Nakusudia kuishtaki Serikali (TCRA) kuzima Simcard za wateja wa mitandao

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,843
Kwanza ni kinyume cha Katiba ya uhuru wa kupata mawasiliano, pili ni uhujumu uchumi kwa serikali yenyewe na tatu kuzuia wananchi kupata habari kupitia mitandao ya kijamii. Kesi inafunguliwa jumatatu kanda ya Dar es Salaam.

Mimi sio wakili ila nimewasiliana na mawakili wangu 3 na tunakusudia kupeleka hoja za msingi mahakamani ili kuzuia watu zaidi ya milioni 24 kupoteza mawasiliano.



 
Na uhakika utakuwa mmoja wa wale wa tuma kwenye namba hii 😆😆😆😆😆, huu ni ushamba. Unachotakiwa kufanya ni kuomba, hata Mimi ukifungua Kesi na Mimi nakufungulia kwa kuwaibia Watanzania kwa kutumia cm.
 
Mkuu, mbali na kusudio lako la kutaka kuishitaki serikali, lkn uharaka wa kukimbilia kuzima namba ambazo hazijasajiliwa kidijikali kupitia "finger print" na namba ya kitambulicho cha uraia kitilewacho na NIDA zinaleta usumbufu na adha kubwa kwa raia wengi. Licha ya sababu za kiuchumi ambazo umezigusia, pia hakukuwa na ulazima wowote wa kukimbilia kufanya siku ya tarehe 20-01-2020 kupitia tamko la Rais.

Kwanza kwa upande wa serikali yenyewe inaonyesha dhahiri kabisa hakukuwa na matayarisho ya kutosha ktk kuvitoa vitambulisho hivyo. Bali pia kwa upande wa raia, hakukuwa na muamko wa kutosha ktk kuhakikisha kuwa kila mtu anamiliki kitambulicho chake cha taifa. Nafikiri mchakato wa kukipata kitambulicho hiki umekuwa mgumu mno na hauleweki vya kutosha, kiasi kwa watu wengi wanajikuta wakikosa fursa ya kuwa na kitambulicho hiki muhimu.

Nipende kuhitimisha kwa kusema hakuna ulazima wala sababu yoyote ile nyeti na pia yenye mantiki ya kukimbilia kuzizima simu zisizo sajiliwa kwa mfumo huu. Rai yangu ni kuwa, bado busara ionekane mbele ya watawala kuongeza muda wa usajili ili pande zote mbili zijipange na kujiandaa vyema ili zoezi husika likapate kufanyika kwa ufanisi uliokusudiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahakama ya Tanzania huwa haishughuliki na vitu ambavyo ni hypothetical. Nakuomba usipoteze muda.(pingamizi la kwanza)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…