Nakusudia kumshtaki baba yangu

Nakusudia kumshtaki baba yangu

Ni kweli baba yako ni mpumbavu.

Ingawa na wewe pia umefanya upumbavu.

Kuumwa na nyoka mara mbili kwenye eneo lile lile ni upumbavu.

Binafsi baba hakunilea wala sikumjua mpaka nahitimu kidato cha sita. Kwa kuwa hakunilea kabisa nilidhani labda baada ya kukutana sasa atachukua majukumu yake kumbe bado mpuuzi tu.

Nikamwambia tu kama vile ambavyo hatukuwa na ukaribu zamani, tuendelee vivyo hivyo kiroho safi.

Usiweke ukaribu na JOKA ukidhani ipo siku litabadilika na kuwa samaki.
Wewe kama Mimi kabisa Mzee wangu akunisomesha saivi tunaongea fresh Ila nimejifunza mtu kama alikutenga udogoni mwako au alikujeruhi Kwa chochote aiseee usiweke uwaminifu tena kwake Mimi nikwambie tu mtoa mada pole Ila timiza wajibu wako Kwa mama yako na wadogo zako Baba yako uje kumsaidia akiumwa Tu tofauti na hapo usijiweke kwake tena Ila iyoo million 16 kadai haki yako mahakamni kivyovyote mkuu nyingine samehe Ila iyoo hapana na jifunze pia wadogo zako si wakuwaaamini pia wawezeshe kivyao wasijiingize kwenye biashara zako utalia zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
umemlea Lea sana ndio maana anathubutu kukuchezea.

Mzee wangu niliwahi kumuambia siku akiingilia maisha yangu nitamkata kichwa mchana kweupe. Alibaki ameduwaa huku ndugu wengine wakiwa hawaamini.

Tokea siku hiyo hakuna usumbufu na maisha yanasonga.

Dunia iendeshe utakavyo sio MTU Fulani atakavyo
 
acha ku generalize mambo mkuu, watu watakudharau sana
Wamachame utawajua tu! atakaye mdharau huyo aliye generalise ni mjinga. sababu amekataa hint; hao si watu!
 
Sina neno zuri la kutumia zaidi ya kusema nimebahatika kuzaliwa na baba mpumbavu sana, mjinga na asiyejielewa, sina mantiki ya kumdharau baba yangu lakini mpaka hapa nilipofika Sina budi kusema ni mjinga na imefika hatua namchukia kwelikweli Kuna misemo mingi ya wahenga kuhusu wazazi lakini wengine ni gundu, Mimi pia ni baba wa watoto 4 lakini huyu mzazi wangu hafai kuigwa na mzazi yeyote aliye smart.

Stori ni ndefu sana hapa naifupisha kidogo, Huyu baba yangu hana maisha ya dhiki ni mtu mwenye uwezo wa kufanya chochote anachotaka pamoja ya kuwa na miradi hajawahi kuishirikisha familia na hakuna anaejua miradi yake ilipo hata Mimi pamoja na kusikia tu kwa watu sijawahi kumuuliza na wala hilo halijawahi kuwa tatzo kwangu na wadogo zangu.

Tatizo ni hili,Kuna kipindi baba yangu alifirisika alichoka sana kiuchumi, kipindi hicho Mimi nilikuwa vizuri kiuchumi baada ya kumaliza chuo wajomba zangu waliniwezesha nikawa nina miradi ambayo ilikuwa inatoa profit nzuri kipesa na kiutafutaji nilikuwa mkoa tofauti na wazazi na tulikuwa karibu sana kimawasiliano. Siku moja Baba alinipigia simu akiniomba tuongee kwa kina , yalikuwa maongezi marefu lakini kikubwa alikuwa ananiambia amefirisika na gari zote alizokuwa nazo ameuza na alihitaji msaada wangu wa kuinua uchumi wake. Ilibidi nifunge safari kurudi nyumbani kwa wazazi ili tuzungumze vizuri sikutaka kufanya maamuzi nikiwa mbali nikiwa sijui ukubwa wa tatzo.

Na hii ndio ilikuwa mara ya kwanza kuongea na baba yangu kwa kina hakuwahi kunishirikisha kwenye mambo yake yoyote yale, tulizungumza kwa kina na ilikuwa siku nzuri sana kwetu na familia kiujumla tulifika muafaka kwa ustawi wa familia na wadogo zangu ambao walikuwa bado wako shule ambao walihitaji msaada zaidi kufika malengo yao na kwa vile pesa aliyoomba ilikuwa ndani ya uwezo wangu nilimpa mara 2 ya kile alichoomba nikamnunulia na gari la kutembelea, na hapa niseme ukweli pamoja na kwamba nyumbani kulikuwa na magari baba yangu alikuwa hataki kuona watoto tunajua kuendesha lakini kwa vile mjomba alikuwa na gari na mwanae alikuwa anajua aliweza kunifundisha na nikawa najua na sikuwahi kuendesha gari la baba alikuwa haruhusu mpaka anafirisika, Sasa kulingana na ufinyu wangu wa mda kuna nyumba ilikuwa inauzwa huo mkoa anaoenda kuwekeza nikampa pesa zingine ili akamilizie kunilipia na achukue document zote kwa niaba yangu na aninunulie viwanja kadhaa ambavyo tayari nilikuwa kwenye mawasiliano na wauzaji.

Kipindi chote tukawa tunawasiliana na kumuweka karibu na wale wauzaji na nyumba na viwanja ili kuhakikisha anavinunua na kuhusu maendeleo ya miradi yake aliyofungua. Sikujua chochote ndani ya mwaka mzima mpaka pale mdogo wangu aliyekuwa anaingia kidato cha 2 na mwingine cha 4 kunipigia simu kwamba wamefukuzwa shule kwa sababu ya ada Ikabidi nishtuke kumpigia mzee kutaka kujua nini kimetokea maana moja ya makubaliano yetu ni watoto kulipiwa ada, bila matarajio alinijibu kiukali sana na kunitaka nilipe gharama zake za matunzo yangu alivyonilea, ikanibidi nianze kufuatilia kupata hati za nyumba na viwanja nilivomtuma aninunulie kufika pale kwenye nyumba na viwanja vyote vishauzwa na yeye amejenga nyumba nyingine ambayo anaishi na mwanamke mwingine na tayari Wana mtoto mzee kweli ni mhuni lakini sikutegemea atafikia kiwango hiki. Nilihisi kuchanganyikiwa, ilileta mgogoro kidogo kati yangu na yeye lakini niliradhimika kusamehe. Mzigo wa pale nyumbani watoto wa5 wote wako shule private baba yangu akawa hana mda nao tena.

Nikaingia kwenye majukumu mazito na magumu lakini mungu akanifungulia riziki kipato nilichokuwa nakipata kikawa si haba nikapambana nao mpaka wengine leo wako chuo na kuweza kujenga nyumba nzuri zaidi kwa ajili ya familia na nikafungua miradi pale nyumbani ili kuwezesha kupata pesa za matumizi madogo na kujikimu kwa familia, wakuu sikujua lengo la baba kwa kweli yaani alichukua kirikuu akasomba vitu vyote dukani mpaka leo haijulikani alipeleka wapi na mtaji wote wa biashara za mobile money transaction akachukua.

Kinachonifanya nimfungulie kesi ni hiki, nilinunua kiwanja mwaka juzi kwa 16m na yeye akiwa shahidi hati nikaiacha nyumbani kwa mama na mara kadhaa nimekuwa naisahau kuichukua mwezi January naenda kuweka uzio kwenye uwanja wangu nakuta kumeshajengwa, namuuliza aliyepo anasema ameuziwa na baba na hati anatoa ambayo niliyouziwa mimi mwanzoni kumuuliza mama anasema yeye alitunza kwenda kuangalia alipoiweka haipo, na Mimi nina familia nishachoka nitaka nimburuze mahakamani.

Kuna mda inafika kiwango cha uvumilivu kinaisha, ukisikia watu watu wanauana ni mambo Kama haya na hapa ndipo unapoona Kama Diamond hama mda na baba yake hapaswi kulaumiwa Hawa wazee wengine ni WAPUMBAVU mambo mengi nimeamua kufupisha, maana nahisi kumtwanga hata risasi huyu mke wake amerudisha nyuma sana kwenye uchumi wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu ushauri tu wa bure.
Achana naye huyo mzee atakufifisha nyota yako ambayo Mungu amekujalia.
Tafuta tu sehemu nyingine, fanya biashara yako -na unaonekana una mkono mzuri tu.
Kikubwa cha kumshukuru Mungu ni uhai wako.
 
Hivi wewe uko sawasawa kweli habari za mke zinakujaje hapa? Unadhani naendeshwa na mke

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nimeipata picha kamili kukuhusu wewe, na kwa sasa umeyumbishwa akili hata ya huyo babako unae mwita mpumbavu Ina nafuu. Kwenye ndoa ambapo mke ni mshauri mzuri, usingefikia level ya kuchanganyikiwa uliopo. Tafuta ushauri nasaha, u can even kill.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom