Nakusudia kuishtaki Serikali (TCRA) kuzima Simcard za wateja wa mitandao

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,954
48,751
Kwanza ni kinyume cha Katiba ya uhuru wa kupata mawasiliano, pili ni uhujumu uchumi kwa serikali yenyewe na tatu kuzuia wananchi kupata habari kupitia mitandao ya kijamii. Kesi inafunguliwa jumatatu kanda ya Dar es Salaam.

Mimi sio wakili ila nimewasiliana na mawakili wangu 3 na tunakusudia kupeleka hoja za msingi mahakamani ili kuzuia watu zaidi ya milioni 24 kupoteza mawasiliano.


Sheria ya mawasiliano cap 306 ya 2010 kifungu Cha 93 ibara ndogo ya ii inatambua vitambulisho vinne katika usajili wa simu, na hili limetiliwa mkazo kwenye barua ya mkurugenzi wa tcra ya tarehe 17 July 2017

Vitambulisho vinavyokubalika kisheria Ni National I'd, TIN, driving licence na passport. Hivyo ukifungia laini iliyokidhi hivyo vigezo unaweza shitakuwa na kulipa faini na fidia kulingana na jedwali lililowekwa na mamlaka husika. Hivyo kuweni makini.

Hakuna sheria inayosema lazima usajili kwa NIDA, sheria unasema lazima line isajiliwe kwa kitambulisho kinachotambulika. Na vitambulisho hivyo vimeainishwa kisheria katika sheria namba 306 ya Mwaka 2010.

Unaweza kujiuliza maswali 200,na usipate jibu hata moja juu ya taifa la Tanzania hasa watu wake.

Hivi hawa ni Binadamu kutoka sayari hii ya Dunia au ni viumbe kutoka Planet X?

Binadamu aliyekamilika ni lazima awe na kumbukumbu za kutosha juu ya kila Tukio analopitia.

Tanzania hii hakuna tena anayekumbuka juu ya vitambulisho vya kupigia kura na Driving Licence kuwa vyote vina mfumo wa Biometric (unaohifadhi alama za vidole).

95% ya Watanzania wana vitambulisho vya kupigia kura vyenye mfumo wa Biometric sawa tu na Vitambulisho vya Taifa, lakini leo hii eti hivyo Vitambulisho havitakiwi kusajilia line za simu hadi viwe Vitambulisho vya Taifa.

Eti lengo ni kudhibiti uhalifu, sasa binadamu mmoja ana fingerprints ngapi kama ID za kura ambazo pia zilipatikana kama Vitambulisho vya Taifa kwa njia hiyo hiyo ya alama za vidole leo tena havifai?

Wenye akili wameshasoma mchezo, kuna kitu kinatafutwa hapo, kwa sababu fingerprints tayari watu walishachukuliwa kwenye Vitambulisho vya kura na Driving Licence, sasa kuna haja gani ya kutesa watu kiasi hiki?

Details za kila raia na fingerprints zake zipo Tayari kupitia Vitambulisho vya kura. Taifa lenye mamilioni ya wajinga wamesahau kuwa information zao zilishachukuliwa na fingerprints pia.

Neno la Mungu katika Kitabu cha Mithali linasema "Mwanangu mtafute sana Elimu na wala Usimwache aende zake”.

Poleni Watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza ni kinyume cha katiba ya uhuru wa kupata mawasiliano, pili ni uhujumu uchumi kwa serikali yenyewe na tatu kuzuia wananchi kupata habari kupitia mitandao ya kijamii. kesi inafunguliwa jumatatu kanda ya Dar es salaam.

Mimi sio wakili ila nimewasiliana na mawakili wangu 3 na tunakusudia kupeleka hoja za msingi mahakamani ili kuzuia watu zaidi ya milion 24 kupoteza mawasiliano.
Na uhakika utakuwa mmoja wa wale wa tuma kwenye namba hii 😆😆😆😆😆, huu ni ushamba. Unachotakiwa kufanya ni kuomba, hata Mimi ukifungua Kesi na Mimi nakufungulia kwa kuwaibia Watanzania kwa kutumia cm.
 
Mkuu, mbali na kusudio lako la kutaka kuishitaki serikali, lkn uharaka wa kukimbilia kuzima namba ambazo hazijasajiliwa kidijikali kupitia "finger print" na namba ya kitambulicho cha uraia kitilewacho na NIDA zinaleta usumbufu na adha kubwa kwa raia wengi. Licha ya sababu za kiuchumi ambazo umezigusia, pia hakukuwa na ulazima wowote wa kukimbilia kufanya siku ya tarehe 20-01-2020 kupitia tamko la Rais.

Kwanza kwa upande wa serikali yenyewe inaonyesha dhahiri kabisa hakukuwa na matayarisho ya kutosha ktk kuvitoa vitambulisho hivyo. Bali pia kwa upande wa raia, hakukuwa na muamko wa kutosha ktk kuhakikisha kuwa kila mtu anamiliki kitambulicho chake cha taifa. Nafikiri mchakato wa kukipata kitambulicho hiki umekuwa mgumu mno na hauleweki vya kutosha, kiasi kwa watu wengi wanajikuta wakikosa fursa ya kuwa na kitambulicho hiki muhimu.

Nipende kuhitimisha kwa kusema hakuna ulazima wala sababu yoyote ile nyeti na pia yenye mantiki ya kukimbilia kuzizima simu zisizo sajiliwa kwa mfumo huu. Rai yangu ni kuwa, bado busara ionekane mbele ya watawala kuongeza muda wa usajili ili pande zote mbili zijipange na kujiandaa vyema ili zoezi husika likapate kufanyika kwa ufanisi uliokusudiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza ni kinyume cha katiba ya uhuru wa kupata mawasiliano, pili ni uhujumu uchumi kwa serikali yenyewe na tatu kuzuia wananchi kupata habari kupitia mitandao ya kijamii. kesi inafunguliwa jumatatu kanda ya Dar es salaam.

Mimi sio wakili ila nimewasiliana na mawakili wangu 3 na tunakusudia kupeleka hoja za msingi mahakamani ili kuzuia watu zaidi ya milion 24 kupoteza mawasiliano.
Mahakama ya Tanzania huwa haishughuliki na vitu ambavyo ni hypothetical. Nakuomba usipoteze muda.(pingamizi la kwanza)
 
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom