Mmm mkuu nimekuPMkidambinya,
Mkuu historia yako inafanana na yangu 100%. Mie nilikuwa nawathamini sana wazazi wangu, wadogo zangu na ndugu wote kwa ujumla. Nilianza harakati za kuwasaidia wadogo zangu kabla hata maisha yangu mwenyewe hayajasimama maana nilikuwa very naive. Niliamini kumsaidia mdogo wako au ndugu ni wajibu wangu na watakuja kunithamini au wananithamini kama ninavyowathamini.
Nilipata bahati ya kuishi nje ya nchi hivyo nilijitahidi kujinyima nilichokuwa nakipata na kukituma nyumbani kwa wazazi na shuleni kuwasaidia wadogo zangu issue za ada na mambo mengine. Niliporudi nchini nikabahatika nikapata kazi yenye hela nzuri. Nilizidisha kutoa misaada kwa wazazi na kwa kila ndugu aliyeniomba sikusita kumsaidia. Hamadi!!!! Siku hazilingani.
Kazini mambo yakaharibika, nikaachishwa kazi, nikafulia kinoma. Wadogo zangu washamaliza vyuo na mambo yao yapo juu ya mstari. Nilidhani watanisaidia, bwanaee hakuna hata mmoja aliyekumbuka wema wangu. Hadi wazazi wangu wakanigeuka, sikuamini. Nilitokea kumchukia kila mtu. Nilihangaika peke yangu, mke wangu alikuwa mjamzito na nilikuwa na mtoto wa darasa la kwanza, nilipata tabu sana.
Niliapa sitasaidia mbwa yoyote kwenye maisha yangu. Nimekaa karibia miaka miwili nahangaika bila msaada kutoka kwa ndugu. Marafiki pekee ndio walikuwa wananisaidia. Mungu ni mwema, tayari nimeshaanza kuyarudisha tena maisha yangu kwenye mstari.
Na tayari nishaanza kuwaona washaanza kujipendekeza. Kama ulivyosema hata mimi namshukuru Mungu amenisaidia kuwajua ndugu zangu walivyo. Sasa hivi ndugu zangu ni mke wangu na watoto wangu basi.
Eti nipe mchango wa ndoa, mzazi hata hajui mwanae yuko wapiMsukuma Original, Nimepitia machungu mengi sana ingawaje sijafikisha hata 37 years, Mungu alinifanya nikaajiriwa nikiwa na miaka 24 nilithaminiwa, nikapoteza ajira, yaliyonikuta sitoyasahau kamwe kwani nishatukanwa tusi zito huku mama mzazi akiangalia mwanawe akinitukana.
Nimeapa kutosaidia ndugu msaada wa kumtoa kimaisha zaidi ya kinafiki, marafiki ndio wananipigania, nakula kwao, Nalala, ninaumia maana sina ajira kwa sasa ila wameniambia nisikate tamaa yataisha. Mungu kunionesha mapema adui zangu kanisaidia sana, ashukuriwe Mungu!
Hapa napoandika huu ujumbe ni kuwa hao ndugu hawajui nipo wapi wala nakula nini ila utashangaa mzazi anakuambia nipe mchango wa ndoa! Kaka hiyo siku bila kuwa mzazi wangu wa kunizaa basi tusi ambalo nilitaka kumpatia sidhani kama angenitafuta tena. Hii dunia sio kabisa ndugu yangu, kwani ndugu utasikia wanakuambia kuwa sisi nduguzo kisa unazo mali, fulia ujue rangi zao.
Ilifikia hatua nilianza michakato ya kutafuta scholarship nikasome nje nipate uraia huko kwani hapa sina msaidizi au ndugu but sijakata tamaa, nikipata chance hiyo nasepa jumla...

Ebwanae eeh!Mzazi wa hivo Mimi siwezi kuwa na mawasiliano nae yaani huyo ni Kama paka na panya kwangu, nakushauri somesha wadogo zako na pambana nao mpaka wajitegemee ukiwaacha utakuja kuwa na mzigo mkubwa sana huko mbeleni.
Mimi michepuko huwa nahit and run siweki kibanda ni hatari sana, nimeshuhudia rafiki yangu wa damu tunafanya nae kazi hapa TPA nae Sasa kashatelekeza familia yake mke wake na mtoto wanauza ndizi barabarani ili wapate kula, yeye kaoa jikegume la huko Njombe kubwa Lina watoto wakubwa wako chuo halafu jamaa kawa MJINGA ukimshauri arudiane na familia yake mnakubaliana vizuri lakini akirudi nyumbani anamuelezea hilo jike lake halafu bila aibu linakufata kukuchamba.
Nililipiga bit kulizabua makofi na urafiki na huyu jamaa uliisha, ukikutana na mke wake akianza kukuelezea hakika ni huzuni alifurahia mume wake alipopata kazi bandari kumbe hakujua ndio tiketi yake kuingia motoni
Sent using Jamii Forums mobile app

Naomba mtag mwenye Uzi mkuu, niusome pia huo uziSio kweli ule uzi nimetoka kuusoma mda huu una miezi 10 tu tangu uandikwe acha kudanganya na hauko hivi japo jamaa anaweza kuwa ni huyu kwa asilimia nyingi na hapa anaonesha kukata tamaa na kwenye uzi wa mwanzo anaonesha kutafuta suluhu nadhani mambo yameshindikana
Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi Sina moyo wa uvumilivu mzee Kama huyo naachana nae kabisa na ndio sikubahatika kupata wazazi Kama hao.Umekaa na Baba yako miaka 20 Unashindwa kumuelewa tabia yake? tena afadhali huyo anakupigia na simu mnaongea! wengine anajiona Matawi, Haongei na Failure wa Shule, tena maskini, haya kwenye Misiba wapwa zake ndiyo wasemaji wakuu wenye akili. nyinyi mlio wake ni wasugua Masufuria ya Msibani na kutafuta kuni. kifupi nyumbani kwenu ni km Matahaira msio kuwa na Dira.
Km haitoshi unakuja likizo toka Shule Kabla ya kukaa, anakwambia ''Mbona unakuja bila taarifa? sababu tu umekuta ana gonga Menu nene na Kihawala chake Nyumbani kwenu! Ukipata Shule kali ambayo utapasua kuliko yeye, anakwambia Masomo hayo Magumu, ntapoteza hela zangu bure! anakutafutia vi-course vya hovyo!
Haya yamepita hayo, ameumwa sasa!!! mnamuuguza na kumpa hela, bado ana Mind na kurudi kwa michepuko na kuipa hela zako, hafurahi kuwa na wewe km anavopenda vitoto vya hawala haramu! mbele yenu, tena kwako mpaka mkeo anashangaa, anauliza mbona baba yuko hivi? huyo huyo Mzee kachoka anakwambia Mshauri mama yako nioe mwanamke mwingine! si niwazi hakutaki?
Unapomsaidia ki hivyo, ndiyo anaona wewe Fara kabisa hujitambui ulisharogwa na Dada zake akili imepotea ndo maana unafanya mambo ya kisenge. anakuona km takataka! huyo ungembana kisaikolojia mpaka ajambe cheche! hampigani wala kumpeleka Mahakamani sijui Polisi, Mfilisi kwa akili tu. halafu mtulize eneo moja ale ugali dagaa tu! hawapendagi Nyama hao! Usilogwe uendeleze miradi yake bali hamisha mtaji wake kijanja.
Ndio zipo mali za aina hiyo, ila kama mmoja wapo akifariki basi mwenye haki ya kwanza kurithi ni mmoja kati ya hao.Mkuu imekaaje hiyo?
Kuna mali ya mke kisheria ambayo haimuhusu mume?
Naomba ufafanuzi kidogo ili niunganishe dots.
Sent using Jamii Forums mobile app
Baba Mkuu kumbuka na Mazuri pia alokufanyia awali, wkt utotoni mnacheza karata!! halafu ujue wanaume wanarogwa mno, na michepuko, labda umsaidie umkomboe kutoka kwenye umateka wa mchepuko! hasa km baba akiwa na kijana Afya , Handsome, na hela fulani hivi wee!!!!Mimi Sina moyo wa uvumilivu mzee Kama huyo naachana nae kabisa na ndio sikubahatika kupata wazazi Kama hao.
Mzazi akiwa MJINGA familia nzima inakuwa hatarini kimuelekeo wa maisha kwenye maisha ni bora umtose MJINGA uokoe maisha ya wengi hakuna laana hapo kuliko kupoteza muelelekeo wa familia nzima kwa ajili yake
Sent using Jamii Forums mobile app
Nilimjibu kuwa unajua nilipo?Eti nipe mchango wa ndoa, mzazi hata hajui mwanae yuko wapi
Inatia hasira balaa
Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi ni mchangia mada sio muhusika mkuuBaba Mkuu kumbuka na Mazuri pia alokufanyia awali, wkt utotoni mnacheza karata!! halafu ujue wanaume wanarogwa mno, na michepuko, labda umsaidie umkomboe kutoka kwenye umateka wa mchepuko! hasa km baba akiwa na kijana Afya , Handsome, na hela fulani hivi wee!!!!
si unaona vidume maskini walivo salama, hakuna kushobokewa na wanawake michepuko? ale nini mtu ana baiskeli tu.... familia zao?
Kumbuka na wewe ni mwanaume unaelekea huko! hapo ujue kuna baadhi ya Mashangazi zako wanamuonea wivu Mama yako! watamshauri babako aoe ttu! ili nyie na mama yenu mkose maisha. mtaabike. ...mchawi ndugu paka katumwa!
kuwakomesha tafuta Mpunga hasa uwe hata mara kumi yake ndo dawa!
Ukute kaoa MmachameKosa pia alifanya hapo. Hii ya kuacha hati kwingine na yeye yupo eneo tofauti ni mbaya sana.