Nakusudia kumshtaki baba yangu

Nakusudia kumshtaki baba yangu

Sifa moja ya mwanaume mkuu ni ku-handle mambo magumu kama haya. Kwanza nakupongeza kwa kuwa tajiri wa hata kuweza kulipa 10m kwa wadogo zako ili wasome. Wewe ni shujaa usiyeimbwa hakuna baya utafanya kwa huyo mzee umkomoe ila tu msamaha na kuachana naye ni njia nzuri sana ya kukuepusha na mabalaa mengine.

Fikiria umechukua maamuzi mabaya kwake tuseme ameondoka duniani, unadhani utakuwa umesolve tatizo au umetengeneza tatizo la kujirudia katika ukoo wako? Umewaza kwa kiasi gani wadogo zako huomba Mungu ili uwe na afya njema ili mambo yao yaende, nadhani hujajua umuhimu wako kwa familia ndiyo maana unajikuta unawaza hata kuandikwa na vyombo vya habari kwa maamuzi mabaya unayoweza kufanya.

Je uko tayari msingi wa maisha yako ubomolewe na huo upumbavu wa huyo mzee? Jibu ni hapana wewe ni mwanaume yaani hapa ndipo sehemu pekee ya kuonesha watu wanaokutegemea kuwa wana kiongozi mahiri ambaye anaongoza vyema chombo chao hata wapitapo katika bahari chafu.

Familia nyingi sana ambazo ni masikini hata zile zenye uwezo mzuri kimapato zina migogoro hasa na wazee wao. Kila mtu hawezi kuandika hapa mkuu ila mimi huyu ninaeandika hapa nina matatizo same to you ila nimekuwa mpumbavu. Ili kujenga familia yangu ambayo itakuja kuniita baba/kaka, mjomba n.k.

Hutakiwi uwe na maamuzi katika hasira uliyonayo sasa.

Mkuu achana na mambo ya kuandikwa kwenye vyombo vya habari mimi nina mengi ya kuongea na wewe, nimekaa muda natype hapa kwa ajili yako usikengeuke huyo mtu mpumbavu akakuweka kwenye matatizo makubwa.
Mkuu Black Night kiukweli nilikuwa nimefikia point mbaya ya maamuzi hii reply imenifanya niwaze tofauti. Anyway mungu ni mwema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usijaribu kamwe kumshitaki BABA yako mzazi, hakika chochote utakachomfanyia kitajirudia kwako, mhehimu, kwepana nae upate kuyasukuma na kumaliza maisha yako vema,

Yaonekana wote ni wajasriamali wazuri ISIPOKUWA kuna kakilema ndani ya damu yenu fatilia huko nyuma pia, mtihani huo
 
Sina neno zuri la kutumia zaidi ya kusema nimebahatika kuzaliwa na baba mpumbavu sana, mjinga na asiyejielewa, sina mantiki ya kumdharau baba yangu lakini mpaka hapa nilipofika Sina budi kusema ni mjinga na imefika hatua namchukia kwelikweli Kuna misemo mingi ya wahenga kuhusu wazazi lakini wengine ni gundu, Mimi pia ni baba wa watoto 4 lakini huyu mzazi wangu hafai kuigwa na mzazi yeyote aliye smart.

Stori ni ndefu sana hapa naifupisha kidogo, Huyu baba yangu hana maisha ya dhiki ni mtu mwenye uwezo wa kufanya chochote anachotaka pamoja ya kuwa na miradi hajawahi kuishirikisha familia na hakuna anaejua miradi yake ilipo hata Mimi pamoja na kusikia tu kwa watu sijawahi kumuuliza na wala hilo halijawahi kuwa tatzo kwangu na wadogo zangu.

Tatizo ni hili,Kuna kipindi baba yangu alifirisika alichoka sana kiuchumi, kipindi hicho Mimi nilikuwa vizuri kiuchumi baada ya kumaliza chuo wajomba zangu waliniwezesha nikawa nina miradi ambayo ilikuwa inatoa profit nzuri kipesa na kiutafutaji nilikuwa mkoa tofauti na wazazi na tulikuwa karibu sana kimawasiliano. Siku moja Baba alinipigia simu akiniomba tuongee kwa kina , yalikuwa maongezi marefu lakini kikubwa alikuwa ananiambia amefirisika na gari zote alizokuwa nazo ameuza na alihitaji msaada wangu wa kuinua uchumi wake. Ilibidi nifunge safari kurudi nyumbani kwa wazazi ili tuzungumze vizuri sikutaka kufanya maamuzi nikiwa mbali nikiwa sijui ukubwa wa tatzo.

Na hii ndio ilikuwa mara ya kwanza kuongea na baba yangu kwa kina hakuwahi kunishirikisha kwenye mambo yake yoyote yale, tulizungumza kwa kina na ilikuwa siku nzuri sana kwetu na familia kiujumla tulifika muafaka kwa ustawi wa familia na wadogo zangu ambao walikuwa bado wako shule ambao walihitaji msaada zaidi kufika malengo yao na kwa vile pesa aliyoomba ilikuwa ndani ya uwezo wangu nilimpa mara 2 ya kile alichoomba nikamnunulia na gari la kutembelea, na hapa niseme ukweli pamoja na kwamba nyumbani kulikuwa na magari baba yangu alikuwa hataki kuona watoto tunajua kuendesha lakini kwa vile mjomba alikuwa na gari na mwanae alikuwa anajua aliweza kunifundisha na nikawa najua na sikuwahi kuendesha gari la baba alikuwa haruhusu mpaka anafirisika, Sasa kulingana na ufinyu wangu wa mda kuna nyumba ilikuwa inauzwa huo mkoa anaoenda kuwekeza nikampa pesa zingine ili akamilizie kunilipia na achukue document zote kwa niaba yangu na aninunulie viwanja kadhaa ambavyo tayari nilikuwa kwenye mawasiliano na wauzaji.

Kipindi chote tukawa tunawasiliana na kumuweka karibu na wale wauzaji na nyumba na viwanja ili kuhakikisha anavinunua na kuhusu maendeleo ya miradi yake aliyofungua. Sikujua chochote ndani ya mwaka mzima mpaka pale mdogo wangu aliyekuwa anaingia kidato cha 2 na mwingine cha 4 kunipigia simu kwamba wamefukuzwa shule kwa sababu ya ada Ikabidi nishtuke kumpigia mzee kutaka kujua nini kimetokea maana moja ya makubaliano yetu ni watoto kulipiwa ada, bila matarajio alinijibu kiukali sana na kunitaka nilipe gharama zake za matunzo yangu alivyonilea, ikanibidi nianze kufuatilia kupata hati za nyumba na viwanja nilivomtuma aninunulie kufika pale kwenye nyumba na viwanja vyote vishauzwa na yeye amejenga nyumba nyingine ambayo anaishi na mwanamke mwingine na tayari Wana mtoto mzee kweli ni mhuni lakini sikutegemea atafikia kiwango hiki. Nilihisi kuchanganyikiwa, ilileta mgogoro kidogo kati yangu na yeye lakini niliradhimika kusamehe. Mzigo wa pale nyumbani watoto wa5 wote wako shule private baba yangu akawa hana mda nao tena.

Nikaingia kwenye majukumu mazito na magumu lakini mungu akanifungulia riziki kipato nilichokuwa nakipata kikawa si haba nikapambana nao mpaka wengine leo wako chuo na kuweza kujenga nyumba nzuri zaidi kwa ajili ya familia na nikafungua miradi pale nyumbani ili kuwezesha kupata pesa za matumizi madogo na kujikimu kwa familia, wakuu sikujua lengo la baba kwa kweli yaani alichukua kirikuu akasomba vitu vyote dukani mpaka leo haijulikani alipeleka wapi na mtaji wote wa biashara za mobile money transaction akachukua.

Kinachonifanya nimfungulie kesi ni hiki, nilinunua kiwanja mwaka juzi kwa 16m na yeye akiwa shahidi hati nikaiacha nyumbani kwa mama na mara kadhaa nimekuwa naisahau kuichukua mwezi January naenda kuweka uzio kwenye uwanja wangu nakuta kumeshajengwa, namuuliza aliyepo anasema ameuziwa na baba na hati anatoa ambayo niliyouziwa mimi mwanzoni kumuuliza mama anasema yeye alitunza kwenda kuangalia alipoiweka haipo, na Mimi nina familia nishachoka nitaka nimburuze mahakamani.

Kuna mda inafika kiwango cha uvumilivu kinaisha, ukisikia watu watu wanauana ni mambo Kama haya na hapa ndipo unapoona Kama Diamond hama mda na baba yake hapaswi kulaumiwa Hawa wazee wengine ni WAPUMBAVU mambo mengi nimeamua kufupisha, maana nahisi kumtwanga hata risasi huyu mke wake amerudisha nyuma sana kwenye uchumi wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana brother.

Jipe muda kwanza upoe hasira. Usifanye kwa hasira.

Ni kweli nia na sababu za kisheria za kumshtaki baba yako unazo, lakini nikushauri tu, busara ikuongoze.

Kwa sababu, kama nimekuelewa vema, baba alifilisika, na hayo ayafanyayo sasa ni kutapatapa ili abaki kwenye iwango vyake vya awali.

Nakusihi, fanya mchanganuo wa madai yako na ufungue madai kwa lengo la kurejesha maliza usifanye kumkomoa baba isije ikakugharimu baadaye ukajikuta tena wewe ndiye unaemlipia kumwokoa (kumbuka damu nzito kuliko maji).

Vile vile iwe funzo kwamba sasa ni wakati wa kusonga mbele kujisimamia mwenyewe na kumwacha mzee afanye maisha yake nawe umsaidie kutokea mbali.

Cha mwisho, mwoneahe utii tu, lugha uliuotumia kwenye aya ya kwanza ga uzi wako iishie humu na usimtamkie baba hata kama amekosa, nami naona kakukosea. Jipe moyo, kuwa na kifua, mudu hasira na busara ikuongoze salama.

Pole sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Black Night kiukweli nilikuwa nimefikia point mbaya ya maamuzi hii reply imenifanya niwaze tofauti. Anyway mungu ni mwema

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante sana kwa kuelewa. Sasa jipe muda wa kutafakari kipi kimeshikilia maisha yako kwa sasa ni hayo madeni ya mzee wako au wewe mwenyewe. Yaani bila kulipwa hilo deni huwezi kuendelea na maisha yako.

Kama maisha yako hayategemei hiyo pesa unayotaka kudai huyo mzee basi fanya kama umetoa sadaka hicho kiasi.

Bado sioni kama ni sahihi kupelekana na huyo mzee mahakamani ila jiulize tu kuwa bila hizo pesa ndogo unazomdai huwezi kuendelea na mambo yako? Kama unaweza achana naye ale hicho kidogo alichokwapua katika sehemu ya kikubwa chako.
 
Mkuu usitake nikutane Kama huna point ondoa ujuha wako hapa jinga wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu umeumia, tulia-tulia Mkuu.

Tunashauriwa kukaa kimya na kutofanya maamuzi tukiwa na maumivu.
Hayo yote uliyoandika ni kweli yanaumiza sana, na Ile kwamba mzee anahudumia familia nyingine ni kama mwiba kwenye kidonda, inauma sana. Lakini piga moyo konde, tulia.

Sio vyema kumuita baba yako kwa majina unayomuita hapa, ni kosa na ni dhambi mbele za Mungu.
Baba ni baba, hakosei- anapitiwa.
Mkuu ombi langu kwako tulia shusha pumzi kwanza. Baada ya muda utaweza kusamehe na maisha yataendelea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu siku zote hasira huenda isitende haki. Kuna jambo la kufanya, najua nia yako ni kumkomoa ila hautaweza kumkomoa kwa pigo la kumpeleka ktk vyombo vya sheria.

Una pesa za kuendesha maisha yako si ndivyo? Mpaka sasa unavyoona pasipo hivyo viwanja kuna kitu ambacho kimeharibu maisha yako? Utaingia mgogoro na Mzee ila kiuhalisia familia nzima itatikisika ktk hili.

Utamfunga ila watakuja wengi wakikwambia ulotenda ni kubwa, either jamii, ndugu ama marafiki. Ishu za mtoto na mzazi ni ngumu. Ni wewe ndie unayesikia uchungu, wao hawafeel vile ambavyo wewe unafeel. Sio ajabu kwao kuja kukwambia umekosea kumpeleka vyombo vya sheria.

Mimi nnachokushauri ni hiki, achana na mzee. Ikiwezekana kata naye mawasiliano kabisa. Hizo fedha zitatumika mwisho kabisa zitaisha. Mzee atakumbuka fadhila za nyuma zote alizotendewa, na hapo ndipo atakapomkumbuka mkewe wa kwanza na msaada wako.

Hatoweza kufanya lolote zaidi ya moyo wake kumuhukumu, ogopa saana moyo wako ujihukuku kwa mabaya uliyomfanyia mtu, hata usingizi huwezi ukaupata kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Naunga mkono!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sina neno zuri la kutumia zaidi ya kusema nimebahatika kuzaliwa na baba mpumbavu sana, mjinga na asiyejielewa, sina mantiki ya kumdharau baba yangu lakini mpaka hapa nilipofika Sina budi kusema ni mjinga na imefika hatua namchukia kwelikweli Kuna misemo mingi ya wahenga kuhusu wazazi lakini wengine ni gundu, Mimi pia ni baba wa watoto 4 lakini huyu mzazi wangu hafai kuigwa na mzazi yeyote aliye smart.

Stori ni ndefu sana hapa naifupisha kidogo, Huyu baba yangu hana maisha ya dhiki ni mtu mwenye uwezo wa kufanya chochote anachotaka pamoja ya kuwa na miradi hajawahi kuishirikisha familia na hakuna anaejua miradi yake ilipo hata Mimi pamoja na kusikia tu kwa watu sijawahi kumuuliza na wala hilo halijawahi kuwa tatzo kwangu na wadogo zangu.

Tatizo ni hili,Kuna kipindi baba yangu alifirisika alichoka sana kiuchumi, kipindi hicho Mimi nilikuwa vizuri kiuchumi baada ya kumaliza chuo wajomba zangu waliniwezesha nikawa nina miradi ambayo ilikuwa inatoa profit nzuri kipesa na kiutafutaji nilikuwa mkoa tofauti na wazazi na tulikuwa karibu sana kimawasiliano. Siku moja Baba alinipigia simu akiniomba tuongee kwa kina , yalikuwa maongezi marefu lakini kikubwa alikuwa ananiambia amefirisika na gari zote alizokuwa nazo ameuza na alihitaji msaada wangu wa kuinua uchumi wake. Ilibidi nifunge safari kurudi nyumbani kwa wazazi ili tuzungumze vizuri sikutaka kufanya maamuzi nikiwa mbali nikiwa sijui ukubwa wa tatzo.

Na hii ndio ilikuwa mara ya kwanza kuongea na baba yangu kwa kina hakuwahi kunishirikisha kwenye mambo yake yoyote yale, tulizungumza kwa kina na ilikuwa siku nzuri sana kwetu na familia kiujumla tulifika muafaka kwa ustawi wa familia na wadogo zangu ambao walikuwa bado wako shule ambao walihitaji msaada zaidi kufika malengo yao na kwa vile pesa aliyoomba ilikuwa ndani ya uwezo wangu nilimpa mara 2 ya kile alichoomba nikamnunulia na gari la kutembelea, na hapa niseme ukweli pamoja na kwamba nyumbani kulikuwa na magari baba yangu alikuwa hataki kuona watoto tunajua kuendesha lakini kwa vile mjomba alikuwa na gari na mwanae alikuwa anajua aliweza kunifundisha na nikawa najua na sikuwahi kuendesha gari la baba alikuwa haruhusu mpaka anafirisika, Sasa kulingana na ufinyu wangu wa mda kuna nyumba ilikuwa inauzwa huo mkoa anaoenda kuwekeza nikampa pesa zingine ili akamilizie kunilipia na achukue document zote kwa niaba yangu na aninunulie viwanja kadhaa ambavyo tayari nilikuwa kwenye mawasiliano na wauzaji.

Kipindi chote tukawa tunawasiliana na kumuweka karibu na wale wauzaji na nyumba na viwanja ili kuhakikisha anavinunua na kuhusu maendeleo ya miradi yake aliyofungua. Sikujua chochote ndani ya mwaka mzima mpaka pale mdogo wangu aliyekuwa anaingia kidato cha 2 na mwingine cha 4 kunipigia simu kwamba wamefukuzwa shule kwa sababu ya ada Ikabidi nishtuke kumpigia mzee kutaka kujua nini kimetokea maana moja ya makubaliano yetu ni watoto kulipiwa ada, bila matarajio alinijibu kiukali sana na kunitaka nilipe gharama zake za matunzo yangu alivyonilea, ikanibidi nianze kufuatilia kupata hati za nyumba na viwanja nilivomtuma aninunulie kufika pale kwenye nyumba na viwanja vyote vishauzwa na yeye amejenga nyumba nyingine ambayo anaishi na mwanamke mwingine na tayari Wana mtoto mzee kweli ni mhuni lakini sikutegemea atafikia kiwango hiki. Nilihisi kuchanganyikiwa, ilileta mgogoro kidogo kati yangu na yeye lakini niliradhimika kusamehe. Mzigo wa pale nyumbani watoto wa5 wote wako shule private baba yangu akawa hana mda nao tena.

Nikaingia kwenye majukumu mazito na magumu lakini mungu akanifungulia riziki kipato nilichokuwa nakipata kikawa si haba nikapambana nao mpaka wengine leo wako chuo na kuweza kujenga nyumba nzuri zaidi kwa ajili ya familia na nikafungua miradi pale nyumbani ili kuwezesha kupata pesa za matumizi madogo na kujikimu kwa familia, wakuu sikujua lengo la baba kwa kweli yaani alichukua kirikuu akasomba vitu vyote dukani mpaka leo haijulikani alipeleka wapi na mtaji wote wa biashara za mobile money transaction akachukua.

Kinachonifanya nimfungulie kesi ni hiki, nilinunua kiwanja mwaka juzi kwa 16m na yeye akiwa shahidi hati nikaiacha nyumbani kwa mama na mara kadhaa nimekuwa naisahau kuichukua mwezi January naenda kuweka uzio kwenye uwanja wangu nakuta kumeshajengwa, namuuliza aliyepo anasema ameuziwa na baba na hati anatoa ambayo niliyouziwa mimi mwanzoni kumuuliza mama anasema yeye alitunza kwenda kuangalia alipoiweka haipo, na Mimi nina familia nishachoka nitaka nimburuze mahakamani.

Kuna mda inafika kiwango cha uvumilivu kinaisha, ukisikia watu watu wanauana ni mambo Kama haya na hapa ndipo unapoona Kama Diamond hama mda na baba yake hapaswi kulaumiwa Hawa wazee wengine ni WAPUMBAVU mambo mengi nimeamua kufupisha, maana nahisi kumtwanga hata risasi huyu mke wake amerudisha nyuma sana kwenye uchumi wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
pole sana mzee Haya maisha nomaaaaaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asiluletee upuuzi mburuze mahakamani, humo hakuna cha laana wala nini.
 
Pole sana brother.

Jipe muda kwanza upoe hasira. Usifanye kwa hasira.

Ni kweli nia na sababu za kisheria za kumshtaki baba yako unazo, lakini nikushauri tu, busara ikuongoze.

Kwa sababu, kama nimekuelewa vema, baba alifilisika, na hayo ayafanyayo sasa ni kutapatapa ili abaki kwenye iwango vyake vya awali.

Nakusihi, fanya mchanganuo wa madai yako na ufungue madai kwa lengo la kurejesha maliza usifanye kumkomoa baba isije ikakugharimu baadaye ukajikuta tena wewe ndiye unaemlipia kumwokoa (kumbuka damu nzito kuliko maji).

Vile vile iwe funzo kwamba sasa ni wakati wa kusonga mbele kujisimamia mwenyewe na kumwacha mzee afanye maisha yake nawe umsaidie kutokea mbali.

Cha mwisho, mwoneahe utii tu, lugha uliuotumia kwenye aya ya kwanza ga uzi wako iishie humu na usimtamkie baba hata kama amekosa, nami naona kakukosea. Jipe moyo, kuwa na kifua, mudu hasira na busara ikuongoze salama.

Pole sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kwanza samahani Kama nimetumia lugha ngumu lakini jaribu kujiweka kwenye viatu vyangu Kuna mambo mengi sijaweka hapa, just imagine nilimpa 28m kuboost miradi yake, 30m ili amalizie kulipa malipo ya nyumba yangu, na 12m aninunulie viwanja alinunua kweli lakini Baadae akauza akajenga nyumba ambayo amemkabidhi kimada wake ambae amemkuta na watoto wawili wakubwa wako secondary anawasomesha yeye kwa mchango wa jasho langu ikiwa wanae/wadogo zangu Hana mpango nao tena.

Halafu ameuza tena kiwanja changu kwa 24m bila aibu ameenda kumfungulia miradi mingine huyo kimada wake wakati mama yangu aliyehangaika na Mimi Hana mradi huyu mzee ni MPUMBAVU acha tu nimuite hivo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama una uchungu sana kata tu mawasiliano naye.. Kumshtaki hapana usijaribu!
 
Ushamjua tabia yake bado unaendelea kumkabidhi mali,how?
Laana isiyo na sababu haimpigi mtu.
Nenda kamshtaki apigwe jela mchezo uishe.
Kuzaa sio tiketi ya kumlalia mtoto.
Mali zako wewe ni kwaajili yako na watoto wako
 
Ww yakwako mbona madogo hayo kunq wazee miyeyusho mbn dingi ako cha mtoto uyo kudhurumiwa kiwanja unampeleka mahakamani ujakutana na wazee miyeyusho ww jambo dogo sana hilo wwbpotezea tuu.

121.
 
Na wewe unaye sapoti senge na wewe pia ni senge. Mzazi akiwa vyovyote ni mzazi na huwezi mlipa chochote mzazi wako
Mmezaliwa na makahaba nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha sina mood ya kubishana nawe kwa leo nitafute siku nikiwa akili sawa na zako tuchafuane.

Macho yako yamezibwa hayaoni mbele kwa hizo ofa unazo pata kutoka kwa marafiki wa kiume wa mama yako.
 
Sina neno zuri la kutumia zaidi ya kusema nimebahatika kuzaliwa na baba mpumbavu sana, mjinga na asiyejielewa, sina mantiki ya kumdharau baba yangu lakini mpaka hapa nilipofika Sina budi kusema ni mjinga na imefika hatua namchukia kwelikweli Kuna misemo mingi ya wahenga kuhusu wazazi lakini wengine ni gundu, Mimi pia ni baba wa watoto 4 lakini huyu mzazi wangu hafai kuigwa na mzazi yeyote aliye smart.

Stori ni ndefu sana hapa naifupisha kidogo, Huyu baba yangu hana maisha ya dhiki ni mtu mwenye uwezo wa kufanya chochote anachotaka pamoja ya kuwa na miradi hajawahi kuishirikisha familia na hakuna anaejua miradi yake ilipo hata Mimi pamoja na kusikia tu kwa watu sijawahi kumuuliza na wala hilo halijawahi kuwa tatzo kwangu na wadogo zangu.

Tatizo ni hili,Kuna kipindi baba yangu alifirisika alichoka sana kiuchumi, kipindi hicho Mimi nilikuwa vizuri kiuchumi baada ya kumaliza chuo wajomba zangu waliniwezesha nikawa nina miradi ambayo ilikuwa inatoa profit nzuri kipesa na kiutafutaji nilikuwa mkoa tofauti na wazazi na tulikuwa karibu sana kimawasiliano. Siku moja Baba alinipigia simu akiniomba tuongee kwa kina , yalikuwa maongezi marefu lakini kikubwa alikuwa ananiambia amefirisika na gari zote alizokuwa nazo ameuza na alihitaji msaada wangu wa kuinua uchumi wake. Ilibidi nifunge safari kurudi nyumbani kwa wazazi ili tuzungumze vizuri sikutaka kufanya maamuzi nikiwa mbali nikiwa sijui ukubwa wa tatzo.

Na hii ndio ilikuwa mara ya kwanza kuongea na baba yangu kwa kina hakuwahi kunishirikisha kwenye mambo yake yoyote yale, tulizungumza kwa kina na ilikuwa siku nzuri sana kwetu na familia kiujumla tulifika muafaka kwa ustawi wa familia na wadogo zangu ambao walikuwa bado wako shule ambao walihitaji msaada zaidi kufika malengo yao na kwa vile pesa aliyoomba ilikuwa ndani ya uwezo wangu nilimpa mara 2 ya kile alichoomba nikamnunulia na gari la kutembelea, na hapa niseme ukweli pamoja na kwamba nyumbani kulikuwa na magari baba yangu alikuwa hataki kuona watoto tunajua kuendesha lakini kwa vile mjomba alikuwa na gari na mwanae alikuwa anajua aliweza kunifundisha na nikawa najua na sikuwahi kuendesha gari la baba alikuwa haruhusu mpaka anafirisika, Sasa kulingana na ufinyu wangu wa mda kuna nyumba ilikuwa inauzwa huo mkoa anaoenda kuwekeza nikampa pesa zingine ili akamilizie kunilipia na achukue document zote kwa niaba yangu na aninunulie viwanja kadhaa ambavyo tayari nilikuwa kwenye mawasiliano na wauzaji.

Kipindi chote tukawa tunawasiliana na kumuweka karibu na wale wauzaji na nyumba na viwanja ili kuhakikisha anavinunua na kuhusu maendeleo ya miradi yake aliyofungua. Sikujua chochote ndani ya mwaka mzima mpaka pale mdogo wangu aliyekuwa anaingia kidato cha 2 na mwingine cha 4 kunipigia simu kwamba wamefukuzwa shule kwa sababu ya ada Ikabidi nishtuke kumpigia mzee kutaka kujua nini kimetokea maana moja ya makubaliano yetu ni watoto kulipiwa ada, bila matarajio alinijibu kiukali sana na kunitaka nilipe gharama zake za matunzo yangu alivyonilea, ikanibidi nianze kufuatilia kupata hati za nyumba na viwanja nilivomtuma aninunulie kufika pale kwenye nyumba na viwanja vyote vishauzwa na yeye amejenga nyumba nyingine ambayo anaishi na mwanamke mwingine na tayari Wana mtoto mzee kweli ni mhuni lakini sikutegemea atafikia kiwango hiki. Nilihisi kuchanganyikiwa, ilileta mgogoro kidogo kati yangu na yeye lakini niliradhimika kusamehe. Mzigo wa pale nyumbani watoto wa5 wote wako shule private baba yangu akawa hana mda nao tena.

Nikaingia kwenye majukumu mazito na magumu lakini mungu akanifungulia riziki kipato nilichokuwa nakipata kikawa si haba nikapambana nao mpaka wengine leo wako chuo na kuweza kujenga nyumba nzuri zaidi kwa ajili ya familia na nikafungua miradi pale nyumbani ili kuwezesha kupata pesa za matumizi madogo na kujikimu kwa familia, wakuu sikujua lengo la baba kwa kweli yaani alichukua kirikuu akasomba vitu vyote dukani mpaka leo haijulikani alipeleka wapi na mtaji wote wa biashara za mobile money transaction akachukua.

Kinachonifanya nimfungulie kesi ni hiki, nilinunua kiwanja mwaka juzi kwa 16m na yeye akiwa shahidi hati nikaiacha nyumbani kwa mama na mara kadhaa nimekuwa naisahau kuichukua mwezi January naenda kuweka uzio kwenye uwanja wangu nakuta kumeshajengwa, namuuliza aliyepo anasema ameuziwa na baba na hati anatoa ambayo niliyouziwa mimi mwanzoni kumuuliza mama anasema yeye alitunza kwenda kuangalia alipoiweka haipo, na Mimi nina familia nishachoka nitaka nimburuze mahakamani.

Kuna mda inafika kiwango cha uvumilivu kinaisha, ukisikia watu watu wanauana ni mambo Kama haya na hapa ndipo unapoona Kama Diamond hama mda na baba yake hapaswi kulaumiwa Hawa wazee wengine ni WAPUMBAVU mambo mengi nimeamua kufupisha, maana nahisi kumtwanga hata risasi huyu mke wake amerudisha nyuma sana kwenye uchumi wangu

Sent using Jamii Forums mobile app

Damu yako ni ya Baba Mpumbavu, Mjinga na asiye jielewa! Regardless anachofanya mzazi huwa tunawasitiri na kujaribu tu wasitupe hasara!
 
Ww yakwako mbona madogo hayo kunq wazee miyeyusho mbn dingi ako cha mtoto uyo kudhurumiwa kiwanja unampeleka mahakamani ujakutana na wazee miyeyusho ww jambo dogo sana hilo wwbpotezea tuu.

121.
Mkuu mbona kiwanja tu ningekuwa nimeshasamehe hebu pitia comment vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jikatae kivyako hebu achana na huyo mshua atakupotezea muda tu

Fanya yako maana hata ukimdai n sawa na bure kudai mtu unaejua

hawezi kukulipa ni kupoteza muda wako bure tu,kesi ya madai ni yakijinga

sana tena inazidi kuwa ya kijinga mara 100 kama mdaiwa ni baba yako mzazi.
 
Back
Top Bottom