Nakusudia kumshtaki baba yangu

Nakusudia kumshtaki baba yangu

Pole sana mkuu.

Nimekuelewa vema tena sana japo ni ngumu kujua maumivu katika hisia zako dhidi ya baba.

Baba amekukosea sana, na una sababu za kumwita na kukusudia lolote dhidi yake.

Nakushauri tu, kuwa makini, mudu hisia ili uweze kukabili uyapangayo kwa usahihi tena bila hasira.

Kwa sababu imeshatokea, kisheria utamshinda vizuri tu, lakini kisaikolojia n.k inaweza kukuathiri (ndio maana nakwambia, jimudu, mudu hasira nanhisia pia).

Tuko pamoja mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu umeongea vizuri sana, lakini ukijaribu kuvaa viatu hakika inaumiza yaani baba yako anauza Mali zako anaenda kumtajilisha hawara na kulea watoto wa mwanaume mwenzake huku mzigo wa familia yake akiwa hautambui ni bora angetumia pesa zake nisingekuwa na tatizo nae

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna Baba mpumbavu, weka kwenye akili yako hilo...ipo shida mahala kwa Mzee wako lakini sio mpumbavu..

Kwa wakati huu, jitahidi kumlea Mama na wadogo zako kwa maana ya future ya wadogo zako kadili Mungu atakavyokubaliki. Jitahidi Baba yako ale vizuri, atibiwe akiumwa, avae vizuri na akifa mzike kwa heshima..

Kila mali inayohusu jasho lako hakikisha unaisimamia mwenyewe na kutunza documents zako mwenyewe, usimhusishe Mzee wala mama kwenye documents zako.. Kama wadogo zako wanadiscipline kidogo kidogo waingize kwenye mitikasi yako..

Achana na biashara ya kumfungulia kesi samehe kwa sasa hilo... Fanya uchunguzi kama amezaa na huyo mama aka mchepuko wake, kama hakuzaa naye jaribu kufanya uchunguzi wa hiyo nyumba documents zake ikiwezekana uziteke uwe nazo halafu tafuta namna Mzee achomwe sindano ya uzazi asizae tena..

Ikishindikana hapo juu, fungueni kesi Mzee wenu hayuko sawa kiakili na huyo mama anatake hiyo advantage ili kumfirisi Baba yenu na asset za familia hapo umiliki wa mali zote na asset na documents zote zinakuja kwenu...
Mkuu umetoa ushauri mzuri sana mengi nakubaliana na wewe, lakini wewe unaweza kuuza Mali za mwanao na kuitelekeza familia ukaenda kumjengea na kumfungulia miradi hawara na ukabeba majukumu ya kusomesha watoto wa mwanaume mwenzio uliowakuta kwa huyo hawara wako ukawatelekeza?

Hapa ilikuwa imebaki point niende huko nikamfumue huyo mwanamke risasi naamini ndiye anayempa haya mashinikizo sio rahisi kaka ni jambo gumu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
aya mambo yapo maana nna uncle wangu anatabia kama za mzee wako, ndugu na familia haina mda nae now ameishia kutishia watoto wake kutaka kuwaachia laana.
 
Sina neno zuri la kutumia zaidi ya kusema nimebahatika kuzaliwa na baba mpumbavu sana, mjinga na asiyejielewa, sina mantiki ya kumdharau baba yangu lakini mpaka hapa nilipofika Sina budi kusema ni mjinga na imefika hatua namchukia kwelikweli Kuna misemo mingi ya wahenga kuhusu wazazi lakini wengine ni gundu, Mimi pia ni baba wa watoto 4 lakini huyu mzazi wangu hafai kuigwa na mzazi yeyote aliye smart.

Stori ni ndefu sana hapa naifupisha kidogo, Huyu baba yangu hana maisha ya dhiki ni mtu mwenye uwezo wa kufanya chochote anachotaka pamoja ya kuwa na miradi hajawahi kuishirikisha familia na hakuna anaejua miradi yake ilipo hata Mimi pamoja na kusikia tu kwa watu sijawahi kumuuliza na wala hilo halijawahi kuwa tatzo kwangu na wadogo zangu.

Tatizo ni hili,Kuna kipindi baba yangu alifirisika alichoka sana kiuchumi, kipindi hicho Mimi nilikuwa vizuri kiuchumi baada ya kumaliza chuo wajomba zangu waliniwezesha nikawa nina miradi ambayo ilikuwa inatoa profit nzuri kipesa na kiutafutaji nilikuwa mkoa tofauti na wazazi na tulikuwa karibu sana kimawasiliano. Siku moja Baba alinipigia simu akiniomba tuongee kwa kina , yalikuwa maongezi marefu lakini kikubwa alikuwa ananiambia amefirisika na gari zote alizokuwa nazo ameuza na alihitaji msaada wangu wa kuinua uchumi wake. Ilibidi nifunge safari kurudi nyumbani kwa wazazi ili tuzungumze vizuri sikutaka kufanya maamuzi nikiwa mbali nikiwa sijui ukubwa wa tatzo.

Na hii ndio ilikuwa mara ya kwanza kuongea na baba yangu kwa kina hakuwahi kunishirikisha kwenye mambo yake yoyote yale, tulizungumza kwa kina na ilikuwa siku nzuri sana kwetu na familia kiujumla tulifika muafaka kwa ustawi wa familia na wadogo zangu ambao walikuwa bado wako shule ambao walihitaji msaada zaidi kufika malengo yao na kwa vile pesa aliyoomba ilikuwa ndani ya uwezo wangu nilimpa mara 2 ya kile alichoomba nikamnunulia na gari la kutembelea, na hapa niseme ukweli pamoja na kwamba nyumbani kulikuwa na magari baba yangu alikuwa hataki kuona watoto tunajua kuendesha lakini kwa vile mjomba alikuwa na gari na mwanae alikuwa anajua aliweza kunifundisha na nikawa najua na sikuwahi kuendesha gari la baba alikuwa haruhusu mpaka anafirisika, Sasa kulingana na ufinyu wangu wa mda kuna nyumba ilikuwa inauzwa huo mkoa anaoenda kuwekeza nikampa pesa zingine ili akamilizie kunilipia na achukue document zote kwa niaba yangu na aninunulie viwanja kadhaa ambavyo tayari nilikuwa kwenye mawasiliano na wauzaji.

Kipindi chote tukawa tunawasiliana na kumuweka karibu na wale wauzaji na nyumba na viwanja ili kuhakikisha anavinunua na kuhusu maendeleo ya miradi yake aliyofungua. Sikujua chochote ndani ya mwaka mzima mpaka pale mdogo wangu aliyekuwa anaingia kidato cha 2 na mwingine cha 4 kunipigia simu kwamba wamefukuzwa shule kwa sababu ya ada Ikabidi nishtuke kumpigia mzee kutaka kujua nini kimetokea maana moja ya makubaliano yetu ni watoto kulipiwa ada, bila matarajio alinijibu kiukali sana na kunitaka nilipe gharama zake za matunzo yangu alivyonilea, ikanibidi nianze kufuatilia kupata hati za nyumba na viwanja nilivomtuma aninunulie kufika pale kwenye nyumba na viwanja vyote vishauzwa na yeye amejenga nyumba nyingine ambayo anaishi na mwanamke mwingine na tayari Wana mtoto mzee kweli ni mhuni lakini sikutegemea atafikia kiwango hiki. Nilihisi kuchanganyikiwa, ilileta mgogoro kidogo kati yangu na yeye lakini niliradhimika kusamehe. Mzigo wa pale nyumbani watoto wa5 wote wako shule private baba yangu akawa hana mda nao tena.

Nikaingia kwenye majukumu mazito na magumu lakini mungu akanifungulia riziki kipato nilichokuwa nakipata kikawa si haba nikapambana nao mpaka wengine leo wako chuo na kuweza kujenga nyumba nzuri zaidi kwa ajili ya familia na nikafungua miradi pale nyumbani ili kuwezesha kupata pesa za matumizi madogo na kujikimu kwa familia, wakuu sikujua lengo la baba kwa kweli yaani alichukua kirikuu akasomba vitu vyote dukani mpaka leo haijulikani alipeleka wapi na mtaji wote wa biashara za mobile money transaction akachukua.

Kinachonifanya nimfungulie kesi ni hiki, nilinunua kiwanja mwaka juzi kwa 16m na yeye akiwa shahidi hati nikaiacha nyumbani kwa mama na mara kadhaa nimekuwa naisahau kuichukua mwezi January naenda kuweka uzio kwenye uwanja wangu nakuta kumeshajengwa, namuuliza aliyepo anasema ameuziwa na baba na hati anatoa ambayo niliyouziwa mimi mwanzoni kumuuliza mama anasema yeye alitunza kwenda kuangalia alipoiweka haipo, na Mimi nina familia nishachoka nitaka nimburuze mahakamani.

Kuna mda inafika kiwango cha uvumilivu kinaisha, ukisikia watu watu wanauana ni mambo Kama haya na hapa ndipo unapoona Kama Diamond hama mda na baba yake hapaswi kulaumiwa Hawa wazee wengine ni WAPUMBAVU mambo mengi nimeamua kufupisha, maana nahisi kumtwanga hata risasi huyu mke wake amerudisha nyuma sana kwenye uchumi wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
huu uzi ulishakuwepo humu kipindi cha nyuma au nimeufananisha...
 
Baba yako muheshimu kumbuka hafanyi hayo kwa nguvu yake Bali NI huyo ibilisi aliyeambatananaye tena unapaswa umuhurumie Mana ana Hali ngumu kwa huyo mwanamke. Muombee atoke kwenye HICHO kifungo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ulipaswa kimsahau huyu dingi kitambo sana, alipowatenga wakati anakula bata hiyo ilitosha kutokuwa karibu naye tena..wazungu husema "first choice normally counts" ... Baba yako tangu awali alionesha kuwa hawajali, hivyo hastahili huruma ya kirafiki zaidi ya kumheshimu kama mzazi.
Pia unafeli kushirikisha ndugu hasa wazazi katika mali zako, hii ipo hivi.. mzazi anahesabu kuwa watoto wote ni wake, hivyo mali yako itakuwa yenu na mbaya zaidi anaweza itumia kwa nduguze au kuwekeza kwa vimada wake zaidi.
Ukimshitaki hata hao ndugu zako uliobebeshwa zigo watakuona mbaya kwani hao ni watoto wa huyo baba. Pia kaka jifunze kuwa msiri wa mali zako kama mshua wako ila lazima utambue kuwa wanao ndio warithi wako, jambo ambalo mshua wako alishindwa kutambua na kuamua kutowaamini nyote.
Mshua wako ni dhahiri kuwa ni mpenda hanasa na asiyejitambua but ingekuwa mimi ningesitisha misaada ya elimu kwa wanawe kwani hata iweje yeye ndio mzazi wao.
Ningelipa kisasi kwa style ambayo hata Mungu singeniadhibu kwakuwa singeyaacha majukumu ya baba ambayo si lazima kutekelezwa na mimi ambayo ni kutoa msaada kwa uzao na familia yake.
Kuhusu kumlipa gharama zake, hapo ningemwambia asihofu ila twende kikaandikishiane mahakamani hayo malipo, angenilipa vyote navyo mdai na nilivyowahi kumsaidia kisha naye ningemlipa na kamwe isingekuwa laana kwangu kwani yeye ndiye anayehitaji nifanye hivyo.
Mwisho... Tambua kuwa hata hao ndugu zako ni uzao wake na ng'ombe kamwe hazai chui, kuwa makini nao kaka, ipo siku utanikumbuka kaka. Wekeza kwa ajili ya wanao bila ya nduguzo kujua.
Nimepitia mengi sana kuhusu ndugu, na sasa naishi kwa rafiki Mkoa mwingine, home ni matusi na manyanyaso kisa mlo! Dharau na kejeli kisa sina kazi, but nilipokuwa na kazi nilithaminika na kuwa Mtoto but now ni Mjinga.
Nimeapa kutomuamini binadamu hata awe mzazi wangu, ninayemuamini 100% ni Mungu tu! Kwani yeye hajawahi kuniacha kamwe!
Hatma ya wanao ipo kwako kaka, thamini ndugu uje uteseke uzeeni kwa kuwaacha wanao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa ndgu siwezi kuwa mpumbavu namna hii, katelekeza familia miaka zaidi ya 6 nahangaika kusomesha watoto wake bado kuna mengi nimesahe yeye ameenda kuchukua mwanamke ana watoto wakubwa wa wanaume wenzake kamjengea nyumba nzuri kwa jasho langu na miradi huku wanae, nimuache Mali zangu zifaidishe ukoo mwingine huku wadogo zangu wanateseka

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ni hivi kamshtaki tu

Inauma sana umeeongea kwa uchungu, first born tunabeba misalaba mingi.
Kama itakupendeza naomba ufate ushauri huu, achana na kumpeleka Mzee mahakamani, hiyo kesi ina mrorongo naongea kwa experience najua uendeshaji wa kesi kama yako, utashinda ila baada ya kuumia na kupoteza muda mrefu, na usumbufu wote ni kwa sababu unamstaki baba yako.Mzee wako ni mtata, mizengwe mingi itaibuka hati feki zitatafutwa atahakikisha anaisumbua mahakama, ushahidi kwako utakuwa ni kikwazo,utatoa pesa kwa wanasheria, yaani itakuwa vurugu tupu.

Hivi unajua ni kiasi gani kesi inarudisha maendeleo nyuma? Kwani mil 16 kitu gani ukilinganisha na yote uliyoyafanya?

Kuanzia leo kata misaada yote nyumbani kwenu kasoro matumizi ya mama yako na ada za wanafunzi. Vingine vyote achaaa, umefanya vya kutosha, kata mawasiliano na baba kwa muda, jifanye kama humjui.

Nguvu ambazo unataka kuzitumia mahakamani anza kujijenga upya, kaka una familiya yako kwa nini ununue viwanja hati uweke kwenu? Mpe mkeo mtunze nyaraka zenu.

Umejifunza vya kutosha piga moyo konde, anza upya ndani ya miaka 3 utasahau, baba dunia itamfunza.
Tenda mema nenda zako utalipwa na Mungu, mema yako watu wa naona na jamii inaona yote uliyofanya.

Pole sana.
 
Umemshauri vyema. Atakayoyafanya kwa baba yake yataonwa na jamii yote inayomzunguka, wakiwemo watoto wake. Penye hasira, kiwango cha utu huwa sifuri na kutenda lolote sawa na mnyama. Baadae ndio majuto. Kuna shinikizo kubwa kutoka kwa mkewe, ambaye Leo anamwona mshauri mzuri. Akumbuke inaweza tokea siku moja title ikabadirika na kuwa ' huyo alikuwa mkewe', lakini haitatokea akasema yule alikuwa baba.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni sahihi kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya kujua Id ya mzee wangu humu JF,
Ni mwendo wa kum-quote na kumbishia tu kwenye nyuzi zake.
Btw, na enjoy sana anavyoniita mkuu!
 
Umeongea kwa uchungu sana, Hawa wazee kuna wengine wanafeli sana...

Naomba nikushauri kitu hata mkienda mahakaman nna uhakika hakuna kitu ambacho utarudishiwa kwa namna yoyote ile zaidi ya kupoteza muda
ila kama unao muda wa kufatilia kesi za madai fanya.

Umesema wadogo zako wengine wapo chuo anza kuwaingiza kwenye miradi yako kama ambavyo wajomba zako walikufunza wewe.

Anzisha mradi ambao utakua unalisha familia na kusomesha ambao bado wanahitaji kusomeshwa inaweza isiwe ule mkoa ambako mzee wako yupo au kama huko bas shirikiana na wadogo zako ambao wapo pale bila mzee wako kufaham chochote.

Ushajishusha kwa mzee wako imetosha chakufanya sasa badilisha namna ya kusaidia hao waliobakia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Akienda kumshtaki atapata haki yake, mjomba wangu aliwahi kuuza kiwanja changu, niliweka undugu pembeni, nikamsweka rumande, baadae akapelekwa gerezani, then mahakamani, ushahidi wote ulikuwepo, kiwanja changu kilirudi, ndugu zake walijicommit mahakamani kumlipa yule mnunuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sina neno zuri la kutumia zaidi ya kusema nimebahatika kuzaliwa na baba mpumbavu sana, mjinga na asiyejielewa, sina mantiki ya kumdharau baba yangu lakini mpaka hapa nilipofika Sina budi kusema ni mjinga na imefika hatua namchukia kwelikweli Kuna misemo mingi ya wahenga kuhusu wazazi lakini wengine ni gundu, Mimi pia ni baba wa watoto 4 lakini huyu mzazi wangu hafai kuigwa na mzazi yeyote aliye smart.

Stori ni ndefu sana hapa naifupisha kidogo, Huyu baba yangu hana maisha ya dhiki ni mtu mwenye uwezo wa kufanya chochote anachotaka pamoja ya kuwa na miradi hajawahi kuishirikisha familia na hakuna anaejua miradi yake ilipo hata Mimi pamoja na kusikia tu kwa watu sijawahi kumuuliza na wala hilo halijawahi kuwa tatzo kwangu na wadogo zangu.

Tatizo ni hili,Kuna kipindi baba yangu alifirisika alichoka sana kiuchumi, kipindi hicho Mimi nilikuwa vizuri kiuchumi baada ya kumaliza chuo wajomba zangu waliniwezesha nikawa nina miradi ambayo ilikuwa inatoa profit nzuri kipesa na kiutafutaji nilikuwa mkoa tofauti na wazazi na tulikuwa karibu sana kimawasiliano. Siku moja Baba alinipigia simu akiniomba tuongee kwa kina , yalikuwa maongezi marefu lakini kikubwa alikuwa ananiambia amefirisika na gari zote alizokuwa nazo ameuza na alihitaji msaada wangu wa kuinua uchumi wake. Ilibidi nifunge safari kurudi nyumbani kwa wazazi ili tuzungumze vizuri sikutaka kufanya maamuzi nikiwa mbali nikiwa sijui ukubwa wa tatzo.

Na hii ndio ilikuwa mara ya kwanza kuongea na baba yangu kwa kina hakuwahi kunishirikisha kwenye mambo yake yoyote yale, tulizungumza kwa kina na ilikuwa siku nzuri sana kwetu na familia kiujumla tulifika muafaka kwa ustawi wa familia na wadogo zangu ambao walikuwa bado wako shule ambao walihitaji msaada zaidi kufika malengo yao na kwa vile pesa aliyoomba ilikuwa ndani ya uwezo wangu nilimpa mara 2 ya kile alichoomba nikamnunulia na gari la kutembelea, na hapa niseme ukweli pamoja na kwamba nyumbani kulikuwa na magari baba yangu alikuwa hataki kuona watoto tunajua kuendesha lakini kwa vile mjomba alikuwa na gari na mwanae alikuwa anajua aliweza kunifundisha na nikawa najua na sikuwahi kuendesha gari la baba alikuwa haruhusu mpaka anafirisika, Sasa kulingana na ufinyu wangu wa mda kuna nyumba ilikuwa inauzwa huo mkoa anaoenda kuwekeza nikampa pesa zingine ili akamilizie kunilipia na achukue document zote kwa niaba yangu na aninunulie viwanja kadhaa ambavyo tayari nilikuwa kwenye mawasiliano na wauzaji.

Kipindi chote tukawa tunawasiliana na kumuweka karibu na wale wauzaji na nyumba na viwanja ili kuhakikisha anavinunua na kuhusu maendeleo ya miradi yake aliyofungua. Sikujua chochote ndani ya mwaka mzima mpaka pale mdogo wangu aliyekuwa anaingia kidato cha 2 na mwingine cha 4 kunipigia simu kwamba wamefukuzwa shule kwa sababu ya ada Ikabidi nishtuke kumpigia mzee kutaka kujua nini kimetokea maana moja ya makubaliano yetu ni watoto kulipiwa ada, bila matarajio alinijibu kiukali sana na kunitaka nilipe gharama zake za matunzo yangu alivyonilea, ikanibidi nianze kufuatilia kupata hati za nyumba na viwanja nilivomtuma aninunulie kufika pale kwenye nyumba na viwanja vyote vishauzwa na yeye amejenga nyumba nyingine ambayo anaishi na mwanamke mwingine na tayari Wana mtoto mzee kweli ni mhuni lakini sikutegemea atafikia kiwango hiki. Nilihisi kuchanganyikiwa, ilileta mgogoro kidogo kati yangu na yeye lakini niliradhimika kusamehe. Mzigo wa pale nyumbani watoto wa5 wote wako shule private baba yangu akawa hana mda nao tena.

Nikaingia kwenye majukumu mazito na magumu lakini mungu akanifungulia riziki kipato nilichokuwa nakipata kikawa si haba nikapambana nao mpaka wengine leo wako chuo na kuweza kujenga nyumba nzuri zaidi kwa ajili ya familia na nikafungua miradi pale nyumbani ili kuwezesha kupata pesa za matumizi madogo na kujikimu kwa familia, wakuu sikujua lengo la baba kwa kweli yaani alichukua kirikuu akasomba vitu vyote dukani mpaka leo haijulikani alipeleka wapi na mtaji wote wa biashara za mobile money transaction akachukua.

Kinachonifanya nimfungulie kesi ni hiki, nilinunua kiwanja mwaka juzi kwa 16m na yeye akiwa shahidi hati nikaiacha nyumbani kwa mama na mara kadhaa nimekuwa naisahau kuichukua mwezi January naenda kuweka uzio kwenye uwanja wangu nakuta kumeshajengwa, namuuliza aliyepo anasema ameuziwa na baba na hati anatoa ambayo niliyouziwa mimi mwanzoni kumuuliza mama anasema yeye alitunza kwenda kuangalia alipoiweka haipo, na Mimi nina familia nishachoka nitaka nimburuze mahakamani.

Kuna mda inafika kiwango cha uvumilivu kinaisha, ukisikia watu watu wanauana ni mambo Kama haya na hapa ndipo unapoona Kama Diamond hama mda na baba yake hapaswi kulaumiwa Hawa wazee wengine ni WAPUMBAVU mambo mengi nimeamua kufupisha, maana nahisi kumtwanga hata risasi huyu mke wake amerudisha nyuma sana kwenye uchumi wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivyo unavyo fanyiwa na Baba yako kuna watoto wengi zaidi wamefanyia hivyo wazee wao lakini hawakupelekwa mahakamani, Kwa upande mwingine kosa ni la kwako.

Baada ya kujua mapungufu ya mzee wako ilibidi uchukue tahadhari, haikufaa kuacha document muhimu kama hizo kwa Mama yako ungehifadhi kwingine.
Wazee wetu wanamapungufu yao... Ila ndio milango ya baraka inapopitia unaweza kuta kufanikiwa kwako ni kuyokana na kuvumilia kwako.

Ikitokea tu umemgusa utajikuta unaanguka kuliko kawaida... We komaa hela ipo tu, Usiruhusu ikugombanishe na mzee.

Ila kwa kumaizia, from now on fanya miradi ukishirikiana na wadogo zako wa chuo msaidiane ila mzee mjue jinsi ya kuishi nae bila kuwapiga tena tukio jingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akienda kumshtaki atapata haki yake, mjomba wangu aliwahi kuuza kiwanja changu, niliweka undugu pembeni, nikamsweka rumande, baadae akapelekwa gerezani, then mahakamani, ushahidi wote ulikuwepo, kiwanja changu kilirudi, ndugu zake walijicommit mahakamani kumlipa yule mnunuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo ni mjomba, Hapa unamzungumzia baba mzazi... Huwezi jua nan atakua upande wake kipind cha kufungua kesi....

Inawezekana akashinda kesi akapata hyo milion 16 ila maisha yake na familia yake baada ya hapo yasiwe the same.....

Atafute namna nyengne ya kusaidia familia yake bila kumshirikisha mzee wake... na siku nyengne vitu muhimu avihifadhi nyumbani kwake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sina neno zuri la kutumia zaidi ya kusema nimebahatika kuzaliwa na baba mpumbavu sana, mjinga na asiyejielewa, sina mantiki ya kumdharau baba yangu lakini mpaka hapa nilipofika Sina budi kusema ni mjinga na imefika hatua namchukia kwelikweli Kuna misemo mingi ya wahenga kuhusu wazazi lakini wengine ni gundu, Mimi pia ni baba wa watoto 4 lakini huyu mzazi wangu hafai kuigwa na mzazi yeyote aliye smart.

Stori ni ndefu sana hapa naifupisha kidogo, Huyu baba yangu hana maisha ya dhiki ni mtu mwenye uwezo wa kufanya chochote anachotaka pamoja ya kuwa na miradi hajawahi kuishirikisha familia na hakuna anaejua miradi yake ilipo hata Mimi pamoja na kusikia tu kwa watu sijawahi kumuuliza na wala hilo halijawahi kuwa tatzo kwangu na wadogo zangu.

Tatizo ni hili,Kuna kipindi baba yangu alifirisika alichoka sana kiuchumi, kipindi hicho Mimi nilikuwa vizuri kiuchumi baada ya kumaliza chuo wajomba zangu waliniwezesha nikawa nina miradi ambayo ilikuwa inatoa profit nzuri kipesa na kiutafutaji nilikuwa mkoa tofauti na wazazi na tulikuwa karibu sana kimawasiliano. Siku moja Baba alinipigia simu akiniomba tuongee kwa kina , yalikuwa maongezi marefu lakini kikubwa alikuwa ananiambia amefirisika na gari zote alizokuwa nazo ameuza na alihitaji msaada wangu wa kuinua uchumi wake. Ilibidi nifunge safari kurudi nyumbani kwa wazazi ili tuzungumze vizuri sikutaka kufanya maamuzi nikiwa mbali nikiwa sijui ukubwa wa tatzo.

Na hii ndio ilikuwa mara ya kwanza kuongea na baba yangu kwa kina hakuwahi kunishirikisha kwenye mambo yake yoyote yale, tulizungumza kwa kina na ilikuwa siku nzuri sana kwetu na familia kiujumla tulifika muafaka kwa ustawi wa familia na wadogo zangu ambao walikuwa bado wako shule ambao walihitaji msaada zaidi kufika malengo yao na kwa vile pesa aliyoomba ilikuwa ndani ya uwezo wangu nilimpa mara 2 ya kile alichoomba nikamnunulia na gari la kutembelea, na hapa niseme ukweli pamoja na kwamba nyumbani kulikuwa na magari baba yangu alikuwa hataki kuona watoto tunajua kuendesha lakini kwa vile mjomba alikuwa na gari na mwanae alikuwa anajua aliweza kunifundisha na nikawa najua na sikuwahi kuendesha gari la baba alikuwa haruhusu mpaka anafirisika, Sasa kulingana na ufinyu wangu wa mda kuna nyumba ilikuwa inauzwa huo mkoa anaoenda kuwekeza nikampa pesa zingine ili akamilizie kunilipia na achukue document zote kwa niaba yangu na aninunulie viwanja kadhaa ambavyo tayari nilikuwa kwenye mawasiliano na wauzaji.

Kipindi chote tukawa tunawasiliana na kumuweka karibu na wale wauzaji na nyumba na viwanja ili kuhakikisha anavinunua na kuhusu maendeleo ya miradi yake aliyofungua. Sikujua chochote ndani ya mwaka mzima mpaka pale mdogo wangu aliyekuwa anaingia kidato cha 2 na mwingine cha 4 kunipigia simu kwamba wamefukuzwa shule kwa sababu ya ada Ikabidi nishtuke kumpigia mzee kutaka kujua nini kimetokea maana moja ya makubaliano yetu ni watoto kulipiwa ada, bila matarajio alinijibu kiukali sana na kunitaka nilipe gharama zake za matunzo yangu alivyonilea, ikanibidi nianze kufuatilia kupata hati za nyumba na viwanja nilivomtuma aninunulie kufika pale kwenye nyumba na viwanja vyote vishauzwa na yeye amejenga nyumba nyingine ambayo anaishi na mwanamke mwingine na tayari Wana mtoto mzee kweli ni mhuni lakini sikutegemea atafikia kiwango hiki. Nilihisi kuchanganyikiwa, ilileta mgogoro kidogo kati yangu na yeye lakini niliradhimika kusamehe. Mzigo wa pale nyumbani watoto wa5 wote wako shule private baba yangu akawa hana mda nao tena.

Nikaingia kwenye majukumu mazito na magumu lakini mungu akanifungulia riziki kipato nilichokuwa nakipata kikawa si haba nikapambana nao mpaka wengine leo wako chuo na kuweza kujenga nyumba nzuri zaidi kwa ajili ya familia na nikafungua miradi pale nyumbani ili kuwezesha kupata pesa za matumizi madogo na kujikimu kwa familia, wakuu sikujua lengo la baba kwa kweli yaani alichukua kirikuu akasomba vitu vyote dukani mpaka leo haijulikani alipeleka wapi na mtaji wote wa biashara za mobile money transaction akachukua.

Kinachonifanya nimfungulie kesi ni hiki, nilinunua kiwanja mwaka juzi kwa 16m na yeye akiwa shahidi hati nikaiacha nyumbani kwa mama na mara kadhaa nimekuwa naisahau kuichukua mwezi January naenda kuweka uzio kwenye uwanja wangu nakuta kumeshajengwa, namuuliza aliyepo anasema ameuziwa na baba na hati anatoa ambayo niliyouziwa mimi mwanzoni kumuuliza mama anasema yeye alitunza kwenda kuangalia alipoiweka haipo, na Mimi nina familia nishachoka nitaka nimburuze mahakamani.

Kuna mda inafika kiwango cha uvumilivu kinaisha, ukisikia watu watu wanauana ni mambo Kama haya na hapa ndipo unapoona Kama Diamond hama mda na baba yake hapaswi kulaumiwa Hawa wazee wengine ni WAPUMBAVU mambo mengi nimeamua kufupisha, maana nahisi kumtwanga hata risasi huyu mke wake amerudisha nyuma sana kwenye uchumi wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi ukienda mahakamani akafungwa... Ni nani atapata hasara.. na watoto wako watakuchukuliaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa ndgu siwezi kuwa mpumbavu namna hii, katelekeza familia miaka zaidi ya 6 nahangaika kusomesha watoto wake bado kuna mengi nimesahe yeye ameenda kuchukua mwanamke ana watoto wakubwa wa wanaume wenzake kamjengea nyumba nzuri kwa jasho langu na miradi huku wanae, nimuache Mali zangu zifaidishe ukoo mwingine huku wadogo zangu wanateseka

Sent using Jamii Forums mobile app

Wachukue wadogo zako uwatunze

Wazazi wanachokudai hakithaminiki kwa kiasi chochote cha thamani ya mali kama wewe ni mtu wa shukrani
 
Ishi na wazazi wote kwa tahadhari. Hapo mwenye makosa ni wewe kujali kupitiliza. Weka kipimo chini ya nusu sio kujaa pomoni hata wao walilelewa.
 
Back
Top Bottom