipigia simu akiniomba tuongee kwa kina , yalikuwa maongezi marefu lakini kikubwa alikuwa ananiambia amefirisika na gari zote alizokuwa nazo ameuza na alihitaji msaada wangu wa kuinua uchumi wake. Ilibidi nifunge safari kurudi nyumbani kwa wazazi ili tuzungumze vizuri sikutaka kufanya maamuzi nikiwa mbali nikiwa sijui ukubwa wa tatzo.

Na hii ndio ilikuwa mara ya kwanza kuongea na baba yangu kwa kina hakuwahi kunishirikisha kwenye mambo yake yoyote yale, tulizungumza kwa kina na ilikuwa siku nzuri sana kwetu na familia kiujumla tulifika muafaka kwa ustawi wa familia na wadogo zangu ambao walikuwa bado wako shule ambao walihitaji msaada zaidi kufika malengo yao na kwa vile pesa aliyoomba ilikuwa ndani ya uwezo wangu nilimpa mara 2 ya kile alichoomba nikamnunulia na gari la kutembelea, na hapa niseme ukweli pamoja na kwamba nyumbani kulikuwa na magari baba yangu alikuwa hataki kuona watoto tunajua kuendesha lakini kwa vile mjomba alikuwa na gari na mwanae alikuwa anajua aliweza kunifundisha na nikawa najua na sikuwahi kuendesha gari la baba alikuwa haruhusu mpaka anafirisika, Sasa kulingana na ufinyu wangu wa mda kuna nyumba ilikuwa inauzwa huo mkoa anaoenda kuwekeza nikampa pesa zingine ili akamilizie kunilipia na achukue document zote kwa niaba yangu na aninunulie viwanja kadhaa ambavyo tayari nilikuwa kwenye mawasiliano na wauzaji.

Kipindi chote tukawa tunawasiliana na kumuweka karibu na wale wauzaji na nyumba na viwanja ili kuhakikisha anavinunua na kuhusu maendeleo ya miradi yake aliyofungua. Sikujua chochote ndani ya mwaka mzima mpaka pale mdogo wangu aliyekuwa anaingia kidato cha 2 na mwingine cha 4 kunipigia simu kwamba wamefukuzwa shule kwa sababu ya ada Ikabidi nishtuke kumpigia mzee kutaka kujua nini kimetokea maana moja ya makubaliano yetu ni watoto kulipiwa ada, bila matarajio alinijibu kiukali sana na kunitaka nilipe gharama zake za matunzo yangu alivyonilea, ikanibidi nianze kufuatilia kupata hati za nyumba na viwanja nilivomtuma aninunulie kufika pale kwenye nyumba na viwanja vyote vishauzwa na yeye amejenga nyumba nyingine ambayo anaishi na mwanamke mwingine na tayari Wana mtoto mzee kweli ni mhuni lakini sikutegemea atafikia kiwango hiki. Nilihisi kuchanganyikiwa, ilileta mgogoro kidogo kati yangu na yeye lakini niliradhimika kusamehe. Mzigo wa pale nyumbani watoto wa5 wote wako shule private baba yangu akawa hana mda nao tena.

Nikaingia kwenye majukumu mazito na magumu lakini mungu akanifungulia riziki kipato nilichokuwa nakipata kikawa si haba nikapambana nao mpaka wengine leo wako chuo na kuweza kujenga nyumba nzuri zaidi kwa ajili ya familia na nikafungua miradi pale nyumbani ili kuwezesha kupata pesa za matumizi madogo na kujikimu kwa familia, wakuu sikujua lengo la baba kwa kweli yaani alichukua kirikuu akasomba vitu vyote dukani mpaka leo haijulikani alipeleka wapi na mtaji wote wa biashara za mobile money transaction akachukua.

Kinachonifanya nimfungulie kesi ni hiki, nilinunua kiwanja mwaka juzi kwa 16m na yeye akiwa shahidi hati nikaiacha nyumbani kwa mama na mara kadhaa nimekuwa naisahau kuichukua mwezi January naenda kuweka uzio kwenye uwanja wangu nakuta kumeshajengwa, namuuliza aliyepo anasema ameuziwa na baba na hati anatoa ambayo niliyouziwa mimi mwanzoni kumuuliza mama anasema yeye alitunza kwenda kuangalia alipoiweka haipo, na Mimi nina familia nishachoka nitaka nimburuze mahakamani.

Kuna mda inafika kiwango cha uvumilivu kinaisha, ukisikia watu watu wanauana ni mambo Kama haya na hapa ndipo unapoona Kama Diamond hama mda na baba yake hapaswi kulaumiwa Hawa wazee wengine ni WAPUMBAVU mambo mengi nimeamua kufupisha, maana nahisi kumtwanga hata risasi huyu mke wake amerudisha nyuma sana kwenye uchumi wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
Usimshitaki baba yako ila usiweke uhusiano mali za nyumbani na zako. Mzee asihusike tena na chochote kinacho usiana na pesa. Wazee wana majaribu kinoma.
 
Wazazi wanawazaa, wanatafuta mali, wanawasomesha. Mali walizonazo ni kwa ajili yenu, lakini wanapokuwa hai vyote ni vya wazazi, ikiwemo wewe na mali unazodai ni zako. Mpumbavu si baba yako, bali wewe mwenyewe. Una uwezo wa kumlipa mzazi wako? Huna fadhila. Kitendo cha wewe kuzaliwa tu kinatosha kumshukuru baba yako. Huyo baba yako asingekutana na mama yako, siku hiyo na kwa wakati huo ungezaliwa wewe? Mama yako angekutana na mwanamme mwingine, angezaliwa mtu mwingine tofauti na wewe. Umewahi kujiuliza mama yako anahusikaje na tabia ya baba yako? Una mali, imekupofusha. Shukuru milango ya Jf haivunjwi na takukuru, wewe ndio ulitakiwa usimame mahakamani kueleza unakopata mali hizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na wewe ni zaidi ya MPUMBAVU.
Halafu unadhani Mimi fisadi mpaka nitafutwe na TAKUKURU au unadhani kazi zangu nafanyia mbinguni kwamba sijulikani MJINGA wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila loopholes kibao ulizitengeneza mwenyewe ili mzee akupige.

Mtu unayemuamini ana nafasi moja tu ya "kukupiga" ikitokea upigaji ukajirudia tena basi it's your fault.
 
Mkuu siku zote hasira huenda isitende haki. Kuna jambo la kufanya, najua nia yako ni kumkomoa ila hautaweza kumkomoa kwa pigo la kumpeleka ktk vyombo vya sheria.

Una pesa za kuendesha maisha yako si ndivyo? Mpaka sasa unavyoona pasipo hivyo viwanja kuna kitu ambacho kimeharibu maisha yako? Utaingia mgogoro na Mzee ila kiuhalisia familia nzima itatikisika ktk hili.

Utamfunga ila watakuja wengi wakikwambia ulotenda ni kubwa, either jamii, ndugu ama marafiki. Ishu za mtoto na mzazi ni ngumu. Ni wewe ndie unayesikia uchungu, wao hawafeel vile ambavyo wewe unafeel. Sio ajabu kwao kuja kukwambia umekosea kumpeleka vyombo vya sheria.

Mimi nnachokushauri ni hiki, achana na mzee. Ikiwezekana kata naye mawasiliano kabisa. Hizo fedha zitatumika mwisho kabisa zitaisha. Mzee atakumbuka fadhila za nyuma zote alizotendewa, na hapo ndipo atakapomkumbuka mkewe wa kwanza na msaada wako.

Hatoweza kufanya lolote zaidi ya moyo wake kumuhukumu, ogopa saana moyo wako ujihukuku kwa mabaya uliyomfanyia mtu, hata usingizi huwezi ukaupata kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umemshauri vyema. Atakayoyafanya kwa baba yake yataonwa na jamii yote inayomzunguka, wakiwemo watoto wake. Penye hasira, kiwango cha utu huwa sifuri na kutenda lolote sawa na mnyama. Baadae ndio majuto. Kuna shinikizo kubwa kutoka kwa mkewe, ambaye Leo anamwona mshauri mzuri. Akumbuke inaweza tokea siku moja title ikabadirika na kuwa ' huyo alikuwa mkewe', lakini haitatokea akasema yule alikuwa baba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazazi wanawazaa, wanatafuta mali, wanawasomesha. Mali walizonazo ni kwa ajili yenu, lakini wanapokuwa hai vyote ni vya wazazi, ikiwemo wewe na mali unazodai ni zako. Mpumbavu si baba yako, bali wewe mwenyewe. Una uwezo wa kumlipa mzazi wako? Huna fadhila. Kitendo cha wewe kuzaliwa tu kinatosha kumshukuru baba yako. Huyo baba yako asingekutana na mama yako, siku hiyo na kwa wakati huo ungezaliwa wewe? Mama yako angekutana na mwanamme mwingine, angezaliwa mtu mwingine tofauti na wewe. Umewahi kujiuliza mama yako anahusikaje na tabia ya baba yako? Una mali, imekupofusha. Shukuru milango ya Jf haivunjwi na takukuru, wewe ndio ulitakiwa usimame mahakamani kueleza unakopata mali hizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huu ndio ukweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa ambao hamjawahi kuletewa mapichapicha na wazee wenu mnaweza chukulia poa. Mimi ni mmoja wa wahanga nakushauri mkuu shtaki hilo zee huna kosa wala laana yeyote hapo.
 
Mkuu kwanza samahani Kama nimetumia lugha ngumu lakini jaribu kujiweka kwenye viatu vyangu Kuna mambo mengi sijaweka hapa, just imagine nilimpa 28m kuboost miradi yake, 30m ili amalizie kulipa malipo ya nyumba yangu, na 12m aninunulie viwanja alinunua kweli lakini Baadae akauza akajenga nyumba ambayo amemkabidhi kimada wake ambae amemkuta na watoto wawili wakubwa wako secondary anawasomesha yeye kwa mchango wa jasho langu ikiwa wanae/wadogo zangu Hana mpango nao tena.

Halafu ameuza tena kiwanja changu kwa 24m bila aibu ameenda kumfungulia miradi mingine huyo kimada wake wakati mama yangu aliyehangaika na Mimi Hana mradi huyu mzee ni MPUMBAVU acha tu nimuite hivo

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana mkuu.

Nimekuelewa vema tena sana japo ni ngumu kujua maumivu katika hisia zako dhidi ya baba.

Baba amekukosea sana, na una sababu za kumwita na kukusudia lolote dhidi yake.

Nakushauri tu, kuwa makini, mudu hisia ili uweze kukabili uyapangayo kwa usahihi tena bila hasira.

Kwa sababu imeshatokea, kisheria utamshinda vizuri tu, lakini kisaikolojia n.k inaweza kukuathiri (ndio maana nakwambia, jimudu, mudu hasira nanhisia pia).

Tuko pamoja mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu ambao tunajua wazee wetu kichwani ni mapapai huwa tuko smart sana kukaa nao. Wewe ulishindwa fanya hivyo, mimi mzee wangu naamini anaweza kabisa nitoa kafara. Huwa siendi kwake na kuanzia mwaka huu sitaki kukutana nae tena.
 
Mkuu ulifanya kosa kutomsoma mapema, wazee wengi ngozi nyeusi ni vimeo na wanajiona wana haki sana kupata misaada kutoka kwa watoto wao, ndo maana anakupiga mkwara kuhusu matunzo aliyotumia kukulea utafikiri ulimwomba akuzae....
 
Hakuna Baba mpumbavu, weka kwenye akili yako hilo...ipo shida mahala kwa Mzee wako lakini sio mpumbavu..

Kwa wakati huu, jitahidi kumlea Mama na wadogo zako kwa maana ya future ya wadogo zako kadili Mungu atakavyokubaliki. Jitahidi Baba yako ale vizuri, atibiwe akiumwa, avae vizuri na akifa mzike kwa heshima..

Kila mali inayohusu jasho lako hakikisha unaisimamia mwenyewe na kutunza documents zako mwenyewe, usimhusishe Mzee wala mama kwenye documents zako.. Kama wadogo zako wanadiscipline kidogo kidogo waingize kwenye mitikasi yako..

Achana na biashara ya kumfungulia kesi samehe kwa sasa hilo... Fanya uchunguzi kama amezaa na huyo mama aka mchepuko wake, kama hakuzaa naye jaribu kufanya uchunguzi wa hiyo nyumba documents zake ikiwezekana uziteke uwe nazo halafu tafuta namna Mzee achomwe sindano ya uzazi asizae tena..

Ikishindikana hapo juu, fungueni kesi Mzee wenu hayuko sawa kiakili na huyo mama anatake hiyo advantage ili kumfirisi Baba yenu na asset za familia hapo umiliki wa mali zote na asset na documents zote zinakuja kwenu...
 
Watu ambao tunajua wazee wetu kichwani ni mapapai huwa tuko smart sana kukaa nao. Wewe ulishindwa fanya hivyo, mimi mzee wangu naamini anaweza kabisa nitoa kafara. Huwa siendi kwake na kuanzia mwaka huu sitaki kukutana nae tena.
Wengine unakuta kaoa kazaa na watoto wadogo, anataka akuendeshe umpe pesa kibabe bila kujali na wewe una maisha yako na anakuongelea mbovu kila mahali, na mkeo atasemwa kakukamata kwamba ni mchawi....kuna wazee ni vichwa maji kinoma..
 
Umemshauri vyema. Atakayoyafanya kwa baba yake yataonwa na jamii yote inayomzunguka, wakiwemo watoto wake. Penye hasira, kiwango cha utu huwa sifuri na kutenda lolote sawa na mnyama. Baadae ndio majuto. Kuna shinikizo kubwa kutoka kwa mkewe, ambaye Leo anamwona mshauri mzuri. Akumbuke inaweza tokea siku moja title ikabadirika na kuwa ' huyo alikuwa mkewe', lakini haitatokea akasema yule alikuwa baba.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi wewe uko sawasawa kweli habari za mke zinakujaje hapa? Unadhani naendeshwa na mke

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom